ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 14, 2012

TAMKO LA KUKANUSHA MH LETICIA NYERERE KUKAMATWA


Mh. Leticia Nyerere (Mbuge Viti Maalum)
CHADEMA.


Kulikua na Habari zilizoenea kwenye mtandao wa Jamii Forum kwamba Mh. Mbuge Leticia Nyerere amekamatwa na Uhamiaji kwa kukiuka masharti ya Green Card, Vijimambo ilimtafuta Mh. Mbuge na kumuuliza kulikoni.na haya ndio aliyosema:


NAPENDA KUCHUKUA NAFASI HII KUKANUSHA VIKALI TAARIFA ILIYOSAMBAZWA KUPITIA JAMII FORUMS KWAMBA MH LETICIA NYERERE AMEKAMATWA. KWA KWELI HIZI TAARIFA SI ZA KWELI. NI ZA UZUSHI NA KUTAKA KUCHAFUANA. TUNALAANI VIKALI KWA MTU YEYOTE ALIYEHUSIKA NA KUENEZA TAARIFA HIZI ZA KIZUSHI ZISIZOKUWA NA MSINGI WOWOTE.


6 comments:

mkereketwa said...

KWANZA NINAANZA KWA KUMPATIA POLE MSHESHIMIWA LETICIA.VILEVILE NINGEPENDA KUTOA ONYO KALI KWA CCM KWA KUTAKA KUTUMIA MBINU ZAO CHAFU,MUDA WA UFISADI UMEPITATUMIENI NGUVU ZA HOJA.PIA WALE VIBARAKA WANAOTUMIWA NA CCM TUNAWAFAHAMU KWA HIYO MIMI NA WATANZANIA WOTE TUNAKUOMBENI MJIFUNZE KURUMBANA PASIPO KUTOFAUTIA:AKSANTE.

mkereketwa said...

nyie mnaotapatapa maji yamewafikia shingoni kwa nini msife kishujaa,badala yake mnaanza kumchafulia muheshimiwa wetu jina.MKOME KABISA;

Anonymous said...

Ni kweli hakukamatwa kwa ajili ya makosa ya green card, lakini alikamatwa kwa ugomvi uliosababishwa na ulevi na akaswekwa ndani yeye na wenzie one night na kessy inaendelea kwa sharti kuwa asisafiri nje ya nchi, kama uongo akawashtaki jamii forum. Na hilo la green card linaangaliwa vile vile.

Anonymous said...

Jamani mbona watu mna roho mbaya hivyo.Kwani mtu akiwa na green card yake na sote tunajua umuhimu wake kuna tatizo gani hapo.TUACHE ROHO ZA WIVU JAMANI.

Anonymous said...

Mdau hembu fafanua.Unajua vitu vingine hata kama ni vyaukweli tutashindwa kuviamini kama havina maelezo na uthibitisho wa kutosha.Ugomvi uliosababishwa na ulevi wapi marekani au tanzania? na alizuiwa na nani? manake unaweza kuzuiwa kusafiri endapo tu umefanya kosa kubwa sana la jinai na sio kisa umegombana na mtu barabarani,na pia wewe ulikuwa wapi kushuhudia kama sio mlevi pia?Kama ni kweli basi huo uheshimiwa wote ni aibu tupu.

Anonymous said...

Huyu dada ni mtu mzima si angejituliza jamani, watanzania amueni kitu kimoja, kama mnataka Madaraka ya Nchi yetu si mrudi TZ mkaitumikie nchi yenu, hamueleweki mara yuko USA mara CHADEMA ndo maana anapatwa na matatizo kama hayo. Mara watoto wake anawaachia Wakanengue Viuno na Muibaji kwa jina na Linah. Loo!! wewe Leticia unaliharibu jija na Mheshimiwa Maarufu ambaye angekuwa hai angesikitika sana kuona Wajuu zake wanavaa nusu Uchi na Kungengua Vioni. Ni aibu kwa dada mzima kama wewe ambaye ulitakiwa utulizane na kuwakanya Mabinti zako. Badala ya kusoma na kupata Elimu ya Juu unawashauri wanengue Viuono. Polee saana dada. Uwe na msimamo wa maisha yako yote haya hayatakupata.