![]() |
| Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora, Mhashamu Paul Ruzoka |
Macho na masikio ya Watanzania yakiwa yameelekezwa Dodoma kusubiri bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 itakayowasilishwa kesho, serikali imelaumiwa kwa kupoteza dola za Marekani bilioni moja sawa na Sh. trilioni 1.59 za Tanzania kila mwaka, kutokana na ukwepaji wa kulipa kodi, utoroshwaji wa mali na misamaha ya kodi kwa wawekezaji kama kivutio.
Upotevu wa fedha hizo umebainishwa na ripoti ya utafiti uliofanywa na Kamati ya Viongozi wa Dini ya Haki za Kijamii, Uchumi na Hifadhi ya Uumbaji, kupitia Mchumi, Mtafiti na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk. Honest Ngowi.
Ripoti ya kamati hiyo inayoundwa na viongozi kutoka Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) na Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata), ilizinduliwa katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Akizindua ripoti hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora, Mhashamu Paul Ruzoka, alisema kiasi hicho cha fedha ni moja ya sita ya bajeti ya serikali ya mwaka 2009/2010.
Bajeti ya serikali kwa mwaka huo ilikuwa Sh. trilioni 9.5, ndiyo imesababisha kung'oka kwa mawaziri sita na naibu wawili kutokana na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, ikiungwa mkono na kamati za Bunge.
Katika bajeti hiyo elimu ilitengewa Sh. trilioni 1.7, afya Sh. bilioni 963, miundombinu Sh. trilioni moja, kilimo bilioni 666.9, maji Sh. bilioni 347.3 na nishati na madini Sh. bilioni 285.5.
Kwa bajeti ya 2012/13 serikali inatazamia kutumia Sh. trilioni 15 ikiwa ni ongezeko kutoka Sh. trilioni 13.5 za mwaka wa fedha unaomalizika Juni 30 mwaka huu.
“Kama mapato hayo yangelitumika kwa kugharimia elimu, ingelikuwa ni kama mara mbili ya bajeti ya Wizara ya Elimu; hali kadhalika kwa Wizara ya Afya na Sera ya Kilimo Kwanza ingalifanikishwa vizuri zaidi, labda mara tatu ya ilivyo sasa,” alisema Askofu Ruzoka.
Alisema upotevu wa fedha hizo unatokana na sera mbovu za ukusanyaji wa mapato.
Askofu Ruzoka alisema misamaha ya kodi kwa makampuni inaisababishia nchi upotevu wa Dola za Marekani milioni 288, ambazo ni sawa na Sh. bilioni 457.34 za Tanzania.
Alisema pia utoroshwaji wa mali (fedha na rasilimali nyinginezo) yenye thamani ya takriban Dola za Marekani milioni 300 sawa na Sh. bilioni 476.40 za Tanzania, unatokana na mianya isiyorasimishwa ya mwingiliano wa shughuli za makampuni yaliyo katika nchi zaidi ya moja (ya kimataifa).
“Hayo ndiyo maeneo makubwa kabisa yenye kuliletea taifa hasara na kudumaza maendeleo yenye tija kwa watu wote,” alisema Askofu Ruzoka.
Alisema njia pekee ya kunusuru hali hiyo ni kuwa na mikakati mipya na dhahiri ya ukusanyaji mapato kutoka kwa makampuni yanayoendesha biashara nchini.
Kutokana na hali hiyo, Askofu Ruzoka, alisema kunahitajika mfumo madhubuti utakaoihakikishia serikali mapato ya kutosha kwa kuendesha shughuli zake na kuleta maendeleo endelevu ya taifa badala ya kutegemea mno misaada ya mashirika ya fedha na serikali za nchi hisani.
Alisema vilevile lipo hitaji la kuona na kupanga sawia namna ya kuongeza mapato ya serikali wakati wa kujadili bajeti ya serikali ya mwaka mpya wa fedha wa 2012/2013.
Askofu Ruzoka aliitaka serikali kutazama upya utaratibu wa kuvutia wawekezaji na makampuni katika kutoa misamaha ya kodi na kubainisha namna ya kuipunguza kama siyo kuiondoa kabisa.
Pia aliitaka serikali kujiwekea utaratibu wa kutathmini kila mwaka gharama za matumizi yanayotokana na misamaha ya kodi ili kujua bayana wanaonufaika na misamaha hiyo.
Kadhalika, ihakikishe kuwa mikataba/makubaliano na wawekezaji/makampuni yanayomiliki migodi mbalimbali inajulika au iko wazi zaidi na kwamba inazingatia sheria za Tanzania na kwa faida ya wananchi.
Vilevile, sera ya mafuta na nishati inatazamwa upya ikiwa ni pamoja na kutambua na kuweka tahadhari katika uchimbaji wa urani.
Alisema wana wasiwasi juu ya hali ilivyo na kusikitishwa kuona jinsi rasilimali iliyo utajiri na zawadi ya Mwenyezi Mungu inatoweka kutokana na kutokuwa na sera madhubuti zenye kudhibiti ukwepaji wa kulipa kodi, utoroshaji wa mali na misamaha ya kodi kwa makampuni.
Askofu Ruzoka alisema hivi sasa upo mkakati wa utafutaji wa mafuta na nishati zenye kuambatana na zao hilo na kuhoji ni kiasi gani litamnufaisha mwananchi wa kawaida.
“Tunaiomba serikali iwe makini kwa kusimamia yale yanayotuweka pamoja kwa ustawi wa taifa letu,” alisema Askofu Ruzoka.
Naye Dk. Ngowi alisema utafiti huo ulianza tangu Desemba, mwaka jana na kwamba, vyanzo zaidi ya 70, ikiwamo Benki ya Dunia (WB) na magazeti, vilitumika kuufanikisha.
Viongozi wengine wa dini waliohudhuria ni Katibu Mkuu wa CCT, Lenard Taita; Katibu Mkuu wa TEC, Padri Anthony Makunde; Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki, Stephen Munga; Sheikh Waziri Seif aliyemwakilisha Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam; Sheikh Mohamed Khamis, aliyemwakilisha Sheikh Mkuu Bakwata na Sheikh Salum Ferej, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo.

CHANZO: NIPASHE

No comments:
Post a Comment