HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili, Kitengo cha Taasisi ya mifupa
(Moi),imeelemewa baada ya wagonjwa kufurika katika wodi na kusababisha
wengi wao kulala chini na kwenye korido wakati wakipatiwa matibabu.
Mwananchi
imeshuhudia baadhi ya wagonjwa katika taasisi hiyo, wakiwa wamelazwa
kwenye sakafu ndani ya wodi na wengine wakiwa kwenye korido za
hospitali hiyo.
Moja ya wodi zilizoathirika na msongamano mkubwa
wa ongozeko hilo la wagonjwa ni Wodi ya Sewahaji inayotumiwa na Taasisi
ya Mifupa(Moi) pamoja na Hospitali ya Muhimbili.
Akizungumza na
Mwananchi , msemaji wa Taasisi ya Moi, Almasi Juma alisema kufurika kwa
wagonjwa katika kitengo hicho kumetokana na athari za mgomo wa madaktari
uliomalizika katika siku za hivi karibuni.
“Katika kipindi cha
mgomo wagonjwa waliopatiwa huduma walikuwa ni wa dharura pekee, na hivyo
kupelekea kurundikano kwa wagonjwa wa kawaida,”alisema Almas na
kuongeza:
“Kitengo hiki pia kinahudumia idadi kubwa ya wagonjwa
wanaotokana na ajali, hali hii imechangia kwa kiasi kikubwa kujaa kwa
wodi zetu pamoja na zile tulizopewa na hospitali ya Muhimbili”.
Almasi
alisema, tatizo hilo la mrundikano wa wagonjwa linaweza kuchukua muda
kidogo mpaka athiri za mgomo ziishe ndiyo hali itatengemaa na kuwa ya
kawaida.

No comments:
Post a Comment