Mtandao wa Ghafla Kenya umeripoti kwamba hii ishu imetokea wakati Big Brother alipotangaza kupiga marufuku pombe kwa washiriki ndani ya jumba hilo, Prezzo alishikwa hasira na kusema kwamba anaweza kuondoka muda wowote, na anahisi wakati umefika.
Prezzo alimaind mpaka akawa anabishana na washiriki wenzake akiwemo Keita na kutaka mlango ufunguliwe aondoke lakini baadhi ya washiriki wenzake walimsihi asifanye hivyo.
Huu mchongo umetokea siku 30 baada ya Prezzo kuwa trending topic kwa wakenya kutokana na kuchaguliwa kwake kwenda big brother ambapo wengi walikua wanamdiss kwamba haikutakiwa apelekwe BBA ambapo Nakumbuka Naziz wa Necessary Noise ambae ni mshkaji wa Prezzo alikaa na mimi studio siku 31 zilizopita na kuamplfy kwamba wengi wamemkosoa lakini ni kwa sababu hawamjui Prezzo vizuri.
No comments:
Post a Comment