Mkuu wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, Gerald Guninita amemkamata na kumweka chini ya ulinzi, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Udekwa kilichopo Tarafa ya Mahenge, Obadiah Lubugo, kwa kutochangia Sh. 70,000 za Mbio za Mwenge.
Lubugo, ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alionja kadhia hiyo juzi baada ya kuelekeza fedha hizo katika manunuzi ya chaki kwenye Shule ya Msingi Udekwa.
Rekodi ya kijiji hicho inaonyesha kuwa tangu Tanzania ilipopata uhuru mwaka 1961, Mwenge huo haujawahi kupita hapo hadi hivi sasa, tukio ambalo linatoa tafsiri tofauti na michango halisia ya wananchi.
Akilalamikia hatua hiyo mbele ya mkutano wake na waandishi wa habari, Lubugo alisema amehuzunishwa na hatua hiyo ya Mkuu wa Wilaya kumkamata na kumlazimisha kulipa fedha hizo wakati Mwenge huo ulishapita Juni 22, mwaka huu.
“Amenikamata na kunilazimisha kulipa huo mchango wakati shuleni (Udekwa) kulikuwa hamna hata chaki na tulipeleka kwa Mkuu wa Shule Sh. 274,000 na akasaini kwa ajili ya manunuzi ya chaki na mambo mengine. Lakini cha ajabu alipofika kijijini kwetu, DC akasema kama sina fedha hizo nikae Polisi kuanzia tarehe 29 mwezi Juni hadi Julai 2, mwaka huu ndipo nipelekwe ofisini kwake," alilalamika.
Lubugo alisema Sh. 274,000 zilizoelekezwa na serikali ya kijiji kwenda kwenye manunuzi ya chaki na masuala mengine ya kitaaluma, zilipitishwa na wajumbe wa serikali yake kutokana na shule hiyo kutopata mgawo wa fedha serikalini kwa matumizi hayo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo, yenye kumbukumbu namba KDC/A4/1/30 ya Aprili 12, mwaka huu, kwenda kwa maofisa watendaji wa kata, ikielekeza maandalizi na michango ya Mbio za Mwenge wa Uhuru, inaagiza kila kijiji kuchangia Sh.70,000.
“Sehemu ya barua hiyo inaeleza hivi: "Mwisho wa kuwasilisha michango hiyo ni tarehe 10 Mei, 2012 na kila Mtendaji wa Kijiji anapaswa kupatiwa risiti. Ningependa mhimize suala la uchangiaji wa Mbio za Mwenge kwa vijiji vilivyo kwenye kata zenu ambapo kila kijiji kinatakiwa kuchangia Sh.70,000.”
NIPASHE ilipomtafuta Mkuu wa Wilaya hiyo kwa njia ya simu ya mkononi pamoja na kumtumia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), kwa ajili ya kumtaka kuthibitisha au kukanusha madai hayo, lakini hakujibu.
Afisa Habari wa wilaya hiyo aliyejulikana kwa jina moja la Christopher, aliwajibu waandishi wa habari kwamba hawezi kupokea simu na ameagiza afuatwe kijiji cha Lundamatwe.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment