ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, June 21, 2012

Maendeleo ya msiba wa DMV/ DOMITIAN.


Ndugu zetu waTanzania.
Domitian Rutakyamirwa


Tunapenda kuwapa taarifa za maendeleo ya mipango ya mazishi ya ndugu yetu Domitian Rutakyamirwa.
Mpaka hii leo michango inaendelea lakini bado tuko nyuma. Gharama zinazohitajika ni takriban dola za kiMarekani 15,000.
Kulingana na mahitaji ya fedha na muda mfupi tulionao, tutaanza harambee siku ya Ijumaa (June 22) saa mbili usiku. Harambee hii itafanyika ulipo msiba, nyumbani kwa familia ya Mr & Mrs Deo Mosha.
Anwani ni:

4402 Hatties Progress Dr,
Bowie, MD. 20720

Kama kawaida yetu, tunaomba kinakaka kuja na vinywaji na kinadada kuleta vyakula.

Msiba huu ni wetu sote, UMOJA, MSHIKAMANO NA USHIRIKIANO WETU, ndio utakaowezesha kusafirisha mwili wa ndugu, rafiki, Jamaa, na mTanzania mwenzetu Domitian kwenda nyumbani Tanzania kwa mazishi.
Kwa maelezo zaidi na maelekezo tafadhali wasiliana na:
Idd Sandali (Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV) 301-613-5165
Henry Kente: 240-938-2452
Bernadetha Kaiza: 240-704-5891
Marmetha (Mimi) Kente 301-693-4550
Mubelwa Bandio: 240-281-0574

Kwa wale walio nje ya Washington DC Metro, mnaweza kuchangia kwa akaunti iliyofunguliwa kuwezesha hili. Akaunti hiyo imefunguliwa katika Bank of America.

Jina KAIZA DOMITIAN CARE AND SUPPORT.

Routing.. 052001633

Account.. 446026881993..

Address ya Benki
3344 6th St, SE, #204,
Washington, DC 20032
Tutazidi kuwataarifu juu ya maendeleo ya msiba huu zikiwemo gharama na hatua za kumsafirisha marehemu kuelekea nyumbani Tanzania kwa mazishi.

Raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umuangazie.
Mungu aibariki na kuilinda familia ya Ndg. Domitian Rutakyamirwa, awape faraja na kuwatia nguvu katika kipindi hiki kigumu.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe

No comments: