
WAKATI ipo hivyo kwa upande huo, utafiti unaeleza kuwa wanaume wengi huwa hawakubali neno “nimechoka” ambalo anaweza kuambiwa na mwenzi wake. Inaelezwa kuwa asilimia kubwa ya wanawake walio kwenye ndoa ambao walijaribu kueleza hisia zao kwa ‘mamista’ wao kuwa hawapo tayari kwa tendo, walibakwa.
Inawezekana hili likawa halipati kujadiliwa sana kwa sababu mpaka leo kuna wanawake bado wanaamini kubakwa na waume zao ni sawa. Kinachowapa unyonge huo ni imani kwamba mwanaume ana haki zote za kimsingi za kuutawala mwili wake. Ziangalieni nyumba nje ya kuta, ndani kuna mengi!
Ni vizuri kujitambua. Mfumo wa kubakana haukubaliki! Watu waelewe kuwa ni kosa kubwa kubana unyumba, kwani wengi wao wamejikuta wakisalitiwa kwa sababu hiyo. Yapo mambo ambayo natakiwa nikuchambulie ili kufahamu thamani ya tendo! Naamini baada ya kusoma, utaelewa tofauti ya chumvi na sukari.
Mapenzi ni tendo la furaha. Wakati wa utekelezaji huwa ni sherehe tupu endapo wahusika watakuwa wamekubaliana kwa moyo mmoja. Yaani hisia zao ndizo zilizowashawishi kuingia kwenye ‘bwawa spesho’. Kinyume chake ni mateso na ndiyo chimbuko la tuhuma za wanandoa kubakana.
Kama nilivyoeleza wiki iliyopita, utafiti unaeleza kuwa wanaume wengi huwa hawakubali neno “nimechoka” ambalo ni kawaida kutamkwa na wanamke. Ni lugha ambayo huitumia ili kukwepa ushawishi wa wenzi wao ambao huwataka kuingia nao kwenye sayari ya vionjo vya kimahaba.
Hata hivyo, lipo jibu la kitafiti kwamba asilimia kubwa ya wanawake walio kwenye ndoa ambao walijaribu kueleza hisia zao kwa ‘mamista’ wao kuwa hawapo tayari kwa tendo, walibakwa. Wakati mwingine hili hubebwa kwa tafsiri kuwa ni jambo la kawaida.
Inawezekana hili likawa halipati kujadiliwa sana kwa sababu mpaka leo kuna wanawake bado wanaamini kubakwa na waume zao ni sawa. Kinachowapa unyonge huo ni imani kwamba mwanaume ana haki zote za kimsingi za kuutawala mwili wake. Ziangalieni nyumba nje ya kuta, ndani kuna mengi!
“Mwanamke akiolewa haruhusiwi kulala akiwa amevaa kabati!” Ni msemo ambao unavuma mno. Kinachotajwa hapo ni kuwa anayekubali kuolewa, moja ya masharti ni kukubali ombi la mwenzi wake wakati wowote. Ni kweli? Usiku amelala, ghafla anashtuka uzito umeongezeka kifuani, kuangalia, kumbe ni mume anatimiza haja zake!
Hiyo ni sahihi? La hasha, mapenzi hayapo hivyo! Nimesema kuwa tendo la mapenzi linahitaji uhuru wa hisia. Kulazimisha ni kumuumiza. Kukwea juu ya mwenzako bila taarifa ni unyanyasaji. Kila mtu ana wajibu wa kuheshimu mwili wa mwenzake na azitangatie ‘u-tayari’.
Ni vizuri kujitambua. Mfumo wa kubakana haukubaliki! Ila ni vema pia watu wakaelewa kuwa ni kosa kubwa kubana unyumba, kwani wengi wao wamejikuta wakisalitiwa kwa sababu hiyo. Yapo mambo ambayo natakiwa nikuchambulie ili kufahamu thamani ya tendo!
Itaendelea wiki ijayo.
www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment