Wabunge wa nchini Ukraine
wakizichapa kavukavu wakati wakiwa katika moja ya Kikao cha Bunge nchini
humo baada ya kupishana msimamo kuhusu matumizi ya Lugha ya Kirusi
wakitaka itumike katika Mahakama za nchi hiyo. Wabunge wa chama cha
Rais Viktor Yanukovich, wanataka lugha ya Kirusi ikubaliwe kama lugha
rasmi ya pili nchini humo jambo ambalo wabunge wa vyama vya upinzani
wanapinga vikali kupitishwa kwa sheria hiyo ambayo ingeruhusu lugha ya
Kirusi kutumiwa katika mahakama. |
No comments:
Post a Comment