ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 3, 2012

Yanayoweza kumfanya mumeo atembee na mashosti wako

NI wiki nyingine tena tunakutana kupitia safu hii nakiamini muwazima na mnaendelea vyema na majukumu yenu ya kila siku kama kawaida. Mimi nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwani amekuwa akiniongoza katika kila ninalolifanya katika maisha yangu.
Ndugu zangu, maisha ya kimapenzi yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu sana kwani kuna changamoto nyingi zinazoweza kujitokeza kiasi kwamba usipoangalia unaweza kuishia kusema hutakuja kumpenda mtu, heri uishi peke yako!

Tatizo kubwa ambalo limekuwa likiwasumbua wengi walio kwenye ndoa na wale walio kwenye uhusiano wa kawaida ni usaliti. Uaminifu umepungua kwa kiasi kikubwa, mke wa mtu kutembea na rafiki wa mumewe si kitu cha ajabu siku hizi, mume wa mtu kutembea na mpangaji mwenzake siyo ishu. Nashindwa kuelewa tunaelekea wapi.
Yaani imefika hatua ya mume wa mtu kutembea na ‘hausigeli’ wake tena anafanya hivyo kwenye kitanda anacholala na mkewe, hii si laana jamani? Usiulize kwa nini nimetoa mfano huu, hili limetokea juzi tu kwa mtu wangu wa karibu sana. Alitoka safari na aliporejea usiku akamfumania mumewe akiburudika na ‘hausigeli’, eti mwisho wa siku mwanaume anaomba asamehewe akidai ni shetani kampitia.
Anyway nimeona nianze na hilo ambalo lina uhusiano wa kile ninachotaka kukizungumzia leo. Kama nilivyotangulia kusema hapo mwanzo, imekuwa si jambo la ajabu kusikia mume wa mtu katembea na rafiki wa mke wake.
Wewe utakuwa ni shahidi wa hiki ninachokizungumza kwani kama hakijakutokea basi rafiki yako au ndugu yako kimempata.
Lakini katika uchunguzi wangu nimebaini baadhi ya wake za watu wamekuwa wakitengeneza mazingira ya waume zao kutembea na marafiki zao.
Unaweza kushituka kusikia hivyo lakini ndiyo ukweli wenyewe na utakubaliana na mimi baada ya kusoma vipengele vifuatavyo.
Ukaribu wa mume na marafiki wa mke
Kuna baadhi ya wanawake wamekuwa na tabia ya kuwaweka waume zao karibu sana na marafiki zao. Unakuta mwanamke eti anamruhusu mumewe kwenda klabu au baa na shosti wake. Katika mazingira hayo unatarajia nini?
Sisemi uanze kumfikiria tofauti rafiki yako lakini unachotakiwa kujua ni kwamba, sasa hivi kuna wasichana micharuko ambao ukiwapa nafasi kidogo tu kwa mumeo wanakupindua.
Kwa maana hiyo kitendo cha kumuweka mumeo karibu na mashosti wako unatengeneza mazingira ya kusalitiwa kwa kujitakia hivyo unatakiwa kuwa makini na watu ambao wanastahili kuwa karibu na laazizi wako.
Mawasiliano ya mume na marafiki wa mke
Sisemi marafiki zako wasiwasiliane kabisa na mumeo lakini unatakiwa kuangalia wanawasiliana kwa mambo gani? Utakuwa ni mtu wa ajabu kama utakubali mumeo apigiwe simu au achati na marafiki zako halafu hakuna cha maana wanachoongea, walahi utaula wa chuya!
Unatakiwa kuwa mkali pale unapoona mumeo anawasiliana sana na marafiki zako wa kike kwani waliosalitiwa walianza kuchukulia poa mazingira kama hayo mwishowe wakalia.
Mke kuanika siri za mumewe
Lingine ni tabia ya baadhi ya wanawake kuwasimulia mashosti wao siri ambazo hawastahili kuzitoa nje. Kuna wanawake sijui nisema ni ulimbukeni au ushamba!
Eti unamkuta mke anasimulia mashosti wake jinsi mumewe anavyompa furaha wanapokuwa faragha. Unajiuliza ni kwa nini mtu anafikia hatua hiyo.
Kimsingi hili ni kosa kubwa linalofanywa na baadhi ya wanawake na kujikuta wakikaribisha usumbufu kwa waume zao kutoka kwa wanawake micharuko.
Mwanamke kutochukua nafasi yake
Kwa kifupi mwanamke kushindwa kumdatisha mumewe ni kumfanya aangalie wapi kwingine anakoweza kupatiwa kile anachokihitaji.
Hili liwe fundisho kwa wanawake waliobahatika kuingia kwenye maisha ya ndoa. Kumridhisha mumeo ni kumfanya aepukane na vishawishi vinavyoweza kumfanya akusaliti.
Mpe mapenzi atosheke asifikiria kukusaliti, mpe kila anachokitaka kutoka kwako (ila usimruhusu kuruka ukuta). Hii itamfanya asiwe na tamaa ya kupoteza muda wake kwa marafiki zako ambao ni micharuko wanaotamani kuonja asali yako.
Ni hayo tu kwa leo, tukutane wiki ijayo.

www.globalpublishers.info

4 comments:

Anonymous said...

Hapo umenena kabisa. Yalinikuta hayo. Nilikuwa namsimulia rafiki maraha nayopewa,nikamwacha rafiki amzoee bwanangu hadi kuwa pamoja. Niliwaamini wakanigeuka.

Anonymous said...

Sijue wewe hapo juu ni dada au kaka!hujui kuwa rafiki ni mkia wa fisi?hujazaliwa nae tumbo 1 unafikiri atajali?hata uliezaliwa nae tumbo 1 saa nyingine anakugeuka.Usiamini mtu maana mchimvi hana ndui usoni!Huo ni uchawi!

Anonymous said...

Rafiki sio wa kuwaamini katika mapenzi yako,mie yalinikuta hayo,kidonda bado kibichiii hakijapona ingawaje ni masiku mengi,wala nilikua simuachi rafiki yangu na bwana wangu ila alikua anaona wivu mimi sihangaiki na wanaume kutwa yeye anabadilisha na alikua aanaona tunaaishi kwa raha,akaingia na gia za kusema uongo kuwa nina wanaume nje,anampa bwana wangu stori za uongo,nae akawa kama kichaa akamuamini kumbe bibie alikua anataka anipindue,aibu ikawa yake,kulambwa kalambwa,hakunitoa ng'ooo!anahangaika hapati bwana hata wa kumuweka ndani!na jamaa yangu tukasameheana niko nae hadi keshoooooo.

Anonymous said...

Hivi jamani mtu anakuamini na sukari wa moyo wake halafu unailamba,huoni haya,haswa wanawake,badilikeni hii ni tabia chafu sana,yapo na yanatokea mjini hapa sana tu.Halafu ukiangalia hamna faidaunauvunja utu wako na thamani duniani kwa sukari ambayo sio ya kudumu ni ya kupita tu,ovyooooooo.