Abebeshwa zigo la EPA
Hali ya hewa yachafuka
Hali ya hewa yachafuka
Kwa mara nyingine tena, Bunge jana lilitawaliwa na kauli zilizojaa hisia kali, mivutano, malumbano na maneno ya kuudhi na kashfa, saa chache kabla ya kupitisha makadirio ya matumizi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Safari hii, hali ya utulivu ilitoweka na kuibuka hisia kali na maneno ya kashfa baada ya Mbunge Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba, kutaka kiti cha Spika kitoe agizo au maelekezo kutokana na hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa wizara hiyo, ambayo alisema imejaa uchochezi.
Nchemba alisema hotuba hiyo iliyowasilishwa bungeni jana na Msemaji Mkuu wa Kambi hiyo, Ofisi ya Rais, Profesa Kulikoyela Kahigi, imewatuhumu walimu wa shule za msingi kwamba, wamekuwa wakifanya biashara shuleni wakati wa masomo.
Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Sabreena Sungura, alisimama na kuomba kutoa taarifa, aliporuhusiwa, alisema Kambi ya Upinzani katika hotuba yake hiyo haijasema kuwa walimu wote hufanya hivyo, bali baadhi yao.
Nchemba aliikataa taarifa ya Sungura na kusema arudi darasa la kwanza akajifunze kusoma.
Mnyika alisimama na kuomba kutoa taarifa. Aliporuhusiwa, alisema kinyume cha kanuni za Bunge, Nchemba, mbali ya kuzungumza mambo ambayo hana uhakika nayo kwa kuwa ndani ya hotuba ya kambi hiyo hakuna neno ‘walimu wote’, pia alitoa maneno ya kuudhi.
Baada ya kueleza hivyo, ulizuka mvutano mkubwa wa kikanuni kati ya Mnyika na Mwenyekiti wa Bunge, Jenista Mhagama, katika mvutano huo alimtaka Mnyika kutaja maneno ya matusi yaliyotolewa na Nchemba.
Mnyika alisema kwa kumwambia Sungura arudi darasa la kwanza akasome, Nchemba alitoa matusi dhidi yake (Sungura).
Kutokana na hilo, Mhagama alimtaka Nchemba kufuta kauli yake hiyo, ambayo alitii na kuifuta, lakini akasisitiza kuwa hotuba hiyo kambi ya upinzani haikuwatendea haki walimu.
Nchemba alisema hotuba hiyo ya kambi ya upinzani pia haikuwatendea haki usalama wa taifa kwa kueleza kwamba hawajawahi kusikika wakizuia mipango ya wananchi kuibiwa licha ya kuwa na taarifa za kutosha.
Kauli hiyo ilimfanya Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, kuomba kutoa taarifa.
Aliporuhusiwa alisema kinachofanywa na Nchemba ni kusoma sehemu ya kifungu cha maneno ya hotuba hiyo na hasomi kifungu chote kwa maana ya muktadha.
Hata hivyo, hoja yake ilikataliwa na Mhagama kwa maelezo kwamba kanuni ya Bunge aliyoitumia kutoa hoja yake, haikumruhusu kufanya hivyo.
Mhagama alimruhusu Mnyika, ambaye alisema kilichoelezwa na hatuba hiyo ni sahihi kwa kuwa ushahidi kuhusu usalama wa taifa kuzuia baadhi ya mambo kujadiliwa na Bunge ulikwishawahi kutolewa bungeni.
Mnyika hakuishia hapo, bali alikwenda mbali zaidi kwa kusema Nchemba aliwahi kuwa mtumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambayo ilikumbwa na kashfa za ukwapuaji wa mabilioni fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Nje (Epa) na kwamba, naye ni mmoja wa watuhumiwa.
Kauli hiyo ya Mnyika ilimfanya Mhagama kusimama na kumpa Mnyika siku saba kuwasilisha ushahidi kwamba, Nchemba ni mmoja wa watuhumiwa.
Mvutano huo, pamoja na malumbano, hisia kali na kashfa, vilimfanya Simbachawene kusimama na kupinga vikali tabia hiyo.
Alisema kwa jinsi alivyoshuhudia kauli na mwenendo mzima wa uendeshaji wa Bunge unavyokwenda, kanuni nyingi za Bunge zinavunjwa, ikiwa ni pamoja na wabunge kuhama kwenye shughuli mahasusi za Bunge na kuendekeza mambo yanayolivunjia Bunge heshima mbele ya watu wanaofuatilia shughuli zake.
Hoja hiyo ya Simbachawene ilimfanya Mhagama kutumia mamlaka ya kiti cha Spika kusitisha mvutano uliokuwa ukiendelea na kumruhusu Nchemba kuendelea kuchangia.
Nchemba akijibu tuhuma za Mnyika, alisema alijiunga na BoT mwaka 2006 wakati huo ukwapuaji wa fedha katika benki hiyo ulikwishafanyika.
Alisema wakati wa ukwapuaji wa fedha za EPA unafanyika BoT, yeye alikuwa bado anasoma Chuo Kikuu na kusema: “Wakati huo hata mlango wa Benki Kuu siujui.”
Nchemba alisema baadhi ya wabunge wameingia bungeni kiundugu na kwamba, hata wanavyokaa bungeni hukaa mithili ya watu ambao wako sebuleni.
Hata hivyo, Mhagama alisimama na kumtaka afute kauli, ambapo alitii na kuifuta.
Awali mvutano mwingine uliibuka, baada ya Mbunge wa Kisarawe (CCM), Selemani Jafo, kuruhusiwa na Mhagama, kujadili kadhia ya kutekwa, kuteswa na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka.
Hali hiyo iliibuka tena wakati Mbunge wa Chakechake (CUF), Mussa Haji Kiombo na Nchemba, wakichangia mjadala wa hotuba ya makadirio ya matumizi ya ofisi hiyo.
Pia iliibuka baada ya Nchemba, wakati akichangia mjadala huo kuongea mambo yaliyoonekana kuwa hayakuwa na uhakika na kutoa lugha ya kuudhi, kabla ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, kuingilia kati na kuizima hoja.
Akichangia hoja hiyo, Jafo, alisema ni uchunguzi pekee ndiyo utakaoweza kuisaidia serikali kuondokana na kupakwa matope kwa kuhusishwa na kadhia ya kutekwa nyara, kuteswa na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Ulimboka.
Alisema mbali na kuinusuru serikali na hilo, uchunguzi pia ndiyo utakaosaidia kurejesha hali ya amani nchini kufuatia kadhia hiyo, kwani kuna watu wanaotaka kutumia sakata hilo kwa manufaa binafsi.
Kauli hiyo ilimfanya Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, kuomba utaratibu na aliporuhusiwa na Mhagama, Mnyika, alitumia kanuni ya tano ya Bunge kumuomba mwenyekiti huyo aruhusu mgomo wa madaktari ujadiliwe.
Hata hivyo, Mhagama alikataa hoja ya Mnyika, kwa maelezo kwamba, suala hilo lilikwisha kuamuliwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Baada ya kueleza hayo, Mhagama, alimruhusu Kombo, kuchangia mjadala wa makadirio ya mapato ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Kombo alianza kwa kuwashukuru madaktari kwa kuheshimu kauli ya Rais Jakaya Kikwete iliyowataka pamoja na mambo mengine, kurejea kazini.
Hata hivyo, wakati akiendelea, Mnyika aliomba tena kutoa taarifa na aliporuhusiwa na Mwenyekiti wa Bunge, alisema baadhi ya vyombo vya habari vya jana viliwakariri madaktari bingwa wakisema Rais Jakaya Kikwete alipotoshwa.
Hivyo, akasisitiza hoja yake ya kutaka ripoti ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii kuhusu mgomo wa madaktari ipelekwe bungeni ikajadiliwe.
Mbunge wa Kondoa Kaskazini (CCM), Juma Nkamia, alisimama na kutoa taarifa, ambapo alisema Bunge linaongozwa kwa kanuni na kwa hiyo haliwezi kuendesha mambo yake kwa kuongozwa na vyombo vya habari.
Baada ya Nkamia kutoa hoja hiyo, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Pauline Gekul, pia aliomba kutoa taarifa na aliporuhusiwa na Mhagama, aliungana na Mnyika kwa kusisitiza ripoti ya kamati hiyo ya Bunge ipelekwe bungeni ikajadiliwe.
Mhagama alisimama na kumtaka Kombo atamke iwapo taarifa zote zilizotolewa kama anakubaliana nazo au la.
Kombo alisema anazikitaa taarifa zote kwa sababu wabunge wa Chadema juzi walikataa kuhusika na kuchochea mgomo wa madaktari, lakini jana alipowashukuru madaktari kwa kuheshimu kauli ya Rais Kikwete, wabunge wa Chadema hawakukubaliana na hilo.
Hali iliharibika zaidi baada ya Kombo kutamka kwamba, chama chake cha CUF ni kizuri kwa kuwa kinaongozwa na msomi, Mwenyekiti wake akiwa ni Profesa, lakini akasema kuna chama kingine, ambacho hakukitaja ila kinaongozwa na mtu aliyemwita kwa jina la ‘Disco joka’.
Mhagama hakukubaliana na kauli hiyo, alisimama na kumtaka Kombo kuifuta, ambayo alitii amri hiyo.
Baada ya Kombo kuchangia, alifuatia Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Amina Abdallah Amour, Mbunge wa Korogowe Mjini (CCM), Yusuph Nassir na Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR-Mageuzi), James Mbatia, ambao wote kwa nyakati zao tofauti, walichangia makadirio hayo kwa utulivu.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment