ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 20, 2012

TAKC - Salamu za rambi rambi, Ajali ya MV. Skagit


Jumuiya ya watanzania waishio Kansas City na vitongoji vyake imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali ya Meli ya MV. Skagit iliyotokea wiki hii karibu na kisiwa cha Chumbe.
Tunaungana na watanzania wote kawapa pole ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao na vile vile  tunawatakia kila la heri majeruhi wote wapate kupona haraka na kurudi kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa Taifa.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
Imetolewa na:-
John Adhero – Raisi wa Jumuiya ya Watanzania Kansas City (TAKC).
email: kamati_takc@hotmail.com

No comments: