ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 31, 2012

WANAUME WANAOONGOZA KWA KUVUNJA NDOA ZA WATU

NDUGU zangu, katika maisha ya sasa kuna watu flani ambao ukiona wana ukaribu uliopitiliza kwa mke wako, jua kuna jambo nyuma ya pazia na ukishangaashangaa unaweza kujikuta unamegewa penzi lako hivihivi.
Hiki nitakachokielezea leo nimekifanyia uchunguzi wa muda mrefu na kwa wale waliokumbana na hali halisi ya mambo, watakubaliana nami kwa asilimia zote. Juzi nilipata bahati ya kusuluhisha ugomvi wa rafiki yangu ambaye yeye na mkewe ni wafanyabiashara.

Chanzo cha ugomvi wao ni daktari mmoja ambaye inaonekana kwa muda mrefu amekuwa ‘akiitafuna’ ndoa yao na siku hiyo ndiyo ule msemo wa za mwizi arobaini ulipotimia. Rafiki yangu huyo alinasa sms kutoka kwa dokta huyo akitaka wakutane na mkewe siku hiyo.
Bahati ni kwamba, mwanaume huyo alikuwa akimpenda sana mke wake na hata nilipomshauri amsamehe waanze ukurasa mpya, alinielewa.
Lakini wakati hilo likitokea, jana yake nilisoma habari ya mke wa mtu aliyefumaniwa na kijana mmoja ambaye ni muuza genge mtaani kwao. Aibu ilioje kwa mwanamke huyo! Hivi inakuwaje mpaka mke wa mtu ambaye mume wake anahangaika juani kutafuta noti kisha mkewe huku nyuma anatoa penzi kwa muuza genge kirahisi? Hii inauma sana!
Matukio hayo mawili yalinifanya nifikie hatua ya kuandika makala haya juu ya watu wanaongoza kwa kusambaratisha ndoa za watu.
Muuza genge
Kuna tabia ambayo baadhi ya wanawake walio katika ndoa wanayo ya kubana matumizi yao ya kila siku kwa lengo la kuweka fedha za kufanyia mambo mengine baadaye.
Katika mazingira hayo wapo wanaojiweka karibu sana na watu hao wakiamini watapewa vitu vya bure kama vile nyanya, vitunguu nk. Wanawake wa sampuli hii wakikutana na wauza genge viwembe hawawezi kupona na ndiyo maana mwanaume anashauriwa kuwa makini sana na wauza magenge.
Mwalimu
Hapa nazungumzia zaidi walimu wa vyuoni. Baadhi yao wamekuwa wakiwarubuni wanawake kwa kuwaahidi kuwafaulisha kwenye mitihani na wamekuwa wakiwatishia kuwafelisha endapo watawachomolea. Hilo limekuwa likiwafanya baadhi ya wanawake wasio na msimamo kuwa tayari kwa lolote ili mradi wafaulu.
Dereva bajaji, teksi
Nani asiyejua kuwa baadhi yao wanaongoza kwa ukware? Kwa kifupi hawa ni miongoni mwa watu ambao mwanaume hatakiwi kukubali ukaribu uliopitiliza kwa wake zao kwani historia inaonesha wengi wao wamekuwa wepesi wa kuomba penzi hasa mazoea yanapovuka mipaka.
Muuza duka
Mama mmoja ambaye mume wake anafanya biashara za kusafiri mikoani alinaswa na mpangaji ambaye kwenye nyumba anayoishi mwanaume huyo ana duka. Baada ya tukio hilo ilibainika mama huyo alikuwa na tabia ya kuchukua vitu dukani hapo na siku hiyo alipotakiwa kulipa alimwambia kimasihara kuwa, yeye hana fedha kama vipi wamalizane kwa njia nyingine.
Kama mwanamke huyu alivyosema, wapo wake za watu ambao wamekuwa wakijirahisi sana kwa wauza duka wakijua itakuwa rahisi kwao kuambulia vitu vidogodogo na fedha. Kwa maana hiyo mkeo si wa kumruhusu kuwa na uhusiano wa karibu sana na wauza duka.
Mganga wa kienyeji
Wapo waganga wa kienyeji ambao ni wasanii tu. Katika hawa wanaodaiwa kuwa wasumbufu kwa wake za watu ni wale wanaojidai kutibu magonjwa ya kinamama.
Itaendelea wiki ijayo.

www.globalpublishers.info

1 comment:

Anonymous said...

Hapo Mpwa umesahau na ma-Dj wanawake wapenda starehe kupitiliza, hupenda kuingizwa bure malipo huwa hayohayo