Mh, Asha-Rose Migiro anarudi nyumbani Tanzania baada ya kuitumikia UN kwa kipindi cha miaka 5. Mh Asha-Rose ni Mtanzania wa kwanza mwanamke kupata nafasi kubwa ya kufanya kazi katika Umoja wa Mataifa akiwa kama msaidizi wa Katibu Mkuu Ban Ki-Moon. Mh, Asha-Rose aliandaliwa hafla hiyo na uongozi wa Jumuia ya Watanzania hapa New York kama shukrani zao kwake ambaye alikuwa kama mlezi wa jumuia na alishirikiana na uongozi kwa hali na mali kila alivyo pata nafasi ya kufanya hivyo. Uongozi wa jumuia ya Watanzania New York unamtakia kila la kheri huko aendako na unategemea kuendelea kuwasiliana na kama mlezi.
Juu na chini ni Mhe. Asha Rose Migiro akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Jumuiya ya Watzanania New York. |
Mhe. Asha Rose Migiro akiongea jambo na Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania New York
Picha juu na chini ni Mhe. Asha Rose Migiro na Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania New York wakiendelea kupata chakula
Mama Asha-Rose Migiro akiwa na Shabani Mseba katibu wa Jumia ya Watanzania New York |
Bwana Chiume akiwa na Mama Asha Rose Migiro |
Ukodak Moment na Mama |
Mwenyekiti wa Jumuia ya Watanzania New York Haji Hamisi akiwa na Mama Asha-Rose Migiro |
NY Ebra wa Vijithings akiwa na Mama Asha-Rose Migiro |
Kijana katika Ofisi hii tunasimama hivi, inaonekana NY Ebra akielekezwa na Mama Migiro, Picha na Ny Ebra! mwakilishi wa vijimambo NY. |
No comments:
Post a Comment