ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 18, 2012

SPIKA WA BUNGE AWAKATALIA WABUNGE KUSHILIKI MSIBA ULIOTOKANA NA AJALI YA MELI LEO BAADHI YA WABUNGE WAMESUSIA BUNGE

Spika wa bunge la Tanzania Anna Makinda 

Spika wa bunge akataa wabunge kushiriki msiba ulio tokana na ajali ya meli na kupelekea baadhi ya wabunge kususia kikao cha bunge. 
Baada ya Mbunge wa Wawi kupitia tiketi ya CUF Hamadi Rashid kuomba spika wa bunge kusitisha shughuli za bunge kwaa jili ya ajali ya meli iliyotokea huko Zanziba na spika wa bunge kukataa, Baaadhi ya wabunge idadikubwa wakiwa na wa vyama vya upinzani wameemua kutoka bungeni na kuacha shughuli za bunge zikiendelea kwa wabunge walio baki.

Lakini bunge likiendelea ndipo ilifikia Muheshimiwa Emanuel Mchimbi alitoa hoja ambayo ilisababisha kikao cha bunge kuahirishwa baada ya baadhi ya wabunge kuwa wamesha toka.
Kikao cha bunge kimeairisha mpaka kesho saa tatu asubuhi.

Kwa waliowahi kwenda zanzibar au kutofika, ajali imetokea eneo linaitwa Chumbe kwenye visiwa viwili unavyovipita ukikaribia zanziba. Na ndipo panapo panaposemekana ajali imetokea.

3 comments:

Anonymous said...

Serekali ya muungano haina mpango wowote sioni kiongozi hata mmoja wa bara ngazi ya taifa kashiriki katika ajali hii kwani waliopatwa na ajali si wazanzibari bali ni raia wa jamuhuri ya muungano wa TANZANIA,na wageni ambao wanaliingizia taifa pato la utalii,nafikiri rais wa Tanzania, angekua wakwanza kwenye tukio hili cha ajabu rais yuko busy kusafiri dunia nzima anachokitafuka hakijulikana maisha mabovu watu wanakufa,sijui kwa nini badala ya kua rais angebaki kua waziri wa mambo ya nchi za nje,kwani hiyo ndio kazi nafikiri inamfaa,kwai hata mgomo wa madaktari rais anadai wadai malipo makubwa ok kama malipo makubwa unapata wapi pesa za kusafiri kila siku dunia nzima ,kaa nyumbani tatua matatizo ya wananchi wako kwani una mabalozi na kila wakilishi watakuwakilisha.na cha kushangaza zaidi hata bunge halijaliETI SPIKA HAWEZI KUAHIRISHA KIKAO CHA BUNGU BAADA AJALI KUBWA KAMA HII KUTOKEA SEREKALI GANI HII.WANANCHI AMKENI.

Anonymous said...

Hii ni kweli kabisa,

Anonymous said...

Ubinafsi umewazidi sana na ndiyo maana hawajali wananchi wao,wanaweka maslahi mbele kuliko ubinaadam!Viongozi wasiyojali wananchi wao inabidi waondolewe haraka sana!Viongozi wapo kwa ajili ya huduma kwa raia na nchi yao,na tunalipa kodi ili tupate huduma nzuri,lakini matokeo yake mafisadi ni wengi na kutulia pesa zetu bure tu!Sasa tumechoshwa na serikali hii ya unyonyaji!Watanzania tuamkeni sasa na tushirikiane kwa pamoja!