ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, June 7, 2012

Wanaume wanaoongoza kwa kuvunja ndoa za watu-2

WIKI iliyopita utakumbuka nilianza kuzungumzia wanaume ambao wamekuwa wakilalamikiwa huko mitaani kwa kuongoza kuvunja ndoa za watu.
Makala hii imetokana na uchunguzi wa muda mrefu ambao umeonesha kuwa, kuna aina flani ya watu ambao wamekuwa na ushawishi wa hali ya juu kwa wake za watu na hatimaye kutembea nao.
Nilianza kuwazungumzia madeveva wa teksi na bajaji, wauza magenge na maduka pamoja na walimu ambapo tumeona ni kwa jinsi gani wamekuwa wakiogopeka kutokana na tabia zao ambazo zimesababisha migongano katika ndoa nyingi.

Lakini utakumbuka nilikomea kuwazungumzia waganga wa kienyeji ambao nao ni tatizo. Baadhi ya watu hawa ni wasanii hasa wale wanaojitangaza kutibu magonjwa ya kinamama.
Matukio ya waganga wa kienyeji kudaiwa kupora wake za watu hasa maeneo ya vijijini yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara lakini baada ya muda inabainika nguvu za giva ‘zinatumikaga’.
Katika hili nawashauri wanaume kutowaruhusu wake zao kwenda wenyewe kwa waganga wa kienyeji ili kujihakikishia usalama wa ndoa zao.
Mabosi
Baadhi ya wake za watu walioajiriwa wamekuwa wakijirahisi sana kwa mabosi wao kwa kile kinachoelezwa kuwa, wanaogopa kupigwa chini.
Wengi wako tayari kwa lolote ili mradi wasitemeshwe mzigo, matokeo yake baadhi ya mabosi hutumia mwanya huo vilivyo kwa kuwaomba penzi wakijua kukataliwa ni vigumu.
Na kweli, ukijaribu kufuatilia katika asilimia 100 ya wanawake wanaotongozwa na mabosi wao, unaweza kukuta ni 25 tu ya wanaokataa lakini 75 wanakubali wakiamini kwa kufanya hivyo ni wanajijengea ulinzi wa ajira zao, hapo ndipo tatizo linapotokea.
Kwa maana hiyo ukiona mkeo yuko ‘close’ sana na bosi wake wa kiume, usiridhike na jibu la kwamba ni ni kutokana na majukumu ya kikazi bali kengele igonge akilini mwako na ufuatilie kama huyo bosi hakutafunii mali zao.
Fundi chereheni
Huko uswahilini kuna mafundi cherehani ambao ni tishio kwa ndoa za watu. Kama ujuavyo baadhi ya wanawake wanapenda kila mshono unaotoka wauvae wakati uwezo wa kumudu gharama hawana.
Matokeo yake unamkuta mke wa mtu ‘anajiweka’ kwa fundi akijua siku akipata tu kitambaa anaweza kushonewa nguo bure na maisha yakaendelea.
Mbaya zaidi, baadhi ya mafundi hao ni viwembe na wanawake wanaojipendekeza kwao hawawalazii damu.
Madaktari
Kuna baadhi ya madaktari ambao wanawachafulia wenzao kwa kuwa na tabia zisizofaa kwa wake zatu hivyo kwenda kinyume na maadili ya kazi yao. Yaani wao akienda mke wa mtu kwa lengo la kuchekiwa tatizo flani linalohusu maeneo nyeti, baadhi yao huona ni dili na huchukulia hiyo kama njia ya kuwachomekea.
Matukio ya wagonjwa kubakwa na madaktari yamekuwa yakiripotiwa kila mara. Hata madaktari ambao wanadaiwa kutongozatongoza wake za watu ovyo huko mtaani ni wengi.
Kwa kuhitimisha niseme tu kwamba, watu hao hapo juu si wote wabaya lakini tabia ya baadhi yao kuwa viwembe na kuwa wepesi kutongoza wake za watu kwa kutumia nafasi zao iwe changamoto kwa wanaume kuwa makini nao ili wasije wakashtuka wameshapokonywa matonge midomoni.

No comments: