Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa UNDP nchini Tanzania Dk. Alberic Kacou akizungumza kwa niaba ya UNDP kuhusiana na kuzinduliwa kwa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 ambapo amesema huu sasa ni wakati kwa nchi za Afrika haswa zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara kujenga mazingira ya kuelekea mustakabali wenye uhakika wa chakula
Baadhi ya Mabalozi, Maafisa wa Serikali na Umoja wa Mataifa na Taasisi mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Ripoti hiyo.

Mshauri wa Uchumi UNDP Bw.Amarakoon Bandara akifanya 'presentation' ya Ripoti hiyo. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou, Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Mbene na Mkurugenzi wa UNDP Tanzania Bw. Phillipe Poinsot.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Mbene na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Dk. Alberic Kacou (kulia) wakifuatilia maoni ya Uchambuzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 kutoka kwa Maprofesa wa Vyuo vikuu nchini.
Dr. John Mduma akifanya majumuisho ya nini kifanyike kukabiliana matatizo ya uhaba wa chakula yanayolikabili bara la Afrika na Afrika Mashariki.
Profesa Joyce Kinabo wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine akieleza uhifadhi wa Chakula kwa ajili ya matumizi ya baadae.
Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya Maofisa wa Umoja wa Mataifa na Wadau wa Serikali wakichangia maoni yao kuhusiana na Ripoti hiyo.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Membe (MB) akisoma hotuba wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012. Kushoto ni Mkurugenzi wa UNDP Tanzania Bw. Phillipe Poinsot.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Mbene (MB) akikata utepe kuzindua rasmi Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou.
"Sasa imezinduliwa rasmi" Mgeni rasmi Mh. Janet Mbene na Dk. Alberic Kacou wakionyesha Ripoti hiyo kwa wageni waalikwa na waandishi wa habari.
Baadhi ya Wageni waalikwa wakipitia Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 kuelekea kwenye Mustakabali wenye uhakika wa Chakula kwa nchi za Afrika iliyozinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam. Picha na MO BLOG
No comments:
Post a Comment