Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwasili na ujumbe wake kwenye Uwanja wa ndege wa Bukoba, kwa ajili ya ziara ya siku moja ya kikazi mkoani Kagera ambako pamoja na shughuli nyingine alifungua Baraza la Vijana wa CCM, Wilaya ya Missenyi mkoani humo.
Nape akiwa na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Avelyne Mushi baada ya kuwasili
Nape akizungumza na viongozi katika Ofisi ya CCM mkoa wa Kagera
Nape akitoka katika ofisi hiyo baada ya mapokezi
Nape akitoa salam za Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kwenye msiba wa aliyekuwa mtumzishi wa siku nyingi, Balozi, Dk. Vedasto Kyaruzi, mjini Bukoba
Kijana wa CCM akimvisha skavu Nape. Kulia ni Mkt wa UVCCM mkoa wa Kagera, Revocatus Bubeye na Wapili kushoto ni Kamanda wa Vijana Kagera, Dioniz Malinzi
Nape na viongozi waliompokea wakiwasili kwenye kambi ya Baraza la Vijana wilaya ya Missenyi.
Nape akikata utepe kuingia kwenye uwanja wa Mashujaa, kuzindua Baraza hilo.
Msanii wa kundi la Nshomile Family la mjini Bukoba, Nazir Abdallah akitoa burudani kwenye kambi hiyo
Nape akimkabidhi cheti Kamanda wa Vijana mkoa wa Kagera, Dioniz Malinzi kwa kuwa mmoja wa waliowezesha kambi hiyo ya Baraza la Vijana
Kwa picha zaidi na maelezo Bofya Read More
Vijana waliopo kati ya Baraza la Vijana, Missenyi, wakimsikiliza Nape
Nape akimsalimia Simon Andrea ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Walemavu , wilaya ya Misenyi.
Nape akiagana na Viajana kwenye kambi hiyo
Baadhi ya viongozi kwenye kambi hiyo wakimpungia mkono Nape wakati akiondoka
Nape alipata fursa pia kucheza gofu kwenye viwanja vya mchezo huo vya Dioniz Malizni (kulia) nje kidogo ya mji wa Bukoba
Nape katika Gofu
Juu na chini Nape akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na baadhi ya ujumbe aliofuatana nao kwenye uwanja wa gofu
Mabaki ya kanisa lililolipuliwa kwa mabomu na Idi Amin eneo la Kyaka Bukoba
Mto Kagera mkoani Kagera
No comments:
Post a Comment