![]() |
| Sheikh Ponda Issa Ponda |
Ni kifungo cha miezi sita gerezani, faini
Wito umetolewa kwa watu kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa litakaloanza Agosti 26 hadi Septemba Mosi, mwaka huu kwani ni suala la kisheria na kutokushiriki katika zoezi hilo ni kosa la jinai.
Akizungumza na NIPASHE jana, Mwanasheria katika Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), Oscar Mangula, alisema suala la sensa ni la lazima kwa kila Mtanzania na watakaokiuka agizo hilo adhabu kali itachukuliwa dhidi yao ikiwemo kwenda jela miezi sita, faini ya Sh. 600,000 au vyote viwili kwa pamoja.
Kwa upande wake, Mratibu wa sensa ya watu na makazi, Irenius Ruyobya, alisema sensa ni muhimu kwa watu wote na ina manufaaa makubwa katika maendeleo ya Taifa.
Aliongeza kuwa wamefanya jitihada mbalimbali kuhamasisha jamii kushiriki katika sensa ikiwemo kutoa vipeperushi, kutumia mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari ili kuhakikisha kila mtu ana uelewa na kushiriki kikamilifu zoezi la sensa.
Aidha, alieleza changamoto zinazowakabili ni kuwepo kwa baadhi ya makundi yanayotishia kugoma kushiriki katika sensa na imani potofu kwa kudhani kitendo cha kuhesabiwa ni suala la kishirikina.
Kauli hiyo imekuja wiki kadhaa baada ya Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini kutangaza mgogoro na Serikali kwa kutangaza kufanya maandamano kushinikiza kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso la sensa vinginevyo watagomea zoezi hilo.
Katibu wa Jumuiya hizo, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema Jumuiya hizo zitahamasisha Waislamu waandamane siku ya sensa na kupinga suala hilo kwa sababu serikali haina nia ya kubadilisha msimamo wake na kuingiza kipengele cha dini kwenye zoezi la sensa.
Alisema mapendekezo yao wameyawasilisha serikalini lakini kwenye mkutano uliowakutanisha viongozi wa dini, serikali na ofisi ya sensa mjini Dodoma hivi karibuni, ulidhihirisha kwamba serikali haina nia ya kuingiza kipengele cha dini na uwakilishi wa dini zote kwenye zoezi hilo baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, kuwajibu kwamba kufanya hivyo kunaweza kuhatarisha amani ya nchi.
Alisema Wasira alieleza kuwa serikali haipangi maendeleo kwa kuzingatia dini na kwamba Tanzania inafuata utaratibu wa sensa wa kimataifa wa kuhesabu watu bila kuhusishwa kabila wala dini zao.
“Siku ya Agosti 26, iliyopangwa kuanza hiyo inayoitwa sensa, Waislamu tumejipanga kufanya maandamano makubwa ya amani nchi nzima kupinga misingi dhuluma dhidi ya Waislamu…tutatoka nchi nzima ili ulimwengu washuhudie idadi ya Watanzania ambao hawakushiriki kuhesabiwa,” alisema Ponda.
Alisema kumekuwepo na takwimu mbalimbali zinazokinzana kuhusu idadi ya Waislamu na Wakristo, huku akiishutumu serikali kwa kufumbia macho takwimu hizo zikiwemo zilizopo kwenye tovuti ya Kanisa Katoliki, Bodi ya Utalii na Idara ya Uhamiaji.
Hata hivyo, alipoulizwa kama wanatambua idadi ya Waislamu, Ponda alikataa kujibu akieleza kwamba takwimu zao ni kwa matumizi yao wenyewe.
Mbali ya maandamano hayo, Ponda alisema wanakusudia kwenda mahakamani kuzuia zoezi la sensa hadi hapo mapendekezo yao yatakapoingizwa kwenye dodoso la sensa.
Imeandikwa na Winfrida Kanyika (SJMC) na Neema Nyagonde (Tudarco)
CHANZO: NIPASHE

3 comments:
utumbo mtupu bongo bongo nja tu si umeona mwenyewe dj luke ukiwa huku kwani unalazimishwa kuhesabiwa? na kupewa adhabu kali kama za bongo, aise noma kiyama bongo bongo, ningekuwa kule ningekata kuhesabiwa na niwaona wanitiye ndani au kutaka faini nja nja inakufanya mtu utu wako unauza na kutumia mabavu bongo njaa kiyamaa na upstairs zime hama
Wewe anon wa hapo unachokiongea hukifahamu, ni kosa kisheria kuhamasisha watu kupinga sensa, ila kama wewe unataka kutohesabiwa mwenyewe hiyo ni sawa. Kosa ni kuhamasisha watu wengine au group la watu wasitake sensa. Nashangaa huyo mchovu kama Ponda issa anaweza kuhamasisha watu wasihesabiwe...kama anataka yeye na familia yake wanaweza wasitake kuhesabiwa hiyo haina tatizo. Anachodai hakijulikani na wala hakuna wa kumsikiliza huyo mhuni anayejiita sheikh. Wasiotaka kuhesabiwa basi waondoke katika jamii ili wasije kuongeza mzigo katika bajeti kwa kuwa bajeti ya maendeleo inapangwa kutokana na idadi ya watu. Hivyo wewe anon hapo juu unatakiwa ufikiri kwa kutumia kichwa
wewe anonymous wa july at 10:31 pm watu wameshakaa chini na kutumia bongo zao na kufikiria na kuchambua sana hii issue usituone mabwege labda wewe ndo maana wanawahamasisha watu wasipige kura, wasajua mchezo mnaoucheza, Tanzania waislamu wako wengi kuliko wakiristo ukitaka usitake nakupa nyeti wewe mwenye akili ya mgando.Wanajidai kuwahesabu watu halafu wanachekechua kama kawaida yao, watu tumeshashtuka long time.
Na ukome mwanzo leo na mwisho kumuita sheikh wetu muhuni mbona mapadri na mapasta wenu wanachukua wake za watu na mnajidai kuoa eti mke mmoja na huku mnavimada kibao mbona uzinzi wenu hamuoni na uhuni wenu, potea huko kawahubiriye chekecheka na hao hao chekechea ukiwahubiria wakigundua unawadanganya watakupuuza
tumesha amkaa bro labda wewe na familia yako laleni na nendeni mkahesabiwe pamoja na fanicha za nyumba zenu na bajeti ya maendeleo kula wewe na familia yako na mapadri zenu
Post a Comment