ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 12, 2012

MUME WA JACK PATRICK ANASWA KWA MADAWA




Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa akionyesha madawa yaliyokamatwa na kumuhusisha Abdullalatif Fundikira.

Kamanda Nzowa alisema kuwa jeshi lake limelazimika kumkamata Fundikira baada ya kuwa katika orodha ya watu waliotajwa kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya.
 
Aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo alidakwa nyumbani kwake, Mbezi Beach, Kinondoni Jijini Dar es Salaam saa 12.00 asubuhi.
“Fundikira tulimkamata nyumbani kwake, ilikuwa saa kumi na mbili asubuhi. Kwa sasa tunamshikilia na upelelezi unaendelea, utakapokamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili,” alisema Kamanda Nzowa.
Akaongeza: “Fundikira alikuwa akitafutwa na jeshi tangu Mei 16 mwaka huu baada ya kutajwa na mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Mariam Mohamed Said, 29, kuwa ni miongoni mwa wauza madawa ya kulevya.
“Huyu mwanamke alinaswa katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere katika operesheni ya polisi ya ‘kufagia’ mtandao wa madawa ya kulevya.”

No comments: