ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 19, 2012

Maalm Seif: Toeni maoni yenu kueleza muungano mnaotaka

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (Cuf), Maalim Seif Sharif Hamad, amewahimiza wananchi visiwani Zanzibar kujitokeza kwa wingi katika mikutano ya ukusanyaji wa maoni juu ya Katiba mpya na kkuwa huru kueleza aina ya Muungano wanaoutaka.

Akiwa katika ziara ya siku moja ya kukagua uhai wa chama chake kisiwani Pemba jana, Maalim Seif, alisema fursa ya kutoa maoni mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ni adimu na itakuwa si jambo la busara kwa wananchi kutoitumia vema  kwa maslahi ya Zanzibar.
Aliwaambia wananchi kutoka majimbo ya uchaguzi ya Mgogoni na Micheweni  waliokusanyika huko Mapofu Wingwi, mkoa wa Kaskazini Pemba kuwa, katika miaka 48 ya muungano wananchi  hawajapata fursa kama hiyo, hivyo  wasikubali kuitupa, kwani inaweza isitokee tena katika muda ujao wa uhai wao.
“Kwa mtazamo wangu ajenda kuu kwa Wazanzibari katika mchakato wa kuandika Katika mpya ni muungano, kwa sababu Zanzibar  inayo Katiba yake ya mwaka 1984,” alisema Maalim Seif  ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar.

Aliwakumbusha  wananchi  kwamba, Katiba ya Zanzibar inajumuisha mambo mengi  yanayogusa maslahi ya Wazanzibari, kama vile  haki za binaadamu na  mgawanyo wa madaraka.
Mwakilishi wa Mgogoni, Abubakar Khamis Bakary kwa upande wake  aliwataka wananchi kuwa na imani na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Alisema wananchi wawe na imani  kwa sababu  kisheria tume hiyo itaheshimu maoni yao na kwamba hakuna namna  utendaji wa chombo hicho unaweza kuruhusu udanganyifu.

 
CHANZO: NIPASHE


5 comments:

Anonymous said...

SAFI SANAA HII MAALIM SEIF OYEEEEEEEEEEEEEEE
NA INSHALLAH ALLAH ATAKULINDA NA MAFISADI WANAOTAKA KUKULIA NJAMA ZA AINA ZOZOTE ZILE INSHALLAH NA KUKUBARIK BWANA WEWE ALLAH MA AMIN.

TUMUOMBENI DUA KWA WINGI WAISLAMU WOTE POPOTE TULIPO TUNAOITAKIA KHERI NA AMANI KATIKA VISIWA VYETU HIVI VIWILI.


ALLAH KISHASEMA TUSIZULUMU WALA TUSIZULUMIWE NA WALA TUSIISHI KWA UNYONGE NA KUZALILIWA KAZI KWENI WAISLAMU NA WAPENDA AMANI POPOTE PALE MLIPO

HAKI SAWA KWA SOTE MPENDA AMANI NEW YORK

Anonymous said...

Kutokana na uwezo wangu mdogo wa kufikiri, nilidhani pia mtoa maoni wa kwanza anaelewa kuwa wapo pia wakristo wazanzibari wanaovitakia visiwa hivyo amani.

Anonymous said...

unapokwenda mji wa vipovu na wewe jaribu kubinya jicho lako uwe kama wao, kinyume na hivyo watalitofua uwe kipofu kabisa, kio kama tunawadharau hawa wakristo asili wa zanzibar ni miongoni mwa walio wengi zanzibar tuna kwenda nao misikitini na tunafunga nao, sio hao wakristo walioletwa kupiga kura, hawa hawaitakii mema zanzibar na hatuwatambui.

Anonymous said...

anonymous wa pili ndugu yangu mimi nafahamu fika kwamba wapo pia wakristo wazanzibari wanaovitakia visiwa hivyo amani nafahamu sana hilo na najua kwamba wapo bega kwa bega na wanzanzibari wenzao ili tumebaguliwa sana waislamu ndo maana niliandika hayoo maneno juu, nisamehe sana ndugu yangu kama nimekosea lakin nia yangu hakuwa kutokuwaweka wakiristo wa kizanzibari nao mbele sawa na wakati wa kuomba dua katika dini yetu inabdi mtu unawawake walio waumini wote pamoja. nisamehe sana ndugu yangu tena siyo nia na madhumuni yangu kuwatenga wakiristo wa zanzibari

Anonymous said...

huyu anonymous wa 10 37 wa mwisho kanikera sana kusema kumuomba radhi mkiristo ebwana eeh kulikuwa hakuna wakiristo zanzibar, hakuna mzanzibari wa kikiristo, wameletwa na muungano na ndo wakashamiri ebwana eeh nina ushahidi wa hili so ndugu yangu mpendwa usiombe radhi kijinga kijinga njoo kwangu nikupe kitabu usome na uona kwamba kulikuwa hakuna mkiristo wa kizanzibari