ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, May 6, 2012

SIMBA YAIFANYIA UNYAMA YANGA YAIBANJUA 5-0


Mchezaji wa timu ya Simba mganda Emmanuel Okwi akishangilia goli mara baada ya kuifungia timu yake goli la kuongoza katika mchezo wa kumaliza michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom inayomalizika leo kwenye uwanja wa Taifa huku ikiwa tayari ni mabingwa wa ligi hiyo, Hivi sasa ni kipindi cha pili Simba inaongoza 5-0 dhidi ya Yanga.
Goli la pili la Simba limefungwa na mchezaji Felix Sunzu kwa njia ya penati na dakika chache zilizopita tayari Emmanuel Okwi ameongeza goli la tatu , Juma Kaseja ameongeza goli moja wa penati wakati pia Patrick Mafisango amefunga goli la tano baada ya wachezaji wa Yanga kufanya makosa katika eneo la hatari 
Mchezaji wa Simba Emmanuel Okwi akiwania mpira mbele ya Shadrack Nsajigwa wa Yanga katika mchezao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania inayomalizika leo.
Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia timu yao.
Mashabiki wa timu ya Yanga wakiangalia kitu jukwaani haikufahamika lilikuwa ni tukio gani.
Wachezaji wa timu za Simba na Yanga wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.
Kikosi cha timu ya Simba ambao ndiyo mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom 2011-2012 kikiwa katika picha ya pamoja na Kocha wao Milovan.
Manahodha wa Simba na Yanga Juma Kaseja kushoto na Shadrack Nsajigwa wakisalimiana mbele ya waamuzi kabla ya kuanza kwa mpambano huo.
Mashabiki wa timu ya Simba wakiwa wamefurika uwanjani hapo.

Picha kwa hisani ya FULL SHANGWE

No comments: