Advertisements

Monday, July 30, 2012

Vigogo Chadema Kortini kwa kumtusi Mbunge-Mwananchi

VIGOGO wawili wa Chama cha Maendeleo na Demokrasi (Chadema), leo Jumatatu asubuhi wanatarajiwa kuburuzwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mjini hapakujibu tuhuma ya kumtolea lugha ya matusi Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigullu Lameck Mwigullu.

Vigogo hao ni pamoja naOfisa sera na utafiti wa ChademaMakao makuu,Waitara Mwita Mwikwabe (37) na mshauri wa Chadema na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam, DkKitila Mkumbo wotewakazi wa jijini Dar-es-salaam. 

Washitakiwa hao  kwa nyakati tofauti wiki mbili zilizopita,walipandishwa katika mahakama hiyo na kukana kutenda kosa hilo.

Kwa mujiubu wa mwanasheria wa Serikali,Seif Ahmedalidai mbele ya hakimu wa mahakama hiyo,Ruth Massamu kuwa Julai 14, mwaka huu saa 10.00 alasiri huko katika kijiji cha Nguvumali kata ya Ndago wilayani Iramba,washtakiwa bila halali alimtusi Mbunge Mwigullu kuwa ni malaya,mzinzi na mpumbavu huku akijua wazi kuwa kitendo hicho ni kinyume na sheria.

Seif alisema washitakiwa hao bila halali,alitenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nguvumali uliolenga viongozi wa Chama hicho kuzungumza na wananchi.

Pamoja na vigogo hao, leo asubuhi vijana nane wakazi wa kijiji cha Nguvumali ya Ndago,Jimbo la Iramba magharibi,wanatarajiwa kupandishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mjini hapa,wakituhumiwa kumw
uuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (CCM) kata ya Ndago, Yohana Mpinga (30).

Washitakiwa hao ni Manase Daudi (40),Williamu Elia (33),Frank Stanley (20),Charles Leonard (36),Tito Nintwa, Fillipo Edward (30),Paulo Shakilingwa na Emmanuel John Shilla (20).

Mwanasheria wa Serikali mwandamizi, Neema Mwanda,alidai mbele ya hakimu Massamukuwa Julai 14 ,saa kumi alasiri katika kijiji cha Nguvumali kata ya Ndago,washitakiwa wote kwa pamoja,bila halali walimpiga kwa kutumia fimbo na mawe  mwenyekiti huyona kusababisha kifo chake.

Vile vile jumla ya washitakiwa 12 wanaotuhumiwa kufanya vurugu katika mkutano huo wa hadhara wa Chadema katika kijiji cha Nguvumali kata ya Ndago na kusababisha  kuvunjika kwa amani na utulivu,nao wanatarajiwa kupandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mjini hapa.

No comments: