Kwa ndugu Watanzania wenzetu
Kwa niaba ya Watanzania waishio nje ya nchi,
DICOTA inachukua fursa hii ukiwa ni wakati mgumu kwa Taifa letu na kwa wananchi
wote wa Tanzania hususani kwa ndugu jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao
katika ajali ya meli MV Skagit.
DICOTA, tumepokea huu msiba kwa mshtuko na majonzi makubwa. Tunatambua kwa hakika kuwa hiki ni kipindi kigumu kwa wafiwa na Taifa letu kwa ujumla. Pamoja na umbali wetu tunapenda kuwahakikishia ndugu zetu kwamba tuko pamoja nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa kwa taifa letu.

Kwa wale waliopata majeraha, lakini maisha yao
yakasalimika tunawapa pole sana na Mwenyezi Mungu awaponye haraka ili muweze
kurudi katika afya zenu za kawaida na kuweza kuungana na familia na ndugu zenu
katika kulijenga Taifa letu.
Tunachukua nafasi hii
pia kuwashukuru Viongozi wa Serikali, Mashirika ya kiserikali na yasio ya
kiserikali, watu mmoja mmoja na taasisi zote kwa juhudi zao za kuokoa maisha ya
wenzetu.
Mwisho tunatoa
changamoto kwa jumuiya zote duniani kuona ni kwa namna gani tutaweza kuwasaidia
hawa wenzetu, sasa na hata baada ya hali ya kuokoa maisha ikiwa imetulia pia
kutafuta njia zitakazoweza kufuta kabisa ajali za aina hii sizitokee tena.
Mungu Ibariki
Tanzania, Mungu wabariki watu wa Tanzania na atuwezeshe kukipita kipindi hiki
kigumu tukiwa na mshikamano ulio imara kama Taifa.
Uongozi wa DICOTA (Diaspora Council of Tanzanians in
America)
No comments:
Post a Comment