Meli yenyewe namna ilivyo.
|
Sehemu mbalimbali za meli hiyo zinavyo onekana hii ni sehemu ya kuingilia magari.
Korido maalum.
Sehemu ya kupaki magari.
Abiria wataweza kubarizi ubaridi na raha za pwani.
Inavyoonekana kwa mbele ikiwa na magari.
sehemu nyinginee.
Picha zote kwa Hisani ya Juma Mmanga ( RAHA ZA PWANI)
Meli ya kisasa karibuni kuzinduliwa inauwezo kubeba magari 200, abiria 1500 na Mizigo tani 500.
KAMPUNI ya Usafiri wa baharini ya Azam Marine inatarajia kuzindua meli kubwa ya kisasa kwaajili ya abiria waendao Dar es Salaam, Pemba na Unguja. Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Hussein Mohamed Said, amesema Julai 15 mwaka huu meli hiyo yenye urefu wa mita 100 itazinduliwa.
Mohamedi alisema shida ya usafiri itapungua kwa asilimia kubwa kutokana na meli hiyo kuwa na uwezo wa kubeba abiria 1500, Mizigo tani 500 na magari 200 ambapo abiria atakae jisikia kwenda na gari lake Zanzibar, Pemba au Dar es Salaam ataweza kufanya hivyo.
Waziri Mwenye dhamana ya Mawasiliano na Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hamadi Masoud, alithibitisha kwamba anataaarifa za ujio wa meli hiyo ambayo alisema kwa kiasi kikubwa itakuwa ni ya kutoa huduma tu na siyakutengeneza faida. Meli hiyo inauwezo wa kwenda kasi ya notkomail 20.
No comments:
Post a Comment