Hatimaye Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara Zanzibar, (JUMIKI) imeanza kuwaponza waasisisi wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, (SUK) Makamu Mwenyekiti wa CCM Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad.
Waasisisi hao wametakiwa kuvunja ukimya na kulielezea kinagaubaga suala la Uamsho kama linawakera au wanaliafiki baada ya jumuiya hiyo kuendelea kufanya kampeni za kutaka Zanzibar kujitenga katika mfumo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Taarifa za uhakika toka ndani ya kikoa hicho cha CCM kilichofanyika huko Kinduni Mkoa Kaskazini Unguja juzi zinaeleza jinsi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa Kaskazini Unguja Haji Juma Haji (Penya) alivyombana Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai na kumtaka alifafanue hilo.
Hata hivyo, Vuai alionekana kulikwepa na kulipa mgongo suala hilo na kulikwepa kulitolea majibu suala hilo hata wakati akifanya majumuisho ya mkutano wake wa kukagua uhai wa chama katika mkoa huo.
Penya alisema kuwa ukimya wa viongozi hao wa juu wa kisiasa Zanzibar unatia mashaka hivyo ni vyema wakajitokeza hadharani na kusema ikiwa wanaunga mkono au wanailaani jumuiya hiyo.
Mwenyekiti huyo alisema kwamba Jumuiya hiyo kwa zaidi ya miezi mitano imekuwa ikifanya kampeni za kuvunja muungano na kuchafua hali ya hewa ya kisiasa bila ya kukemewa na viongozi wakuu wa vyama vinavyoounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.
Alisema kwamba vitendo ambavyo vimekuwa vikifanywa na uamsho vina madhara makubwa katika Nyanja ya kiuchumi pamoja na kuyumbisha umoja wa kitaifa kwa wananchi wa Tanzania.
Inaelezwa kuwa Penya alipoanza kusimama na kuchangia suala la Uamsho alisikika akisema huku akilaumu ukimya wa viongozi hao tokea kuanza kwa harakati za mikutano ya Uamsho na kufanyika kwa maandamano katika mikoa ya Zanzibar.
“Ni kwanini Dk Kaume na Maalim Seif hawataki kulizungumzia suala hili,je wao wanaliafiki au wanalilaani,wajitokeze na kusema ili wananchi wajue mbivu na mbichi”alisemas Mwenyekiti huyo.
Aidha Mwenyekiti huyo wa CCM Kaskazini Unguja pia alihoji ni sababu ipi iliowafanya viongozi wa Uamsho kuamua kukutana na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na kukwepa kukutana na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd hadi sasa wakati ndiyo mtendaji mkuu wa serikali.
“Tulichokiona ni viongozi wa Uamsho akiwemo Farid Hadi na wenzake wakikutana na Maalim Seif, mbona hawajapata shauku ya kukutana na Balozi Seif ambaye ni Mtendaji Mkuu wa kazi za SMZ?”Alihoji huku akishangiliwa na wanaCCM.
Akiizungumzia Jumuiya hiyo Penya alisema yeye kwa upande wake anafikiri kuwa Uamsho imepoteza sifa za kisheria kuwa Jumuiya ya kidini iliosajiliwa kihalali baada ya kuamua kujiingiza katika masuala ya kisiasa na inapaswa kufutwa kwa mujibu wa sheria.
Mwenyekiti huyo wa CCM alimtaka Waziri wa Katiba na Sheria Abobakary Khamis Bakary kujiuzulu wadhifa wake kwa kushindwa kuishauri vizuri serikali kuhusu sheria na katiba na kusababisdha vurugu na makanisa kuchomwa moto Zanzibar.
4 comments:
Dj luke naomba uweke hii comment please kama uwmeweza kuweka huu ujumbe basi na hii comment weka please.
Who does he think he is "penya sijui panya, who is he, kutaka UAMSHO UFUTWE NA KUTAKA WATU WAWAJIBIKE WANAOTETEA HAKI YA NCHI YAO. NI KIBARAKA TUU HUYU NA KWA NINI ANATAKA WAJIELEZE WAKUU WETU KWANINI YEYE KAMA NANI HUYU PENYA AU PANYA NA AMATUMWA NA NANI?
NA NANI KASEMA KUCHANGANYA DINI NA SIASA NI MARUFUKU, NA UAMSHO HACHANGANYI DINI NA SIANA ILA UNAPIKA KABISA BIRIANI WATU WAPATE KUJA KULA SIYO KUCHANGANYA TUU.
MMESHAZOEA KUWAVUA MADARAKA WAKUU WETU NA KUTAKA WAWAJIBIKE MBONA HUKO KWENU BARA WEWE PENYA PANYA MUSUBUTU KUSEMA KAULI HIZO AU KUTAKA WATU WAVULIWE MADARAKA YAO.
UNAFIKIRI TUMELALA BADO AU TUNA SINZIA, TUNA UHURU WA KATIBA YETU NA MKITAKA KACHOMENI HII KATIBA NA ANDIKINI NYINGINEWE
UKWELI UKIJIZIHIRI UONGO HUJITENDA DAIMA NA ITAJULIKANA MBIVU AU MBICHI KAMA TUMEVUNJA SHERIA AU LA NA HAKI YA NCHI YETU MTATUPA INSHALLAH MUNGU YUPO PAMOJA NA SISI
MAONEVU BASI TUMESHACHOKA NA SISI SI WAPUMBAVU KAMA UNAVYO DHANI WEWE PENYA PANYA
UNATAKA MADARAKA YA DUNIANI KESHO AKHERA RAHMAN ANAKUSUBIRI USILISAHAU HILO
DJ LUKE PLEASE NIWEKE HII COMMENT
Jumuiya ya UAMSHO Imekuwa ikiandawa kipindi kirefu tangu kuanzishwa kwake mfano mwaka 2004 walipotaka kufanya maandamano Polisi ilikubali kwa kutoa kibali rasmi,lakini siku mbili kabla ya kufanyika kwa maandamano hayo baadhi ya Masheikh wa Jumuiya hiyo walianza kukamatwa kwa visingizio mbalimbali.
“Haya yanayotokea sasa ya sisi kusingiziwa kuwa tumevuruga amani si mageni haya yameandaliwa yalianza siku nyingi ,lakini jambo la kushangaza hapa kulichomwa kuran tukufu hakuna kiongozi aliyekemea,lakini leo yamechomwa makanisa kila kiongozi ana laani.
sehemu kubwa ya makanisa yaliyochomwa hayakuwa na hati miliki kutoka kwa Mamlaka zinazohusika kwani hapo mwanzo zilikuwa ni makaazi ya kawaida,lakini wakayageuza kuwa makanisa,licha ya kuomba kwa kipindi kirefu,Serikali haikuwa imewapa.
chakuchekesha hivi juzi juzi mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd ameagiza makanisa yote yasiyokuwa na hati miliki yapewe haraka…naambiwa jana katuma ujumbe kwa watu wa ardhi kwenda kuwahimiza hao ndio viongozi wetu.
tunataka nchi yetu na utaifa wetu tumechoshwa na uonevu muungano ni jambo la hiyari RATIFICATION si kulazimishana na kuburuzwa kana ni mzigo mnavyodai basi tuachiyeni mzigo wetu wenyewe tubebe lakin ni kiini macho mnauhitaji sana muungano kama mnavyohitaji KUPUMUA watu wa tanganyika.
katika dunia ya leo hakuna anayependwa kusimwangwa na kuonewa labda awe ametaka kwa hiyari yake mwenyewe na muungano hauna ulalali na si wahiyari na hatuutaki na nendeni sasa mkarekehishe makatatasi feki na kuuhalalisha
luke weke hii kitu mkuuu
kama serikali ishalaani na hawa watu wamo ndani ya serikali kuna haja gani atoke binafsi alaani..! kama mnahitaji kila mtu ndani ya SMZ alaani basi itachukuwa mwezi mzima..
na who is panya penya by the way anataka ukuu siyo?
nashkuru sana mkuu kwa kuniwekea comment zangu najua sasa umejirekebisha na umekuwa kama michuzi thanks man
Post a Comment