Wakati ujio wa kocha wa Simba, Milovan Cirkovic ukiwa bado ni kitendawili, beki wake, Nassor Masoud ' Cholo' ataikosa michuano ya Kombe la Kagame ambayo inatarajia kuanza kufanyika mwishoni mwa mwezi huu kutokana na kutakiwa kukaa nje kwa muda wa wiki sita, imefahamika.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka ndani ya uongozi wa Simba, Cirkovic hakusaini mkataba mpya kutokana na kutofikia makubaliano na viongozi hivyo mpaka kufikia jana bado hatma ya yeye kurejea nchini ilikuwa haifahamiki.
Chanzo hicho kiliendelea kuongeza kwamba kinachokwamisha ni kiasi cha mshahara alichopendekeza kocha huyo kulipwa na imewafanya viongozi kulijadili na kufikia mwafaka.
"Ni ongezeko la mshahara ndio lilikuwa tatizo, lakini tunaelekea vizuri na tutamtumia mkataba mpya kama alivyohitaji ili aweze kuja mapema wiki hii," alisema Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala.
Mtawala alisema kuwa baada ya kufikia maamuzi ya kumpatia mahitaji yote aliyopendekeza kocha huyo, wakati wowote wanatarajia kumpokea hapa nchini.
Hata hivyo Mtawala hakutaka kuweka wazi kiasi ambacho kocha huyo alipendekezwa alipwe ikiwa ni pamoja na kuhakikishiwa nyumba ya kuishi badala ya hoteli.
Licha ya Mtawala kukataa kutaja kiasi hicho, tayari imesharipotiwa kuwa kocha huyo aliyekuwa akilipwa mshahara wa dola 6,000 ametaka alipwe dola 8,000 kwa mwezi na kutokana na maelezo Simba kwamba wako tayari kumlipa anachotaka inamaanisha kwamba Mserbia huyo atalipwa kiasi hicho ambacho ni sawa na Sh. milioni 12 kwa mwezi. Kwa mkataba wa miaka miwili, Milovan atatia kibindoni Sh. milioni 288.
Wakati huo huo, Daktari wa Simba, Cosmas Kapinga, amesema kuwa Cholo atakuwa nje ya dimba kwa muda wa wiki sita kuanzia jana na hiyo imetokana na kugundulika kuwa na maumivu zaidi kwenye goti.
Kapinga alisema kwamba hali hiyo itamfanya beki huyo aliyetemwa kwenye timu ya taifa (Taifa Stars) kuhitaji muda wa kupata matibabu na baadaye ataanza mazoezi mepesi.
"Bado ni mgonjwa na kitalaamu atatakiwa apumzike kwa muda wa wiki sita na baada ya hapo tutamfanyia tena uchunguzi kabla ya kumruhusu kuanza mazoezi pamoja na wenzake," alifafanua Kapinga.
Cirkovic alichukua mikoba ya Mganda Moses Basena na kwa muda mfupi aliibadilisha Simba ambayo ilifanya vizuri kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho lakini safari yake iliishia kwa Wasudan, Al Ahly Shandy.
Kutokana na kuchelewa kwa Cirkovic, wachezaji wa Simba wakiwemo nyota wapya wameanza mazoezi chini ya kocha msaidizi, Amatre Richard.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment