Advertisements

Friday, June 22, 2012

Usisubiri mpaka afikirie kutafuta wa kumtuliza!-2

JIULIZE una tabia ya kulalamika na kujiona unakosewa sana na mpenzi wako kila wakati? Kuna wakati unajiona una thamani kubwa kuliko mwenzako kiasi cha kuchukizwa na mambo anayofanya ambayo huyapendi?
Umekuwa na kawaida ya kumkosoa sana mpenzi wako katika kitu kimoja mara kwa mara na hataki kuacha? Kama majibu ya maswali haya ni ndiyo, unatakiwa kujichunguza vizuri. Ukiona husikilizwi kero zako na mpenzi wako, ujue na wewe una mambo yanayofanana na malalamiko yako. Namaanisha kwamba, ukijichunguza kwa umakini mkubwa, utagundua kwamba hata wewe una tatizo la kubadilika.
Fanyia kazi hili; ili mwenzako akusikilize, bila kujali jinsia...kwanza achana na malalamiko. Anza wewe kumsikiliza. Akikuambia kitu fulani hapendi na ukaona ni kweli si kizuri, acha! Kufanya hivyo kutakutengenezea mazingira ya kusikilizwa na kupewa kipaumbele katika mambo ambayo huyapendi!
Huu ndiyo ukweli! Nimeanza na utangulizi marafiki zangu kwa lengo la kuwekana sawa. Huu ni uwanja mpana wa elimu ya maisha na mapenzi. Ndiyo mahali pake hapa. 

Mada iliyopo mezani ni kama inavyosomeka hapo juu. Leo tunaingia katika sehemu ya pili. Ndugu zangu, ni vizuri kuwachunguza wenzi wetu na kuwafahamu vizuri.
Ni vyema kuwajua ili tusije kukosea bila kutambua kuwa tunafanya makosa. Nazungumzia suala la usaliti. Kwamba wakati mwingine inawezekana wewe ukawa chanzo cha kusalitiwa. Inawezekana mwenzako hana nia ya kukusaliti lakini kwa sababu umeshindwa kumsoma, anaamua kwenda kutafuta kitulizo huko barabarani!
Katika hilo nawagawanya wanawake katika makundi matatu; machakaramu wanaoweza kusema wanawahitaji wanaume zao, wanaozungumza kwa vitendo zaidi na wale wakimya ambao hawasemi chochote zaidi ya kumsubiria mwanaume wake.
Hapa niwe mkweli, wanaume hawana tatizo. Wakitaka wanasema. Hata wasiposema, wanalianzisha na hakuna wa kuwazuia labda kama kuna ‘dharura’. Kwa wanawake ni tofauti, ndiyo maana nachambua hapa ili kuwafahamu zaidi. Twende tukaone.
MACHAKARAMU
Aina hii ya wanawake ni wale ambao wanaweza kueleza moja kwa moja hisia zao. Kama hutakuwa makini, unaweza usimuelewe hasa kutokana na tabia ya kupenda sana utani. Unaweza kuwa kazini mchana, akakutumia meseji: “Leo utaipata!”
Hilo pekee linatosha kabisa kukushtua kuwa mzee mzima una kazi nyumbani. Wa aina hii, anaweza asiseme chochote zaidi ya hapo, akitegemea umeelewa. Unaweza kurudi nyumbani usijue kinachoendelea, ukamuacha na kiu yake. Nini kitafuata?
Mwingine anaweza kusema: “Baby leo nataka tushindane tuone nani mkali.” Sentesi kama hiyo unaweza kuichukulia kama masihara kumbe mwenzako anamaanisha. Hata hivyo, tafiti zilizofanywa na wanasaikolojia mbalimbali duniani, zinaeleza kwamba kauli kama hizo kwa kiasi kikubwa hupunguza uwezo wa kujiamini kwa mwanaume.
Mwanasaikolojia Tonny Stanley wa Taasisi ya Uhusiano na Ndoa (Institute of Relationship & Marriage) wa Uingereza ambaye ndiye mkurugenzi wa taasisi hiyo, anaeleza katika ripoti ya utafiti wa jopo lake ya mwaka 2010 nchini humo kuwa, asilimia 70 ya wanaume wanaoambiwa maneno ya kuandaliwa kabla na wake/wapenzi wao hupoteza msisimko na ghafla kuanza kuwa goigoi.
Sehemu ya ripoti hiyo inasema: “Lakini mwanaume huyo huyo akichepuka pembeni anakuwa moto wa kuotea mbali. Ni kwa sababu huko yeye ndiye anakuwa muongozaji. Ndiyo msingi wa mwanaume.”
ANGALIZO KWA WANAWAKE
Kama unajijua upo katika kundi hili ni vizuri kubadilika. Ingawa kuna ukweli kwamba, baadhi ya wanaume wanapenda wanawake wa aina hii kwa kuwa nao pia ni machakaramu. Jambo kubwa kwako ni kuangalia, upo na mwanaume wa aina gani? Ukimjulia hawezi kukushinda, hapo utajua pia namna ya kuishi naye.
Jinsi ya kufikisha hisia zako vizuri bila kuharibu msisimko wake na kumfanya asi= jiamini, mwisho wake unajua ni nini? Atatafuta anayeendana na tabia zake. Tayari utakuwa umeshasalitiwa. Zinduka mwanamke!
Wiki ijayo tutaingia katika hatua nyingine tuone aina nyingine za wanawake, SI YA KUKOSA!
Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia magazeti ya Global Publishers. Ameandika vitabu vya True Love, Let’s Talk About Love na Whoi is Your Valentine vilivyopo mitaani.

No comments: