Advertisements

Friday, April 25, 2014

SHEREHE ZA UZINDUZI WA SHINA LA (CCM) MARYLAND

Uongozi wa shina la (CCM) Maryland unawaalika wanachama wa ccm, wapenzi wa ccm na watanzania wote kwa ujumla kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa shina la (CCM) Maryland. Sherehe zitafanyika Tarehe 27 mwezi huu wa nne, 2014 katika ukumbi wa Tabeer Restaurant kuanzia saa 10 jioni mpaka saa 2 usiku. Kutakua na chakula, vinywaji pamoja na viburudisho vya aina mbalimbali.
Pia kwa wale watakaopenda kujiunga na shina hili, form za uanachama zitatolewa siku hiyo.
Binadamu Wote ni sawa!! Karibuni waTanzania Wote tusherehekee!!
Tangazo Limetolewa na UONGOZI wa Shina (CCM) Maryland.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi!

22 comments:

Anonymous said...

Kukosa kazi kunatia imani acha Tu !!

Anonymous said...

Oooh not again

Anonymous said...

Ndugu zanguni. Hongereni sana kwa kujitahidi. Tutaendelea kujitangaza kwenye CCM HOYEEEEE ughaibuni na wengi wetu kwenye kamati na wajumbe hata maaratasi hatuna, kamwe hatupigi kura, ndg zetu kule nyumbani wanataabika uongozi umehodhi kila kitu, vibarua vyetu haa mjini ndio hivyo vya Box! Mbona tukiitwa kwenye kuzungumzia DualCTZ, hamuonekaniiki kuunga mkono? Tuacheni ushabiki na tushauri hawa viongozi wanaokuja mambo ya kuijenga Tanzania sio kujidanganya na Oyeeeehhhh! Sawa tutakuja na aomba muweke muda wa maswali. Tafadhali liweke hewani DJL. Usibane mdau.

Anonymous said...

Kidumuu, zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM !! Vijana tunaahidi mbele ya chama mapinduzi tutakulinda mpaka kuufaX2 Mapinduzi ni bado mtoto mdogo tumepewa tukulee upate makamooo
Vijana tunaahidi mbele ya Chama mapinduzi tutakulinda mpaka kufa!! mnakumbukaga?

Anonymous said...

Hivi ilo Tawi la ccm hapa litagombea nyie mmezidi mnapenda sana madaraka

Anonymous said...

absolutely ridiculous...

Anonymous said...

Kuna watu wanatafuta cv ili wakirudishwa bongo watafute pa kutokea maana hapa unyamwezini walishaharibu. Luke usibanie

Anonymous said...

Nilidhani hili shina ni la jermantown mbona mnaliita la maryland??? Hebu tuelezeni ili tupate kuelewa. Au ndio usanii tu?

Anonymous said...

Tuacheni usanii jamani ukiangalia wote walioko kwenye huo mtandao ni matatizo matupu kwa kuwa walishakwama sana hapa mjini basi wameamua kutafuta vimajina ambavyo sidhani kama vitawafikisha mbali ni ushabiki tu na mimi nilikuwepo pale!! Mkiambia kupiga kura mtaenda?? Haya baada ya mkutano anzeni kongamano la serikali mbili na muweke mikutano!!!

Anonymous said...

Mbona kwenye jumuiya ya WATANZANIA HATUWAONI??? SISI NI WATANZANIA KWANZA THEN vinafata vinginevyo CCM CHADEMA DINI UKOO!! Onyesheni uzalendo kwanza kwa kuwa mstari wa mbele kwenye mambo ya jumuiya yetu ya WATANZANIA. Lets build a strong community. ACHENI USHABIKI. JUZI KULIKUWA NA DADA WA KIBONGO nasiwangu kawaletea madaktari na tunajua wengi wetu hapa hawana insurance na watu waliojitokeza ni wachache, tunataka tuone wanajumuiya wanaleta mambo ya maana kama haya si kukutana kunywa na kula na hakuna kuelimishana kwa jambo lolote la maana. Kuna issue nyingi sana kwenye jumuiya yetu we need to start thinking jinsi gani tutasaidiana kama watu wa mataifa mengine. KAMA UMEPATA KITU SHARE NA MWENZAKO TUACHE TABIA ZILIZOKITHIRI ZA KUFICHANA MAMBO YA MAENDELEO.
MUNGU IBARIKI TANZANIA

Anonymous said...

Pumba Tupu..Bongo hakuna maendeleo VYAMA, na hapa Nako mnatuletea VYAMA, WTF.

Anonymous said...

this is BS....lini tutajifunza??

Anonymous said...

Timu yooote hiyo ni kutafuta tu vijina lakini hakuna la maana kwenye Jumuiya wala hawaji. Vipi mmepewa kiasi gani jamani kutangaza VYAMA Ughaibuni au mmeahidiwa mshiko ndo maana tunaona matawi kibao yanafunguka tu America. Hatuna kazi ya kufanya nini??

Anonymous said...

Hahaha napita tu naomben kad na mimi

Anonymous said...

Kwani sikuna tawi la DMV tayari hapa tayari au mnawapiga changa la macho huko bongo waendelee kuwatumia hela za walala hoi

Anonymous said...

Nimependa uhuru na wazi hapa watu kutowa maoni yao.mimi binasfi sina interest,na kuburuzwa na ccm sitaki na siwezi makosa mengi wanafanya sasa ukisha jiunga na ccm unafungwa mdomo kiaina,I know better, I have to do better.

Anonymous said...

What is wrong with my fellow Tanzanians ambao mmetoa comments za kitoto? Some of the comments are so stupid that they don't deserve publication. Nilidhani wabongo wengi tulichukua fursa hii ya kuishi Marekani kujielimisha kidogo, lakini yaelekea baadhi wameridhika na elimu ya Sekondari au shule ya msingi waliyoipata kule TZ. Nasema hivyo kutokana na comments za kijinga kuwalaumu wenzetu ambao wanataka kujumuika (organize)kisiasa kwa kuwa wana CCM or whatever other party of their liking. Hapa Marekani unaweza kujiunga au kuanzisha organization/club yeyote ili mradi huvunji sheria. Wana-CCM wakitaka ni hiari yao, hata wapiga box nao wanaweza kuanzisha chama chao. Huyo Nesi au Ma-CPAs, MBAs, PHDs, Tano au Kumi Ladies etc. wote wana uhuru wa kuanzisha vyama vyao. Therefore, ni vyema kuacha ujinga wa kuwalaumu hao wadau wanoipenda CCM. Nyie mlio-comment mnapenda vyama au clubs gani? America is a free country! Besides, kukutana siyo ni kunywa na kula tuu, but is a great opportunity for networking folks!

Anonymous said...

Huyo mwandishi wa hapo juu watu wametoa maoni yao usiyaite ya kitoto kwa sababu wewe hukubaliani nayo au wewe ndio ccm? It ok let's people watowe maoni yao hata kama wewe binafsi huyapendi.

Anonymous said...

mdau wa hapo juu...watu wanatumia their first amendment rights. by the way hii issue ya kuanzisha matawi ya political parties in US, to me is absolutely ridiculous. we can do better than this crap.

Anonymous said...

Kila anayekimbilia ccm au kuanzisha tawi ujue huyo kaishiwa na sera,fikra finyu,anategemea mambo makubwa na uwezo hana,fikra za kinyonyaji...

Anonymous said...

Ujinga pamoja na matatizo yote bongo.. Nyie mnakuja kuchezea hela huku

Anonymous said...

Njaa mbaya wewe ,acha tu!! 1+1=2 lakini.ccm wanakwambia sema 6 huna jinsi ni.kukubali kuburuzwa.ili uweze kuishi ,inasikitisha