ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 18, 2012

MV SKAGIT ILINUNULIWA TOKA WASHINGTON STATE, NCHINI MAREKANI

The MV Skagit, in a photo from the WSDOT's unsuccessful attempt to sell the boat on eBay.
MV Skagit ni Boti iliyoundwa mwaka 1989 Nchini Marekani iliuzwa pamoja na Boti nyingine iitwayo MV Kalama kwa gharama ya $400,000 kwa Scope Community Consultants of Port Coquitlam ya Zanzibar na ilikua inasafirisha abiria kati ya Seattle na kisiwa cha Vashon Jimbo la Washington State, Nchini Marekani na ilikua idumu kwa miaka 25 tangu kuundwa kwake na mwaka huu ndio ilikua miaka yake wa mwisho mwisho. 


MV Skagit ilisimamishwa shughuli za kusafirisha abiria mwaka 2009 na Washingon State kujaribu kuiuza kwenye eBay pamoja na MV Kalama kwa bei ya $ 300,000 kila moja, ndipo mwaka 2011 Scope Community Consultants of Port Coquitlam ilizinunua boti hizo na kusafirishwa na Meli ya mizigo kuelekea Zanzibar.


Boti hii ya MV Skagit ina urefu wa futi 112 (34.1 m)  na ilikua na jumula ya hp 2,840 kutoka kwenye ingini 4 za dizeli na uwezo wa kubeba abiria 250.


CHANZO: THE SEATTLE TIMES

1 comment:

Anonymous said...

mkuu mimi ndo maana napenda sana kuingia kwenye blog yako kila siku hata kama nikiwa busy kichizi natafuta nafasi japo dakiki kadhaa ningiye. napenda sana hii blog yako mkuu kwa sababu unajua jinsi ya kutafuta habari cheki kama habari hii uliyotuwekea nimetazama blog kibao na sijaona habari hii. aise ubarikiwe daima mkuu big up man

mdau New York