SOKA la Nigeria limeingia doa kubwa baada ya wachezaji 15 wa timu ya taifa ya vijana ya nchini hiyo chini ya miaka 17 kubainika kuwa wamezidisha umri kwa mujibu wa kipimo cha Magnetic Resonance Imaging (MRI).
Wachezaji hao walibainika kuzidi umri huo baada ya kupimwa kama ilivyoangizwa na Fifa kuwa wachezaji wote wanaoshiriki mashindano yanayohusu umri kupimwa kabla ya kushiriki michuano hiyo.
Kwa mujibu ya taarifa za magazeti ya Nigeria zilisema mapema mwezi huu Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) liliamuru wachezaji wote 40 wanaunda kikosi cha U-17 waliokuwa kambini kupima kipimo hicho ili kubaini wale waliodanganya umri kati yao.
Idadi hiyo kubwa ya wachezaji walizidi umri ni pigo kwa kocha wa U-17, Manu Garba, ambaye kwenye uteuzi wake kuna wastani wa mchezaji moja mkubwa kwa kila wachezaji watatu wa kikosi hicho.
Tayari NFF imechukua uamuzi wa kuwatimua wachezaji hao na kuongeza wengine 18 waliokuwa wakichezea kikoso cha Nigeria U-15 kuziba pengo hilo.
Uamuzi huo umechukuliwa ili kupata kikosi kingine cha Nigeria kitachokuwa kambini kwa lengo la kujiandaa na mechi ya mtoano ya kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika 17 dhidi Niger.
Waziri wa Michezo, Bolaji Abdulahi kuanzia sasa wataanzisha sheria ambayo wachezaji wote wa U-17 watachukuliwa wale waliokuwa shuleni tu, ili kuondokana na aibu hiyo.

No comments:
Post a Comment