ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 6, 2012

KASEBA VS CHEKA NANI ZAIDI UWANJA WA TAIFA KESHO


Bondia Japhert Kaseba kushoto na Francis Cheka wakioneshana umwamba wa kila mmoja kutaka kumchakaza mwezake wakati walipopima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika katika uwanja wa taifa siku ya jumamosi katikati ni mratibu wa mpambano huo Kaike Siraju.

Baadhi ya Mabondia na Makocha wakisubili kupima uzito kwa mabondia kwa ajili ya Mpambano wa siku ya sabasaba katika tamasha la matumaini
Bondia Francis Cheka akipima uzito kwa ajili ya kumkabili mpizani wake Japhert Kaseba kesho katika uwanja wa Taifa wakati wa Tamasha la matumaini ambapo kutakuwa na burudani mbalimbali mbali
Mratibu wa mpambano wa ngumi Kaike Siraju katikati akiwainua mikono juu mabondia Japhert Kaseba kushoto na Francis Cheka baada ya kumaliza kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya sabasaba katika uwanja wa taifa wakati wa Tamasha la Matumaini kwa Watanzania litakalojumuisha burudani mbali mbali
Bondia kutoka Kambi ya Ilala Ibrahim Class akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Sadik Momba utakaofanyika Kesho katika uwanja wa Taifa
 Bondia toka kambi ya Ilala Ibrahim Class akipima Afya kwa ajili ya mpambano wake na Sadik Momba utakaofanyika kesho katika uwanja wa taifa
Bondia Francis Cheka akipima Afya kwa ajili ya mpambano wake na Japhert Kaseba utakaofanyika kesho katika uwanja wa Taifa

No comments: