ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 19, 2012

Majimarefu awaponda wanaomzushia kifo


Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Stephen Ngonyaji maarufu Profesa Majimarefu, amesema watu wanaoeneza uvumi wa kumzushia kifo ni mahasimu wake wa kisiasa ambao wanataka kulinyemelea jimbo lake na kuwaponda kwamba wamefilisika kisiasa.

Kumekuwa na uvumi katika jimbo lake ikiwemo mitandao ya kijamii kwamba mbunge huyo amefariki dunia akiwa nchini India alikopelekwa kwa ajili ya matibabu.


Akizungumza na NIPASHE kutoka Korogwe jana, Profesa Majimarefu alisema watu wanaoeneza habari hizo wamefilisika kisiasa.

“Ndugu zangu nimesikitishwa sana na watu wanaoeneza habari kwamba nimekufa, nipo mzima na nimerudi kutibiwa (kutoka India) na hali yangu ya kiafya ipo vizuri sana na kwa ujumla nimepona tatizo lililokuwa likinisumbua,” alisema.

Alisema habari hizo zimeanza kuibuka katika kipindi cha hivi karibuni baada ya kulazwa katika hospitali ya Muhimbili na kisha kusafirishwa kwenda nje kwa matibabu zaidi ambapo watu hao walisema amekufa baada ya kuoza utumbo.

 “Uongozi unatoka kwa mungu, watu wanaokuchagua wanafanya hivyo kwasababu mioyo yao waliyokuwa nayo, unaweza ukanisingizia nimekufa leo kwa ajili ya kupata ubunge lakini waweza usipate hata kama mimi nimekufa hadi Mungu apende unaweza kuwa kiongozi,”alisema.
CHANZO: NIPASHE

No comments: