ALL About Love siku zote ina lengo la kukujenga na kukupanua mawazo yako juu ya uhusiano na mapenzi. Inakupa ujasiri, uwezo wa kujitambua na uhakika wa kukabiliana na matatizo yoyote katika uwanja wa mapenzi.
Naendelea kuzungumza na vijana ambao wapo mbioni kuingia kwenye ndoa lakini hawajui pa kuanzia. Hata kama wanajua wanakuwa na mitazamo chanya zaidi. Wanawaza kukutana na vitu vizuri zaidi kwenye ndoa.

Hawafikirii changamoto ambazo wanaweza kukutana nazo. Hili ndilo tatizo la vijana wengi. Kutokana na mawazo yao hayo, wanapoingia kwenye ndoa na kukutana na vitu tofauti, wanachanganyikiwa.
Dondoo zilizopo katika mada hii ni mwongozo mzuri kwako, zitakuandaa vizuri kuwa mwanandoa bora hapo baadaye. Nilianza na dondoo chache wiki iliyopita, nikitegemea zaidi katika kujipanga kabla ya kuingia kwenye ndoa ambayo wengi huwa na matarajio mazuri zaidi. Tuendelee kuona.
USIJIBADILISHE
Huwezi kumjua mwenzako kama atakuwa anaishi kisanii na wewe kama na wewe utakuwa unaishi kwa sura ya fotokopi! Sikiliza...kwa wiki mnakutana mara mbili tu, tena mnakaa kwa muda usiozidi masaa mawili, si rahisi sana kuweza kujuana tabia zenu halisi.
Pamoja na hayo, wataalamu wa mambo ya mapenzi wanashauri ili mwenzi aweze kuwa wazi zaidi kwa mwenzake ni vyema yeye akaanza kuwa wazi na kuishi maisha yake halisi kwa uwazi. Usijilazimishe kupenda kitu ambacho hukipendi.
Kama kuna jambo ambalo analifanya, linakuboa mwambie ajue ukweli. Kwanza uwazi wako kwake utamfanya naye awe wazi kwako. Hatakuwa na sababu ya kuigiza maisha wakati wewe unaishi maisha yako halisi.
Kila mmoja akimjua mwenzake, ndoa haiwezi kuwa na matatizo, maana kila mtu atakuwa anajua anaishi na mtu wa aina gani. Inawezekana kabisa, mmoja wenu akaona tabia za mwenzake zimemshinda.
Kama ni kweli na umegundua kwamba kuingia kwenye ndoa ni sawa na utumwa, fanya maamuzi sahihi. Ni nini basi? Uingie kwenye tanuru la moto au ujiondoe mwenyewe? Uamuzi uko mikononi mwako.

KUWA MKWELI ANAPOKUKWAZA
Katika kuishi kwako maisha yako halisi, mwenzako naye atakuwa kama wewe. Hiyo ni hatua nzuri maana itakuwa rahisi kwako kugundua tabia za mwenzako. Hapo utazijua nzuri na mbaya.
Acha kulea matatizo, bila kujali jinsia, mwambie mpenzi wako tabia ambazo hazikufurahishi. Ili aweze kubadilika kwa urahisi zaidi, unatakiwa kumwambia kwa utaratibu, lakini pia umpe sababu za wewe kukataa tabia zake.
Akiendelea nazo kuwa mkali, wakati mwingine ukali unasaidia. Kwa kukemea, kama ni kweli anakupenda na anahitaji uhusiano wenu uendelee, basi lazima atabadilika. Akifanya hivyo itakuwa vizuri zaidi kwako, maana utakuwa na uhakika angalau kwa asilimia chache kwamba mpenzi wako anakusikiliza.

CHUNGUZA TABIA ZAKE ZA ASILI
Rafiki zangu, lazima ufahamu kwamba wakati unapambana na tabia za mpenzi wako zisizokupendeza, zipo tabia nyingine ni za asili. Hazibadiliki. Sasa hapo lazima uwe makini kwa mambo mawili; mosi, zitakuathiri?
Pili, ni tabia zitakazokugombanisha na jamii? Maana kuna tabia nyingine zinavumilika, lakini je, hazitakuathiri kwa majirani zenu watarajiwa? Haya ni mambo ya kuyatafakari kabla ya kuingia kwenye ndoa.
Mathalani, kuna baadhi ya watu wana viburi au dharau za kuzaliwa! Hata umfanyeje, habadiliki. Unaweza kumwuliza kitu akanyamaza.
Ni tabia ya kiburi, lakini kwa sababu amezaliwa akiwa na tabia hiyo, hawezi kuiacha. Sasa hapo lazima ujiulize, utawezana naye?
Utaweza kumvuamilia na kiburi chake kwa maisha yenu yote? Huu ni mfano tu rafiki zangu, zipo tabia nyingi za asili, ambazo kwa nafasi yako unaweza kuzichunguza kwa mpenzi wako kabla ya kuchukua uamuzi mzito wa kuingia kwenye ndoa.

TUA MZIGO MOYONI
Ukweli ni silaha, ni haki na siku zote humfanya mtu awe huru. Kama kuna jambo ambalo hujalipenda kwa mpenzi wako, haraka mwambie. Acha kukaa na vitu moyoni. Si utaratibu mzuri.
Hata kama nguo zake hazikufurahishi mwambie: “Baby yaani kiukweli ukivaa hizo jeans zako hupendezi kabisa. Nadhani uanze kuvaa suruali za vitambaa sasa.”
Hapo utakuwa umemwambia ukweli wako, kukubaliana na wewe au kukataa kutatokana na mapenzi yenu. Kama anakupenda atakusikiliza. Kwani anamfurahisha nani huko barabarani zaidi yako?
Mada bado inaendelea, wiki ijayo kuna vipengele muhimu zaidi, USIKOSE!

Joseph Shaluwa ni mshauri wa mambo ya mapenzi anayeandikia magazeti ya Global Publishers, ameandika vitabu vya True Love, Let’s Talk Love na Who is Your Valentine?, vilivyopo mitaani.
No comments:
Post a Comment