Mkurugenzi wa UNDP Tanzania Bw. Phillippe Poinsot akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya kwanza juu ya hali ya kujitolea (SWVR) nchini Tanzania ambapo amesema ripoti hiyo ina umuhimu zaidi katika kuelewa umuhimu wa kujitolea katika maisha yetu na kuwa wanategemea itachangia kuboresha utamaduni wa kujitolea na kuwapa ujasiri zaidi watu wengi zaidi kuwa na nia hiyo. Pia ameshukuru Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kutoa mwongozo na nafasi ya kuwa na majadiliano yenye lengo la kuboresha mfumo wa kujitolea.
Meneja Mradi wa SWVR Bi. Aygen Aytac akifanya Presentantion juu ya maana, umuhimu na faida za kujitolea ambapo pia maefanya majumuisho ya jinsi utaratibu mzima ulivyofanyika kuandaa ripoti ya kwanza juu ya hali ya kujitolea (SWVR) nchini Tanzania.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Msaidizi wa Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk.Kisui Steven Kisui akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Dk. Fenella Mukangara kwenye uzinduzi wa ripoti ya kwanza juu ya hali ya kujitolea (SWVR) nchini Tanzania ambapo amesema mtazamo wa Tanzania ni kuona Uchumi wa kati unakua kufika mwaka 2020 sambamba na malengo ya maendeleo ya milenia.
Kama sehemu ya jitihada za Wizara hiyo katika kuboresha mpango wa kujitolea katika ngazi ya Taifa sambamba na malengo ya maadhimisho ya Kimataifa ya mwaka wa kujitolea inafikira kuandaa taratibu na sera zitakazotoa muongozo kwa wananchi kujizoesha utamaduni huo.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Msaidizi wa Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk.Kisui Steven Kisui (kushoto)akikata utepe kuzindua ripoti hiyo sambamba na Mkurugenzi wa UNDP Tanzania Bw. Phillippe Poinsot.
Sasa imezinduliwa rasmi. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Meneja Mradi wa SWVR Bi. Aygen Aytac (kulia) na Afisa Mipango wa United Nation Volunteers (UNV) Bi. Stella Karegyesa kushoto.
Burudani kutoka kikundi cha International Youth Fellowship (IYF).
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilomo cha Sokoine ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Young Tanzania for Community Prosperity (YTCP) Bw. Alfred Magehema akitoa mada wakati wa uzinduzi huo ambapo amewataka vijana wenzake kujitolea kusaidia jamii bila kujali malipo kwa kuwa tukifanya hivyo tutajenga Taifa litakaloweka mbele faida na kuacha nyuma utu.
Pichani Juu na chini ni Viongozi wa Taasisi mbalimbali za kiserikali, Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Wanafunzi kutoka vyuo na shule mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo.
Na.Mwandishi wetu
Programu ya Wanajitolea ya Umoja wa Mataifa (UVN) leo imezindua ripoti ya kwanza juu ya hali ya kujitolea (SWVR) nchini Tanzania.
Ripoti hiyo inaangalia michango ya muhimu katika maeneo mbalimbali kama vilemaisha endelevu, kushirikishwa kwa jamii, mshikamano wa kijamii na kupunguza hatari ya majanga.
Ripoti hiyo vile vile inatoa mtazamo mbadala wa jamii bora na inaonyesha jinsi ya kusukuma mbele shughuli za kujitolea.
SWVR pia inaeleza umuhimu wa kupima viwango vya kujitolea ili kuvijumuisha kwenye mojawapo ya rasilimali kubwa za mataifa.
Kutokana na utafiti, kazi yakujitolea imechangia asilimia 1.5 ya pato la taifa (GDP) mwaka 2008, wakati wastani kwenye nchi zilizoendelea ni asilimia 0.7 ya GDP.
SWVR ilitolewa kwa jamii ya kimataifa kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 5 Disemba 2011 na kuzinduliwa kwenye nchini (80) duniani.
Picha na Habari na MO Blog
No comments:
Post a Comment