Na Mwandishi Wetu
KOCHA mpya wa Yanga, Marcio Maximo anatarajia kutua nchini Jumapili ijayo, tayari kusaini mkataba na kuanza kuifundisha timu hiyo.
Maximo raia wa Brazil atatua nchini na Ndege ya Emirates akiongozana na msaidizi wake ambaye pia ni raia wa nchi hiyo.
Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa, Taifa Stars amekubali kuifundisha Yanga na klabu yake ya Democrata imemukubali pia lakini ikamuomba asiondoke mapema.
Awali Maximo alitarajia kutua nchini jana lakini uongozi wa Democrata umemuomba awaandalie program maalum ambayo wataitumia hadi watakapopata kocha mpya, pia wametaka aone mechi ya mwisho ya timu yake itakayochezwa Jumamosi hii.
Msemaji wa Yanga, Louis Sendeu jana alithibitisha kuchelewa kwa Maximo ambaye amekuwa akiwasiliana na uongozi wa Yanga kwa ajili ya kufanya usajili.
“Kweli kocha sasa atafika hapa (Dare s Salaam) Jumapili mchana na kila kitu kipo kwenye mstari,” alisema Sendeu.
Mara baada ya kutua nchini, Maximo atafanya mazungumzo na Yusuf Manji kabla ya kuingia mkataba na mara moja ataanza kazi ya kuinoa Yanga kwa ajili ya michuano ya Kagame.

No comments:
Post a Comment