ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 20, 2012

Kampuni ya Bookmaker Paddy Power kumlipia faini Nicklas Bendtner

Mkurugenzi wa kampuni ya Bookmaker Paddy Power amesema kampuni yake itamlipia mteja wake Nicklas Bendtner faini ya Euro 100,000 (743,000 Denish kroner). Mshambuliaji huyo wa timu ya Taifa ya Denmark, ambaye pia anachezea Arsenal F C ya Uingereza, alipata adhabu hiyo kwa kuonyesha mashabiki chupi yenye nembo ya PaddyPower wakati alipofunga goli dhidi ya Ureno katika michuano inayoendelea ya mpira wa miguu ya Ulaya.

Ken Robertson, mkurugenzi wa Paddy Power alisema ‘Bendtners analipwa mshahara mkubwa  kupita faini hiyo ya Euro 100,000, lakini kampuni imeamua kumlipia faini hiyo kutokana na kumjali mchezaji na kuonyesha chupi kwake ilikua ni staili yake ya kushangilia goli.

Hatudhanii Nicklas anapaswa kuadhibiwa kwa jambo hilo dogo, ukweli ilikuwa ni furaha ya kushangilia goli tu.

No comments: