ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 16, 2012

KUMBUKUMBU


MZEE ROBERT MAGWEIGA MARWA
Ni miaka miwili tokea, tarehe 16 Juni 2010, ambapo Mzee Robert Magweiga Marwa ulitutoka ghafla ukiwa una nguvu zako na tukiwa bado tunakuhitaji. Tupo nawe siku zote na unakumbukwa daima na mkeo Mwl. Immaculata Marwa wa Mwisenge-Mtakuja, Musoma, wanao Flora Rhobi Marwa na Flavian Marwa Marwa walio Washington DC, Celestine Mwita Marwa aliye Dar es Salaam, Mrs. Felister Wegesa Aiko na Mrs. Sylvia Bageni Deogratias wa Mwanza na Mrs. Diana Nchagwa Mbuya wa Musoma.

Unakumbukwa pia na wakwilima, wakamwana, shemeji zako na wajukuu walio sehemu mbali mbali Tanzania, USA, South Africa na Kenya pamoja na ndugu jamaa na marafiki.

Bwana ametoa na bwana ametwaa

Kuna ibada St. Luke Catholic Church, McLean, VA, USA na St. Peter’s Catholic Church, Oyster bay, Dar es Salaam

No comments: