SALAMU ZA RAMBI RAMBI
CCM DMV
WASHINGTON DC
Wanachama wa CCM tawi la DMV
tunaungana na watanzania wenzetu popote duniani kutoa salamu Za rambi rambi kwa Kuondokewa na MZEE WETU MKONGWE WA CHAMA CHA MAPINDUZI,
NDUGU AZZAN ALLY MANGUSHI .
Mzee wetu, atakumbukwa kwa hoja zake za kuchangia mambo
mbali mbali ndani ya chama cha mapinduzi hasa kipindi alivyoweza kushika nafasi
ya mjumbe wa halmashauri kuu ya kinondoni-Dar es salaam na mambo mengi yaliyoweza
kulijenga taifa la Tanzania. Wanachama wa ccm wameondokewa na kiongozi imara na
shupavu katika siasa.
Sisi wananchama wa CCM tawi la
Washington, DC Maryland na Virginia tunatoa salamu za rambi rambi kwa ndugu wa marehemu
na wanachama wa ccm popote duniani katika kipindi hiki kigumu.
Mungu ailaze roho ya mzee wetu huyu
peponi
Amin
Uongozi
Tawi la ccm-DMV
Marekani

No comments:
Post a Comment