Siku moja baada ya wabunge wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari wakidaiwa kumpigia debe Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia chama hicho, Zitto Kabwe kuwania urasi mwaka 2015, wabunge hao wameibuka na kukana kufanya hivyo.
Wabunge wa Chadema walionukuliwa na gazeti moja la kila siku (Sio Nipashe) wakidaiwa kumsafishia Zitto njia ya urais wa 2015 ni Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari na Halima Mdee, Kawe.
Katika kujiweka mbali na mpango huo, Nassari jana aliamua kusambaza taarifa kwa vyombo vya habari akisema kuwa hajawahi kutamka wala hatarajii kutamka maneno hayo, bali ni maneno ambayo alilishwa na chombo cha habari kilichoandika habari hiyo.
Nassari alisema akiwa kama Mtanzania ambaye ni mwanachama wa Chadema kinachoamini kuwa suala la urais si kipaumbele, bali muhimu kwa wakati huu ni kushughulika kujua mizizi au vyanzo vya matatizo yanayowakabili Watanzania ikiwemo umaskini, ujinga, maradhi, ufisadi na utawala mbovu wa Chama Cha Mapinduzi CCM.
“Kama ambavyo chama changu, Watanzania wengine makini na mimi mwenyewe, naamini kuwa kwa sasa suala la muhimu kwetu kama Taifa ni kutafuta mizizi au vyanzo vya matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii ya Watanzania,” alisema Nassari katika taarifa yake.
Alisema Chadema na yeye mwenyewe kama mwakilishi makini wa wananchi, inafahamika kuwa suala la urais linategemea mahitaji ya Watanzania na kamwe haliwezi kuamriwa kwa kufuata matakwa na utashi au uchu wa watu binafsi kwani linafuata katiba, kanuni na taratibu za chama hatua ambayo haijafikiwa kwa sasa.
Kwa upande wake, Mdee alitoa taarifa ya kukanusha akisema habari iliyoandikwa na kumnukuu yeye ni ya uongo na imesigina misingi ya uandishi na hususani katika kufuata maadili ya taaluma ya uandishi wa habari kwa kiwango cha kufanya moja ya dhambi kubwa ya kukilisha maneno chanzo cha habari.
“Habari hiyo imeniletea usumbufu mkubwa hasa kwa wananchama wa chama changu cha Chadema ambao wanajua kuwa chama chao makini ni mahiri katika kufuata katiba, kanuni na taratibu katika kuendesha mambo yake kwa manufaa ya watu wote,” alisema Mdee.
Gazeti lililowanukuu wabunge hao liliripoti kuwa Mbunge Nassari alidai kuwa Mkoa wa Kigoma umejitokeza wazi kuwa na wanasiasa mahiri na wenye vipaji vya hali ya juu katika kupigania maslahi ya wananchi pamoja na kupambana na ufisadi unaodidimiza uchumi wa taifa letu na kuwanufaisha wachache kwa kutumia nafasi zao.
”Leo, ni mara yangu ya kwanza kufika Kigoma, lakini kwa jinsi ninavyoona mpangilio mzuri wa shughuli hii, naamini kabisa kuwa, Zitto Kabwe aliyeandaa hafla hii na kuwakusanya wasanii wa Kigoma kuwa kitu kimoja anafaa kabisa kuwa rais ajaye wa Taifa letu. Na haya ninayasema kwa uhakika bila hata chembe ya mzaha," gazeti hilo lilinukuu Nassari.
Mdee alinukuliwa akidaiwa kumliza Zitto jukwaani baada ya kumuelezea kuwa ni ‘jembe’ katika mambo mbalimbali na mtu mwenye uchungu na maendeleo ya taifa.
Mdee aliyepewa nafasi ya kuwasalimia Wananchi alisema amekuwa na Zitto tangu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kwamba kutokana na ujasiri na umahiri wake katuika kutetea masilahi ya wanyonge na taifa, anafaa kuwa mmoja wa viongozi wa juu katika Taifa.
”Ndugu zangu watu wa Kigoma, kwa kweli mna bahati sana, achilia mbali kuwa na vipaji katika sanaa ya muziki na michezo hasa mpira wa miguu, lakini mna wanasiasa wakali ambao ni tishio hapa nchini. Mimi namkubali sana Zitto Kabwe na ninaamini kuna siku atakuwa kiongozi wa juu katika nchi yetu," Mdee alinukuliwa akisema.
Wabunge hao pamoja na Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe, walitajwa na gazeti hilo kuwa walitoa kauli za kumsafishia njia ya urais Zitto wiki iliyopita katika Tamasha alililiandaa na kuwakutanisha wasanii wa Mkoa wa Kigoma katika Uwanja wa Tanganyika mkoani humo.
Mei mwaka huu, Zitto alizungumza na vyombo vya habari akiwa mkoani Mbeya na kusema kuwa anautaka urais, lakini hatarajii kugombea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Zitto pia alisema uamuzi wa kugombea urais ni lazima utokane na ridhaa ya chama chake. Hata hivyo, alisema hatarajii kugombea uongozi ndani ya chama hicho utakaoaza mwaka huu na kukamilika mwakani.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment