Ndugu Watanzania wenzangu,
Baadhi ya mambo aliyoibua Waziri Muhongo na Katibu Mkuu wake
katika Wizara ya nishati ametusaidia kufungua njia na kuelewa u “Ndumila
Kuwili” wa Wabunge wetu jinsi walivyo na sura mbili.Nikisema sema hivi nina
maana ya kwamba Wabunge hawa wamekuwa wakipiga kelele za UFISADI kwenye Taasisi
na Wizara mbali mbali, huku wenyewe ndio wakiwa ndio wakumbatiaji ya mambo ya
ki FISADI yanayofanyika katika taasisi
na Wizara hizo.
Aidha wamekuwa wakifaidika kwa kupata marupurupu toka kwa
baadhi ya watu wao au ndugu zao wanaofanya biashara na Taasisi au Wizara au
wanapatiwa viziba mdomo kutoka kwa Watendaji wa Taasisi au Wizara.
Hapa napenda
kutahadharisha,(bali hizi ni hisia zangu mwenyewe) kwa jinsi Ufisadi huu
ulivyoibuliwa katika Wizara ya Nishati inaelekea kulikuwa na kutoelewana au mgongano wa
maslahi baina ya Watendaji/Menejimenti na Bodi na kamati ya Bunge ya Nishati.
Uozo wote ulioanishwa na Mhe Waziri na Katibu wake, ni ukweli
kabisa mambo haya yamekuwa yakifanyika muda mrefu lakini kwa kulindana na
kukingiana vifua aidha kwa Wabunge wanaofaidika kwa kupata chochote toka kwa
watendaji au wajumbe wa bodi nao walikuwa wakifaidika kwa namna Fulani.
Nina hakika kabisa kwa Bw Mhando kumpatia tenda mke wake na
kuagiza PAKACHA LA MISUMARI badala ya vipuri kwa dhamani ya $ 50.000.000 toka
nje ya nchi, hii ilikuwa dili lilopangwa kwa kuwashirikisha wahusika wote
katika wizara,Tanesco, bodi na kamati ya wabunge wa nishati. Tatizo lililojitokeza
hapa nadhani mgao haukwenda vizuri kwa wahusika wengine. Hivyo wameamua
kumtonya Waziri (lugha ya mjini au kumuuzia dili Waziri).Na Waziri Muhogo bila
kusita akayaweka mambo hadharani.
Nimesoma kwa makini hoja za baadhi yaWabunge husika katika
kamati ya Nishati jinsi walivyojitetea na kujisafisha ya kwamba hawajahongwa au
kufanya biashara na wizara. Ki ukweli kwa sheria zetu za Tanzania itakuwa ni
vigumu sana sana kuthibitisha jambo hili.
Nikisema hivyo nina maana unaweza kwenda Tanesco ukaambiwa
kampuni yenye tenda ya vipuri inaitwa, Masamaki General Traders na ukifuatilia
kwenye kumbukumbu za usajili wa kampuni unakuta mmiliki anaitwa Mr, Tulia bin
Unyolewe. Ukimtafuta huyu bwana hutampata aslani kabisa bali utaambiwa kuna
tetesi kampuni hii inahusuka na Mbunge Fulani,Waziri Fulani au Mwenyekiti wa
Bodi Fulani. Hapo ndio itakuwa umekwama kuthibitisha. Utaanza kukutana na
hekaya za ABUNUWASI.
Na pia ukisema ufuatilie kwenye Benki akaunti ili ujue ni nani
anasaini kutoa au kuingiza fedha, hata benki watakwambia hawamjui mteja huyu
bali wao kazi yao ni kutunza na kuhifadhi fedha za mteja.
Nina hakika katika mabenki kuna Camera sehemu zote, mlangoni,
kwa keshia na kwingineko, lakini pia watakwambia akiingia huyu bwana kuweka au
kuchukua fedha mitandao inakuwa imezima, hivyo ni vigumu kupata picha yake.
Ukifuatilia kwenye kadi ya ufunguzi wa benki akaunti ambayo inawekwa picha
yako, utakuta imewekwa picha ya mtoto wa miaka 12.
Huu ndio ubabaishaji uliopo katika nchi yetu ndio maana
inakuwa ni vigumu kudhibitisha tuhuma yoyote kwa vigogo na wabunge
wababaishaji.
Ndio maana wanajigamba hadharani ya kwamba kama kuna
udhibitisho basi utolewe ili sheria ifuate mkondo wake, wana hakika kabisa ya
kushinda kwenye tuhuma hizi kwa sababu ya kukosa ushahidi kamilifu.
Napenda kuwaambia Watanzania wenzangu, ufisadi kama huu upo
kila kwenye taasisi na wizara zote serikali bali hapajapatika watu makini wenye
uchungu na nchi yao kama Muhongo na Katibu wake.
Bali nina hakika Waziri Muhongo na Katibu wake wamefungua njia
kwa Watendaji wengine kufuayta nyayo zao ili tuikomboe nchi yetu katika dimbwi
la ufisadi.
Hakika kwa sasa tusubiri kusikia mengi yatakayoibuliwa
kutokana na sakata hili, kwani mtego umenasa na kila mtu anajitetea kutoka
ndani ya mtego.
Waziri Muhongo, keep it up
Mungu Ibariki Tanzania , Mungu ibariki Afrika
ALUTA KONTINUA.
1 comment:
Kila kitu kina mwanzo na mwisho wake,mwizi siku zake arobaini,kuna siku Mafisadi wote watakuja kubainika kwa uwezo wa Mola wetu,Maana wananchi tunahangaika na maisha ya kila siku,tunalipa kodi na huduma hatupati,Na baadhi ya viongozi wanakula nchi yetu kiurahisi hivi na kuzidi kuididimiza kimaendeleo,Ubinafsi ni kitu kibaya sana.
Post a Comment