Ndugu Watanzania,
Za leo popote mlipo? Sisi salama. Sahamani sana kwa kuchelewesha kutoa "final update" kuhusu mgeni wetu Mama Precious na "mjukuu wangu Precious" hapo juu, ambaye alikuwa aondoke jana!
Kwanza kabisa napenda kumushukuru Mwenyezi Mungu na Watanzania wote hapa Toronto kwa ushirikiano wenu mzuri ambao umefanikisha zoezi la Mtoto Precious Maduhu, mtoto wa Jumanne Maduhu, Mtangazaji wa Morning Star Radio, FM 105.3, Dar es Salaam.
Kama mnavyojua, Mtoto Precious na Mama yake Beatrice wamekuwa hapa kwa matibabu ya mtoto tangu kama miezi mitatu sasa. Kwa ushirikiano mkubwa, wa Watanzania wote, matibabu yamekwisha na yamefanikiwa vizuri na kupata "dischrage " ya hospitali kurudi Tanzania. Walikuwa waondoke Toronto kurudi Dar es Salaam July 28, 2012. Lakini safari ilibadilishwa ili waondoke jana, July 18, 2012 na KLM kushukia KIA, ili Mama Precious ahudhurie msiba wa Mama yake mzazi uliotokea Dar es Salaam Ijumaa iliyopita na mazishi Moshi.
Ndugu zangu, naandika na majonzi makubwa , Mama Precious na Mtoto hawakuondoka jana. Siku ya Jumanne, July 17, 2012, kati saa sita na saa saba mchana, Mama Precious alimtaarifu mke wangu anaenda kufua. Toka muda huo hakurudi nyumbani pamoja na jitihada za kumupigia simu na meseji nyingi kwamba kuna wageni wanamsubiri hapa nyumbani kumupa pole lakini hakujibu simu wala meseji. Na huo ndio ukawa mwisho wa kuonekana hapa nyumbani kwetu.
Ndugu zangu Watanzania, baada ya kujaribu kuwapigia wote ambao nilijua wako karibu naye na ambao humchukua mara kwa mara kumutembeza, nao wakasema hawajui na kwa siku hiyo hawakuwa naye. Mpaka saa tatu usiku simu alikuwa hapokei simu wala hajibu meseji, ndiyo nikaanza kuhangaika kumutafuta.
Jana Mungu akajalia tukapata taarifa kamili baada ya kuhangaika huko na kule. Mama Precious kashawishiwa na watu (majina tunayo) na mume wake na familia yake abaki hapa kinyume cha sheria kwa kuomba hifadhi ya ukimbizi (Refugee Claim), July 5, 2012 kutoka Serikali ya Canada. Swali hili litaanzwa kusikilizwa baada ya siku 30 huko Etobicoke, Ontario. Hiyo ndiyo taarifa fupi ya hatma ya ya Mama Precious na Mtoto. Kwa kifupi niliumia na kuhuzunika kwamba kwa muda wote huo nimekaa na Mama Precious kama Mtoto wangu , halafu ananizunguka. Nimesumbuka sana kubadilsha tiketi na mambo mengine hospitali yakamilike ili aondoke jana kujumuika na familia kwa msiba uliowapata, kumbe mwenzangu ananiona mimi mjinga; kwani Mumewe Jumamme Madudu na familia yake yote Tanzania ilikuwa inajua. Hili liliniumiza.
Kuna mizigo yake aliyoiacha nyumbani. Jana baada ya kupata uhakika na kujaribu mara nyingi simu yake bila mafanikio, tukaamue kwamba hataki mawasiliano na sisi ya aina yoyote na kwamba alivyoviacha siyo vya muhimu kwake. Pia nilimuambia mume wake kwamba Mama Precious kaacha mizigo na naomba anijulishe maamuzi yake nifanye nini , naye kimya. Kwa hiyo maamuzi niliyoyafanya leo asubuhi kabla ya kwenda kazini nilipeleka kwenye masanduku mbali mbali ya sadaka.
Kwa kifupi mimi nimemaliza. Namtakia kila la heri.
N.B. Hospitali watapeleka mawasiliano ya kufunga jalada kwa Baba Precious kwa sababu hawana contact za Mama Precious. Kwa Watanzania ambao maombi yao yalikuwa kwenye "pipeline" nitawaandikia barua binafsi ya kuwaeleza kwamba, huduma hii nimesimamisha mpaka uchunguzi na "hearing" zote zimekamilika kuhusu Mama Precious. Ubalozi wa Canada Nairobi umejulishwa. Nategemea ushikiano mzuri kati ya serikali ya Tanzania, Kenya na Canada kulimaliza swali hili haraka ikizingatia sheria na haki za wote na kila wakati, maslahi ya Mtoto wetu Precious yatakuwa mbele.
Nawatakia siku njema na ahsanteni tena.
Mungu atubariki sote.
Mabula Sabula

8 comments:
Really? And why are you reporting this to the public? Ili umuaibishe? Get a life
Mitanzania mingine hopless kabisa kwani angekujulisha kama anataka kujilipua ungemzuia? Mijitu mingine huwa ni mishenzi toka ilipotoka hata uisaidie vipi itakuona mavi tu na tatizo linakuja ubalozi wa canada hauna fingerprints zingekuwepo asingefanya ushenzi huo sasa atafaidika nini kama taarifa zake zishafika ubalozini? Sana sana kajiharibia future yake tu coz watatumia picha yake huko immgration ya canada alikojilipulia at the end aibu kwake huyo mama alidhani kawin kumbe kaptikana ha ha ha ha stupid kabisa please utuupdate kitakachojiri
Wakubwa, msameheni huyu dada. Mungu atawalipa kwa mema mliyomkirimia. Mwacheni apate ukimbizi ahangaike mwemyewe na maisha yake. Mkimnenea mabaya, hawezi kufanikiwa. Kama mnaamini kuwa Mungu yupo, nawahakikishia kuyu huyu binti atakuja kuwalilia kuomba msamaha mwenyewe. Hapakuwa na haja na kumtangaza publically wala kumshitaki embassy. Pamoja na usumbufu mliopata, mgenyamaza kimya kabisa baada ya kugundua kuwa yupo salama. Let her fly on her own wings for now and eventully, she will land and realize the reality on the ground.
shule saa ingine inasaidia, na mawasiliano ni muhimu sana. kulikuwa hakuna sababu ya wao kumficha mwenyeji wao maana kawasaidia vya kutosha sema ndio tunasema shukrani ya punda ni mateke.ila waache waendelee na maisha yao wewe mwachie mungu ndio atakulipa hauna haja ya kumripoti wala kuhangaika nao tena.umeshatimiza ulichokuwa unahitaji kumsaidia lakini kakuonyesha kuwa sio mtu wa kumwamini tena.mungu atakulipa ,achana nao
Wahenga wanasema "tenda wema nenda zako usingoje shukurani". Mama pole sana lakini usijali mungu ndiye anayejua na atakulipa. But the thing that hurts the most is the way this girl was so sneaky and could not even tell you the truth. Wazungu wanasema "No good deed goes unpunished" so she will get what she deserves one day.If you are a christian utamsamehe na atakuja kujuta na ushambaa wake. Lakini inatia aibu,poleni sana!
wewe unayesema kwa nn amereport, umeshaishi nchi za watu halafu mtu anakutoroka huwezi jua kama amekufa au hai ...halafu umemsaidi anakufanya wewe mjinga, wewe na yeye akili yenu moja.....I hope serikali na huo ukimbizi hatajinywa na kurudishwa kwao maana watu wemezidi kuja nchi za watu na kujilipua kusema wakimbizi na kufanya wengine maisha kuwa magumu unaenda kuomba VISA unanyimwa maana mnajulikana kwa kuvamia nchi za watu.....MUNGU atamlipa mchana asidhani kuwa mkimbizi ndio maisha marahisi angalia wasudan/wasomali/wakongo/ethiopia wanavyoteseka wanafanyishwa kazi utadhani watumwa ....
lazima kuna sababu kakimbia siajabu alikuwa housegirl manake ukiwa mgeni watu wana mchezo wa kunyanyasa wenzetu, tutizame pande zote mbili. vile vile kwanini watu mnakimbilia tu kajilipua?? sababu hata kama kajilipua ni ana weza kusema alikuwa abused kwa huyo mabula???
kila la heri wote ngoja nikabebe boksi
wamuulize vizuri huyu aliyekuwa anakaa nae sababu mtu ataondoka tu na kukimbia msiba wa mamake? sie waafrica vifo vya mama na baba huwa ni vikubwa.
mwekeeni private investigator akikutwa kajilipua na nini arudishwe hana adabu lakini kama kakimbia sababu ya abuse basi watiwe hatiani ma abuser wake.
Post a Comment