ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 24, 2012

AJARI MBAYA YATOKEA MKOANI IRINGA NA KUUA 3 NA KUJERUHI 38

 Hili ndilo basi la Tony Sley ambalo limepata ajali jana usiku na kuua watu watatu na kujeruhi 38

Majeruhi wakisubiri matibabu Hospitali ya mkoa wa Iringa

Majeruhi wa basi la Tony Sley Bi Agnesy Lukasi akiwa na mtoto wake Dina Lukasi (4) wakisubiri kupewa matibabu katika Hospital ya mkoa wa Iringa baada ya kufikishwa hapo usiku huu wakitokea eneo la ajali mlima wa Kitonga

Ajali ya basi ya Tony Sley yenye namba za usajili T 218 ACH lililokuwa likitokea Tunduma mkoani Mbeya kwenda jijini D’Salaam imeua watu watatu wakiwemo wawili raia ya Zambia na mmoja mtanzania na kujeruhi wengine 38.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la kona za mlima wa kitonga kwenye barabara kuu ya Iringa –D’Salaam jana majira ya saa 12 za jioni baada ya dereva wa basi hilo kushindwa kulipita lori lilolokuwa mbele yake.

Wakizungumza katika eneo hilo na Hospitali ya mkoa wa Iringa majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya Kilolo Ilula walisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wao alisema Agnes Lukasi (30).

Agnesy alisema kuwa kwa upande wake alikuwa amekaa siti ya mbele na wakati dereva huyo akifanya uzembe huyo walikuwa wakimshuhudia hata kujaribu kumuonya bila mafanikio.

Alisema kuwa katika basi hilo alikuwa na mtoto wake Dina Lukas (4) ambaye pia amejeruhiwa katika paji lake la uso.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamhanda ambaye alifika eneo la tukio pamoja na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa aliuthibitishia mtandao huu kuwa jumla ya abiria 38 ndio waliojeruhiwa katika ajali hiyo.

No comments: