ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 19, 2012

Membe: Tuhuma za kuitabiria ushindi Chadema ni uzushi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, amekanusha tuhuma dhidi yake kuwa amekitabiria ushindi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es salaam jana, Membe, alisema wakati ambao alikuwa  Uingereza kuna maneno yaliyokuwa yakienezwa kwamba aliitabiria ushindi Chadema  mwaka 2015.


“Napenda kusema kwamba sijatabiri ushindi kwa Chadema wala mtu yoyote na mimi siyo mtabiri” alisema Membe.

Alisema hajawahi wala haamini kama Chadema ndio waliosema jambo hilo ila  kuna mkono wa mtu, ambaye ahata hivyo hakumtaja.

Alisema yeye ni  mwanachama wa mtiifu kwa  CCM na kwamba tuhuma hiyo ina lengo la kumtifitinisha na CCM.

Akizungmzia kuwakaribisha Chadema alisema: “Ni ukarimu tu na ukarimu hauna chama wala itikadi na pia naamini upinzani sio uadui bali ni ushindani wa nguvu za hoja.”

Alisema maadui wa CCM wako ndani ya chama chenyewe na wanafanya ni sawa na kujitafuna  wenyewe.

Alisema alienda kwenye jimbo lake la  Mtama  ili kufukia mashimo yaliyokuwa yameachwa na Chadema na siyo kukiunga mkono chama hicho cha upinzani.

Pia Waziri membe   alizungumzia swala la taarifa juu ya upotevu wa fedha katika wizara yake ambapo alisema Januari Mosi mwaka huu wakati  yeye, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na Afisa masuhuri hawakuwepo na waliokuwa wanakaimu nafasi zao waliidhinisha fedha za ziara ya Rais Sh. bilioni 3.5 na hivyo kuwepo kwa taarifa za kutoaminika juu ya matumizi na uwepo wa fedha hizo.

Waziri membe alisema kuwa wao kama  wizara waliamua kufanya utafiti kama waliofanya hivyo walifuata taratibu za kifedha na kiutawala.

Alisema kamati hiyo kwa kushirikisha wakaguzi wa fedha, Takukuru,Usalama wa Taifa walibaini  hakuna fedha yoyote iliyobainika kuwa kuibiwa.
CHANZO: NIPASHE

No comments: