ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 23, 2012

WAKEREKETWA CCM DMV WAMWAGA RADHI WASIKILIZE

29 comments:

maisha dunia ngumu said...

kusema ukweli siasa ni mambo makubwa yanayo takiwa mtu awe na upeo wa siasa zenyewe na akili mzunguko wa kufikiri na kueleza yale ambayo unafikiri ni matarajio ya wengi katika kufika hali halisi, kama dmv ccm wanatakiwa kufungua tawi lao hapa, bila shaka wanahitaji viongozi wengine lakini siyo hawa wanaohojiwa kwa vile hawana mvuto wa kisiasa bali wanamvuto na green walizo vaa. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Anonymous said...

Bwana Benja katumia nguvu nyingi kulaumu matusi ya vyama vya upinzani akiwa na yeye anatukana wapinzani wakati huo huo. Nafikiri tatizo kubwa hapa ni communication skills. Hata hivyo nashukuru wamekiri kuwa elimu yao hao wawili ni ya darasa la saba. Kama wangetumia nafasi hii kujiongozea elimu kidogo, nafikiri wangekuwa good communicaters ambao wangeelewa maana ya kutofautiana bila kutukanana. CCM Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!

Anonymous said...

Jamani Watanzania tuweni serious. Huu ni mzaha mkubwa. Imefika mahali sasa tujijue kwamba sisi ni nani na tunakwenda wapi. Huyu kijana anawaongoza watu gani, wa namna gani na kwenda wapi? Tuacheni mzaha, dunia inatuacha kwa kasi kubwa.
Mkaazi wa DC/VA/MD.

Anonymous said...

Benja, don't take it personal. It is just politics. At the end of the day, we are all children of God with Tanzanian nationality.

Anonymous said...

Haya ndiyo maono ya viongozi wa CCM DMV?
wana mawazo duni kweli kweli!
Kusema Chadomo ni matusi na ni utovu wa nidhamu. Bila aibu anadai CDM ndiyo wenye matusi wakati yeye anaytoa mfululizo. Nini kimemshinda kusema CHADEMA kama si hurka yake ya matusi?
Ule msemo wa "akili ndogo inaongoza akili kubwa" umefanywa kwa vitendo katika mahojiano haya.Jamaa ni watupu Upstairs bado wanadhani ni wataalamu.
Kwa upeo wao mdogo,kila wakijaribu kutoa mfano na kunukuu matukio au taratibu fulani wanaishia kujikanyaga sana mpaka unawahurumia. Majibu mengi ni ya mtawanyiko yana knowledge za kijiweni na za kibabe.
Uelewa wao ni mwembaba sana naona, na vichwani mwao kuna ushabiki wa kimakundi zaidi kuliko Siasa,Utaifa na nia ya kuijenga Tanzania.

"Ukifika Marekani ukaweza kujitegemea ni Digirii" Oh my!

"Ukiweza kuishi hapa ni Masters" My God!

Are you kidding me??

Ndiyo maana tuna watu wengi Tanzania wana PhD za kugushi, asili yake ni mawazo kama haya ya viongozi wa CCM DMV.
Kwa Mawazo kama haya ya kiongozi wa CCM DMV WaTanzania wote wana Masters??? Ni za fani ipi??
Unamjua Salma Kikwete? Mzungu akiuliza swali hili kinakuwa ni kigezo cha maendeleo na kuitangaza Tanzania. Give me a break.
LOL!

Anonymous said...

inasikitisha kuona chama cha mapinduzi kina viongozi wa aina hii, inanichanganya sana kuona hawajui nini maana ya upinzani,hawa jamaa wanatafuta umaarufu wa ujinga ni bora wakawa na mawazo ya kurudi darasani kusoma kwanza badala ya kujitangaza ujinga wao,

jee CCM inajengwa kwa chakula cha bure na drinks kama wao wanavyofikilia, na kumleta huyo diamond kwa kukopa hela kuna faida gani na wao au ndio kujitangaza kuwa wana maendeleo.kuna faida gani wao kujionyesha kwenye blog kama hawajui wanachoongea.

huu ni mzaha kuna wana ccm kibao wamekosa ada hapa marekani za kusoma mbona sijawasikia kuwasaidia ,wanakwenda home kuomba hela ili kufungua tawi hapa USA.jee kuna faida gani ya nchi, kuwa na tawi nje ya nchi,....

JAMANI WABONGO UHURU TULISHAPATA TUACHANE NA UJINGA HUU
HAKUNA RA MAANA KUWA NA VYAMA HUKU UGHAIBUNI.KWANINI TUSIWE NA JUMUIYA YETU IFANYE KAZI KAMA JUMUIYA YA WATANZANIA.

HUU UPUUZI WA KUWA NA VYAMA HUKU UTATUPELEKA KUBAYA MAANA WATU TAYARI WAMESHAANZA KUCHUKIANA KWA AJILI YA VYAMA.

JAMANI MWENYE KUWA NA WAZO LA KUWA MWANACHAMA HUKU USA NA ULAYA NI KWA FAIDA GANI ,TUJIULIZE JEE TUNAELEKEA WAPI, TUMESHAPATA UHURU JAMANI, HATUITAJI KUWA WATUMWA WA KIMAWAZO.

MWENYE KUTAKA KUWA KIONGOZI , RUDINI NYUMBANI MKAGOMBEE HUO UJINGA WENU , HATUTAKI CCM WALA CUF WALA CHADEMA. TUNAHITAJI KUWA NA JUMUIYA MOJA KWA MANUFAA YA WATANZANIA.

KAMA UBALOZI WETU NDIO KIINI CHA HAYA MAMBO, UBALOZI BADILIKENI ,MNASHINDWA KUSAIDIA JUMUIYA KIFEDHA LAKINI MKO TAYARI KUTOA HELA ILI WATU WAMLETE DIAMOND, KWA FEDHA YA KODI YA MTANZANIA , HAWA WABONGO WENGI WA HUKU USA HATULIPI KODI HOME TUNALIPA USA, KAMA KWELI TUNAIPENDA NCHI YETU TUJIANDIKISHE TUWE TUNAPELEKA HIYO KODI HOM E.
KUNA SHERIA INAYOTUTAKA WATANZANIA TULIO NJE YA NCHI KULIPA KODI LAKINI KWANINI HATULIPI?????

WEWE UNASEMA UMEJIAJIRI HUKU NJE YA NCHI NA UNAIPENDA NCHI YAKO NA UJAWAHI KULIPA KODI HATA MARA MOJA. TUACHE UJINGA TUIJENGE NCHI YETU PAMOJA TUACHANE NA VYAMA HUKU NJE YA NCHI, KUNA WABONGO KIBAO WANASOTA HUKU NJE YA NCHI, HAWANA KAZI , HAWANA VIPANDE VYA KUFANYIA KAZI, BADALA YA KUKAA NA KUWASAIDIA MNAJITANGAZA KUWA TUNAMLETA DIAMOND. NI KWA FAIDA YENU MAANA HAPO MMESHAKUSANYA MICHANGO HUKO NYMBANI NA UBALOZINI SASA MNATAFUTA JINSI YA KUITUMIA.

Anonymous said...

Hii kweli ni aibu kwa chama na watanzania wote kwa ujumla. Hawa jamaa wanaonekana upeo wao wa kimawazo na ueleo wa chama ni mdogo sana.Siasa si kitu cha kukurupukia, inabidi uwe na ueleo wa kutosha wa Katiba na Sera za chama chako kwanza, na sio kuzungumza kiushabiki tu. Inasikitisha kwa kweli

Anonymous said...

HAMNA AIBU WALA NDIYO MAANA YA SIASA KUNA KILA WATU WAKILA AINA HAWA NDIYO MASHABIKI WA NA KUNA WATU WENYE AKILI ZAO PIA WAPO HAO NDIYO WAFURUKUTWA WA CHAMA BORA HAWA KULIKO CHADEMA CHEDEMA NI MATUSI TUU NA LAWAMA UJUMBE UMEFIKA WEWE KAMA UPENDI MAMBO YA SIASA KAA MBALI NA SIASA WACHA TUWAONA WANAOPENDA KWENYE KILA CHAMA KUNA KILA AINA YA WATU SASA BASI HAO NDIYO WALIVYO KUNA WASOMI NA WASIO WASOMI KUNA WENYE AKILI NA WASIO NA AKILI SASA MNATAKA NINI ASEMA KILA MTU ANAJINSI YA KUONGEA ISIPOKUWA HAMNA KAMA CCM MKUBALI YA ISHEEEEEE

Anonymous said...

UKISIKIA CCM DAMU BASI NDIYO YUKO BENJAMINI MTAKOMA CHADOMOOOO BESHANENI SASA

Anonymous said...

Mwalimu Nyerere ambae ni muasisi wa nchi anasema ili nchi iendelee tunahitaji kuwa na vitu vinne, SIASA SAFI, UONGOZI BORA, ARDHI NA WATU.jee kwa mtazamo wangu naona hapa hakuna kabisa, kwa UONGOZI BORA, JEE KATIKA HAWA WAWILI KUNA UONGOZI HAPA, KAMA KIONGOZI ANASEMA KUFIKA MAREKANI NI DEGREE KUNA KAZI HAPA,
siamini huyu jamaa kweli kachaguliwa na wana ccm hapa DMV au kaamua kuvaa hizo nguo kwa ajili ya kupata umaarufu wa ujinga.
jee hapa kuna siasa safi kama jamaa anasema chadomo, hajui hata maana ya neno chadema maana hata ccm maana yake inaonekana jamaa hajui.

Wana DMV tuachaneni na huu upuuzi wa watu kutafuta umaarufu huku NJE wameshindwa kwenda shule ndio maana wanajipa degree za kufika USA, na kuweza kuishi ndio masters , jamaa jee huu ni upeo wa kiongozo au ndio inaonyesha ujinga wa kiongozi. CCM DMV kama mnahitaji viongozi angalieni vitu hivi, inasikitisha kuona watu tupo USA na tunajisifia ujinga wetu.

Nyerere anasema ili tuendelee tunahitaji viongozi bora na siasa safi sio ujinga wa kifikra kama huu, sasa watu kama hawa wataleta maendeleo gani kwenye nchi. jee maendeleo ni kukusanya vitabu vilivyopitwa na muda na kuvituma home kwa watu wakasome, kwanza sidhani kama kuna mengi yana faida humo kwenye hivyo vitabu ambavyo wazungu huku wanavitupa, mie mwenyewe navyo makapu mawili kama mnavihitaji naweza kuwatumia tupeni address zenu.jee swala la watu mwalimu alikuwa na maana gani wana ccm tujiulize. jee Nyerere aLIKUWA ANATAKA WATU WAKUSANYWE KWA MUZIKI NA CHAKULA CHA BURE AU VINYWAJI VYA BURE.inaonekana zile fikra za kitanzania ndania ya CCM kuwa tukileta mziki hapa na vinywaji vya bure na chakula jamaa watajaa ndio mawazo ya wana CCM hapa DMV.

Inasikitisha kuwa badala ya watu kukubali kuwa mabadiliko ya kifikra ni muhimu inabakia kwa watu kuiga yale yale ambayo tunahitaji kubadilika , inauma sana kuona hata mtu ambae anapata nafasi ya kuwa nchi kama hizi zenye siasa za kiupinzani bado hajaelimika hata kidogo.
JAMANI TUJIULIZE WATANZANIA MLIOKO HUKU JEE MMESHAONA WENZETU HAWA REPUBLIC NA DEMOCRATIC KAMA WANA MATAWI NJE YA NCHI. INASIKITISHA SANA MAANA SIJAWAHI KUONA KABISA DUNIANI KAMA DEMOCRATIC WANA TAWI TANZANIA AU KENYA, JEE MMESHAONA WANA WA MALKIA KAMA WANA TAWI LA CHAMA NJE YA NCHI. jee nini tunajifunza hapa ndugu zangu maana tunajifunza kutoka kwa wenzetu hawa walioendelea.
wenzetu wanapokuwa nje ya nchi wanakuwa nchi moja , KILA MTU ANAJALI UTAIFA WAKE. sasa sisi watanzania tuliokuwa huku USA NA UK tunatafuta nini kuwa na matawi ya vyama huku UGHAIBUNI, jee bado tunatafuta UHURU.SIJAWAHI KUONA HATA WENZETU WA SOUTH AFRICA NA NIGERIA KAMA WANA VYAMA MATAWI HUKU USA. WABONGO KWANINI TUSIIPE UIMARA JUMUIYA YETU HAPA DMV, tuachaneni na hizi siasa za utoto ambazo zinachchewa na watu wenye tamaa ya kuwa viongozi maarufu huku kisha wakisharudi bongo wajulikane. jee ubalozi wetu ni wa chama au wa watanzania. ubalozi acheni mambo ya siasa watumikieni watanzania

Anonymous said...

POTEA WEW MWANA CHADOMO KWANI HAUJUWI MAANA YA SIASA UNATAKA AJUUBIRIE NINI WANA CCM WAZURI WAPO NYUMBANI NA HAPA WAPO WAJITOKEZE TUWAONEE BASI HATA ANGEONGEA NANI BADO UNGAMKOSEA KWENDA WACHA MAMBO YA NYERERE WEWE ULIKUWA WAPI TUKUONE KAMA WEWE UNA MAANA NJOO TUKUONE CHADOMO WEWE SIO KWAMBA HAJUWI MAANA YA CHADEMA BALI WANASTAHILI KUITWA CHADOMOOOOOOOOOOOOOO MAANA WANACHOJUWA NIKUPIGA DOMO HOJA TUTAPELEKA BUNGENI LAKINI JAMAA KANIFURAHISHA KWANI WEWE KUJA AMERICA HAUJUWI NI ELIMU YA KWANZA KUMDANGANYA MZUNGU HAJUI SIO KAZI RAHISI UFANYE KAZI ULIPE BILI ZAKO NA UTUME NYUMBANI HIYO ELIMU YA KUTOSHA NYAMAZA CHADEMA MWACHE NYERERE APUMZIKE

Anonymous said...

TAFADHALI NANI ANASHIDA YA UONGOZI WEKA WAZI WACHA MAJUNGU SIO KILA MTU ANAPOINGIA KWENYE CCM ANASHIDA YA UONGOZI NA KAMA NI HIVYO BASI IONI VIBAYA KABISA NA KWA NINI KILA MTU ASIFANYE KILE ANACHOKITAKA WEWE NI NANI WA KUTUAMBIA KITU CHA KUFANYA UBALOZI UNAUSIKA NINI NA VYAMA NYAMAZA WEWE USIONGEE UTUMBO

Anonymous said...

KWANINI TUWAIGE WAKENYA WEWE VIPI KAMA UPENDI SIASA KAA MBALI NA SIASA KAA MBALI WEWE POTEA AU POTEZWE

Anonymous said...

NIKUJIBU UKIONA MTANZANIA AMEKAA HAPA HANA KAZI NI MJINGA WA MWISHO USIJARIBU TENA KUSEMA UJINGA KAMA ANATAKA KAZI ZIPO NI UVIVU WATANZANIA WAVIVU SANA WAMEKALIA MAJUNGU KAMA WEWE VILE MIJITU HAITAKI KAZI NCHI KAMA HII HAINA KAZI???WEE WACHA UJINGA WAKO NA HIVI VYAMA VITAWAPATIA WENGI KAZI CCM INAWATA MJIUNGE ILI MUWEZE KUFUNGUWA MIRAJI WAKINA MAMA WAWEZE KUJIENDELEZA KWA ACHA DOMO KAYA USITAKE KUARIBU VYAMA VYETU CHADEMA WATAFUTIENI WENZENU MIRADI YAKUFANYA NA CCM IWATAFUTIE CCM MIRADI USIANZE DOMO LAKO MBONA CHADEMA WALIVOKUWA WANAFUNGUWA HAMKUSEMA KAMA SIO WEWE NI LICHADOOMO LA NYAMAZA KABISA WALIKUJA WABUNGE 5 WACHADEMA KUFUNGUWA TAWI LA WATU 10 NYAMAZA WEWE CHADOMO USIJIFANYE UNAFUMBIA WATU HAPA HAUNA HAYA WEWE JITUMIKIE WEWE KWANZA NDIYO UTUMIKIE WENZAKO HAUNA MAANA KABISA WALA HAUKO SAWA TEMBEA HARAKA

Anonymous said...

CCM NJOO LETE MAMBO WANACHAMA TUNAKUHITAJI TUNAPESA ZETU NA TUTACHANGA TUTAFUNGUWA MIRADI YETU NA TUTAWASAIDIA WATU WETU WA TANZANIA NA AMERICA CCM OYEEEEEE KARIBU CHAMA CHETU

Anonymous said...

BENJA NA YASSIN MMECHEMSHA,KAENI KIMYA.ONYESHENI BUSARA ZENU,FICHENI UPUMBAVU WENU.

Anonymous said...

miminampongezasanahuyu benjamini, chadomomtakomakatika chamalazima pawenawatu wakuongea,lakiniyule jamaa mwinginemtupoooooo ccm hamna.from dar

Anonymous said...

UZALENDO UMENISHINDA NIMESHINDWA JIZIWIA HEBU TUACHE MAJUNGU HUKU TUSHIKAMANE KAMA WA TANZANIA MIMI MWANA CCM LAKINI KWA MWENDO HUU UNAOKUJA HAPA MAREKANI HAUNA MUELEKEO KWANI NAONA TUNATAKA KUFUATA SIASA ZA MAJUNGU YANAYO TENDEKA NYUMBANI VYAMA VYETU VYA SIASA TUNA TAKA FANYA KAMA VYAMA VYA MPIRA SIMBA NA YANGA TUSHUKURU MUNGU KUPATA BAHATI YA KUA KWENYE TAIFA HILI AMBALO WENGI WETU TUNAJIONA WAJANJA KULIKO WALIO KWENYE MATAIFA MENGINE AMBAVYO SI KWELI SASA AKILI NI NYWELE LAZIMA TUWE MAKINI NA SIASA ZA NYUMBANI WATU KUTOSANA KWA USHABIKI NAOMBA RADHI KWA WANACHAMA WA CHADEMA KWA MATAMSHI YA NDUGU YANGU CCM MWENZANGU NAPIA KUWA SIHI MABLOGER WANAO INTERVIEW WAWE NA UPEO WA UANDISHI MTAFARUKU KWA JAMII USIZIDI KUA TETE NA PIA KUA BEGA KWA BEGA KAMA WA TANZANIA CHINI YA BALOZI ZETU HIVYO BORA VYAMA VYETU VISIWEPO KABISA HUKU NJE YA NCHI KAMA CHAMA TUKAPIGIANE KELELE NYUMBANI KWANI LAZIMA TUWE WAJANJA WALE WATU NYUMBANI WA VYAMA WASITUYUMBISHE HUKU NA IMEKUA BAHATI DIASPORA IMETULETEA NSSF BILA YA HIVYO MAITI ZETU ZINGEOZEA HUKU KWA KUNGOJA MICHANGO NA HILI BALAA LILILO ANZA LA VYAMA VYA SIASA WATU WATAANZA AAAH ALOKUFA CHADEMA AU CCM JAMANI NA WASIHI TUACHANE NA MAMBO YA VYAMA HAPA MAREKANI TUWE NA JUMUIYA TU YA WA TANZANIA VYAMA NI SAWA NA UKABILA MUASISI WETU TEACHER ALISTUKIA HAYO SHIME SHIME HIVI SASA TUNA JAMBO MOJA ZITO LA MUUNGANO NDIO LA KULIJADILI KWANI UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU MWENYE KUTAKA CHAMA ARUDI NYUMBANI AKA ZUGE HUKO TUNATAKA KUPUMUA MAREKANI MAJUNGU NYUMBANI KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI NA VYAMA VINGINE VYA SIASA KWA MICHANGO YAO AHSANTENI

Anonymous said...

yaonyesha hapa naongea na wale wanaopenda muziki wa bure, chakula cha bure na na shoo za bure , sio mbaya mkaendelea na hayo mawazo yenu ya vya bure, lakini kwa usemiwa kuwa kufika amerika ndio degree hongereni sana maana sikujua hilo hata kidogo, nyie ndio wale ambao mlibahatika kupata elimu ya bure ya UPE????

INAONYESHA KWELI MLIFUTA UJINGA MAPEMA MAANA MLISOMESHWA BURE WAKATI WA MWALIMU, SIDHANI HATA KAMA MWALIMU AKIFUFULIWA LEO AKASIKIA NYIE MLIOKO HUKU USA MNASEMA KUFIKA AMERICA NDIO DEGREE NAFIKILI MZEE WA WATU ATAJUTA KWANINI ALIWAPA ELIMU YA BURE.

KWELI KWA KARNE HII YA LEO BADO TUNA WATU WANA FIKRA FINYU KUWA KUISHI AMERIKA NA KULIPA BILI TAYARI WEWE UMESHAKUWA NA MASTERS. HAWA NDIO WANAOTAFUTA UONGOZI NA KISHA KUWAAMBIA WATANZANIA NILISOMA AMERICA NA NINA MASTERS.

MMENIFUNGUA MACHO SANA MAANA HATA NDANI YA CHAMA CHENYEWE KUNA WATU WA JIITA MADOCTOR PHD.HOLDER NA WALA HATA DEGREE YA PILI HAWANA. NAMKUMBUKA MAREHEMU LAWRENCE GAMA ALIPOSEMA KUWA WATU WANATAFUTA UMAARUFU BILA KUUSOMEA.

SASA NYINYI WENYE MASTERS ZENU HUKU USA KWA KUWEZA KULIPA BILI NA KUISHI HUKU ,MKIRUDI NYUMBANI NAFIKILI NI KUWA MTAKUWA NA PHD .

HAITUSAIDII KUWA NA MATAWI HUKU NJE YA NCHI MAANA HUO NDIO MWANZO WA KULETA MIGOGORO NDANI YA JAMII YA WATANZANIA.TUIGE MAZURI KUTOKA KWA WENZETU MBONA WAO HAWANA UPUUZI HUU WA KIJINGA.

HAKUNA MTUA ANEWAKATAZA KUWA WA CCM OR KUWA WANA CHADEMA AU CUF LAKINI MAHALA PAKE MUAFAKA NI TANZANIA NDANI YA NCHI , HUKU NJE YA NCHI NI UGENINI TUNAGOMBEA NINI SASA HIVI, WAKATI WA UKOLONI UMESHAPITWA NA SASA TUNATAKIWA KUWA WATANZANIA KUURINDA UTANZANIA WETU. NYINYI WOTE MNAJIDAI NI WANA CCM , MBONA MNAKIMBILIA URAIA WA USA. KWANINI MSIBAKI NA UTANZANIA WETU. MNAJIITA WATANZANIA WAKATI MMESHAUKATAA UTANZANIA. ACHENI UNAFIKI KAMA MNAIPENDA NCHI YENU MNAWEZA KUUKANA UTANZANIAAAAAAAAA.

Anonymous said...

aise namuunga mkona benjamin chadomo kuingia hapa ni degree na kuishi ni master nikweli sana ifikiriyeni sana hii deep please msibeze please kwa sababu kuishi marekani si mchezo watanzania hatupendani hata kidogo najua mtawaona hawajasoma lakin fikiriyeni sana hii kitu kuishi hapa ni master na degree they are very right

Anonymous said...

MIE SIKUBALIANI NA HIZI IDEA ZA KUWA NA MATAWI HUKU AMERIKA.KINACHOFANYIKA HAPA NI WATU KUIPUNGUZIA NGUVU JUMUIYA YETU HUKU USA. WAKATI TULIKUWA HATUNA JUMUIYA KULIKUWAN HAKUNA MTU MWENYE MAWAZO YA KUFUNGUA HAYA MATAWI YAO.

KWELI NDIO SASA INAANZA , NA HILI LIMEANZA BAADA YA JUMUIYA KUPATA VIONGOZI HAPA DMV, HAWA WOTE WALIKUWA WAGOMBEA NDANI YA JUMUIYA BAADA YA KUSHINDWA WAKAONA SASA TUWE NA JUMUIYA YENU NYINGINE YA WATANZANIA. JEE KWANINI IMEANZA SASA BAADA YA JUMUIYA HII KUWA IMEKUFA KITAMBO, HAWA WANAOANZISHA HIZI CCM NA CHADEMA WANA AJENDA ZAO , HAWAITAKII MEMA JUMUIYA YETU HAPA DMV, HAIKATAZWI KUWA MWANACHAMA WA CHAMA CHAKO POPOTE PALE DUNIANI, LAKINI JEE KUNA UMUHIMU WA KUWA NA MASHINA HUKU NJE YA NCHI.HUKU NI KUTAFUTA MATATIZO. KULETA MATABAKA.

NDUGU ZANGU WATANZANIA TUNAPOELEKEA KUTAKUWA KUBAYA SANA KAMA HAYA MASHINA YATAENDELEA KUWAPO HUKU NJE KUNA SIKU WATU WATAKUJA KUJUTA MAANA WATAANZA KUNUNIANA.HILI LINAKUJA SASA HIVI KAMA KAULI ZA WATU HIZI ZA KUWA VYAMA NI MUHIMU SANA KULIKO UTANZANIA WETU. HII JUMUIYA NI YA WATANZANIA INGETOSHA SANA KUTUUNGANISHA WOTE BILA ITIKADI ZA VYAMA , LAKINI TUKISHAWEKA HIVI VYAMA NDANI YA HII JAMII YETU INAYOISHI HUKU DMV NA ULAYA NDIO MWANZO WA KULETA MIGOGORO.

MIE NINAVYOJUA SASA SIO SAA YA WATU KUPIGANIA UHURU.ZAMANI WATU WALIKUWA WANAKUTANA UGHAIBUNI WAKIWA WANASOMA NA WAKAWA NA MAWAZO YA KUPIGANIA UHURU, NA NDIO MAANA WASOMI WALIOKUWA NJE WALISAIDIA AFRICA KUWA HURU. SASA BAADA YA UHURU KUNAKUJA TENA VYAMA JAMANI, KWA FAIDA ZIPI AU KUTAFUTA KUJULIKANA NYUMBANI.

RUDINI NYUMBANI MKAGOMBEE KAMA KWELI MNAIPENDA NCHI YETU, SIO KUTULETEA MIGONGANO NDANI YA JUMUIYA YETU

Anonymous said...

labda ulikuwa huna camera benjamin ya kupiga picha kwenye capital hil etc ha ha ha a chadomo mkubwa darasa la saba

Anonymous said...

CCM OYYEEE, MIMI SIO MPENZI WA SIASA LAKINI BAADA YA KUWASIKILIZA HAWA JAMAA IMENIFANYA NITAKE CARD YA CCM.. MAISHA YANA STRESS HAWA WAPUMBAVU WAMENIFANYA NICHEKE... YAANI KUNA CHAMA KINA WAJINGA HIVI NA MIMI NAKITAKA...CCM OYEEE...HIKI NI CHAMA CHA SIASA GANI? CHA UJINGA AU UPUMBAVU? SIJAWAHI KUCHEKA KAMA LEO.. KUANZIA MUWAKILISHAJI WA CHAMA MPAKA REPORTER WOTE WAPUMBAVU WATUPU KAMA MAJUHA..AIBU TUPU KWA WATANZANIA...
KIKWETE AKIWASIKIA AU AKIONA LAZIMA AWAPELEKE HOSPITALI MIREMBE KWA MACHIZI WENZAO..HUYO KATIBU WA VIJANA KAMA YUKO MASKANI KAVUTA BANGI, REPORTER HAJUI TOFAUTI YA CHAMA NA JUMUIA.. BENJA WEWE NI SPECIAL CASE I LOVE YOU MAN.. ARE YOU SERIOUS?
END OF THE DAY MUMEIUZA CCM KWANGU NATAKA CARD YANGU NAKUJA TUVUTE WOTE BANGI HIYO TAREHE 25..CCM OYEE..Chama Cha Mataira DC.. na daimondo ndio raisi wetu..

Anonymous said...

God help us. Forgot about leading..I will never get in a car if one of these guys is driving.

Anonymous said...

mimi nadhanai hawa jamaa sio wa kulaumiwa maana wameishasema kuwa wao ni darasa la saba,so kichwani ni kama watoto wa darasa la saba,ila ninawashauri kuustarabika kidogo maana mmoja hapo naona ndevu zimejaa mvi so ni vizuri kuipa mvi heshima yake,nayo ni kuwa na busara

Anonymous said...

NAWAUNGA MKONO WOTE WANAOITAKIA AMANI NCHI YETU POPOTE PALE. NINAJIVUNIA UTANZANIA WANGU POPOTE PALE DUNIANI. NA NDIO MAANA NAONA SASA HAKUNA UMUHIMU WA KUWA NA HIVI VISHINA HUKU UGHAIBUNI.
WENZETU WAPALESTNA WANAKUWA NA OFISI ZAO NJE YA NCHI SIO KWA KUWA WANAPENDA NI KUWA BADO WANATAFUTA AMANI KWAO, HAWATUMII HAYO MATAWI YAO NJE YA NCHI KUWAGAWA WAO. HATA WAKATI WA ZAMA ZA UBAGUZI WA RANGI SOUTH AFRICA WAO WALIKUWA NA MATAWI YA NJE YA NCHI DUNIA NZIMA HATA TANZANIA WALIKUWA NAYO HUKO, MSUMBIJI , UINGEREZA NA HATA HUKU USA,... LAKINI BAADA YA UBAGUZI KUISHA SIJAWAI KUSIKIA KAMA WANA MATAWI NJE YA NCHI.

TATIZO LETU SISI WABONGO NI KUWA TUNATAFUTA UMAARUFU , MAANA WATU WANATAKA KUJULIKANA KWAA KUWAGAWA WATANZANIA NJE YA NCHI,INGEKUWA BUSARA KAMA WANGEJUA HUKU TUKO NCHI YA WATU. NA JEE WATU WANAJUA MADHUMUNI YA VYAMA VYA SIASA NINI. JEE VINAKUWA NA MATAWI NJE YA NCHI KWA SABABU ZIPI?????????????? HUKU TUNAKUWA NA JUMUIYA ZETU NA MNDIO MAANA ZINASAJILIWA KIHALALI,.. INAKUWAJE MNAKUWA NA MASHINA YA VYAMA HUKU WAKATI HAAKUNA KAZI YA SIASA HUKU TULIPO.MIE NAONA HAYA NI MAMBO YA KUJITAFUTIA UMAARUFU. NA NDIO MAANA UNAWAONA JAMAA WAMEKALIA KUITA WENGINE CHADOMO , HIYO YOTE WANATAKA KUJULIKANA NA SIO LINGINE. TATIZO HAPA NI KUJULIKANA NA KUJULIKANA KWA SIO KWA NIA NJEMA MAANA WANAWAGAWA WATANZANIA HUKU NJE KWA MISISNGI YA USHABIKI WA KISIASA,

MIE NAWASHAURI WALE AMBAO MLIKUWA MNATAKA UONGOZI NDANIYA JUMUIYA NA SAFARI HII HAMKUUPATA BADO MNAYO NAFASI YA KUISAIDIA JUMUIYA HAPA NDANI YA USA NA SIO KUANZISHA MATABAKA YA KISIASA.

HAIKATAZWI KUWA NA KADI YAKO YA CHAMA POPOTE PALE ULIMWENGUNI , LAKINI HUKU KUWA NA MASHINA TENA NA USHABIKI WA KUTOJUA UNAONGEA NINI UTATUFIKISHA KUBAYA, TUACHENI MAMBO YA SIASA HUKU NJE , TUNAITAJI KUWA NA JUMUIYA HAPA MOJA TU TENA IMARA NA NDIO MAANA WATU TULIJITOKEZA TUKAACHA KAZI ZETU KWENDA KUCHAGUA VIONGOZI WETU WATAKAOSIMAMIA JUMUIYA YETU. SASA KAMA KULIKUWA NA HAYO MA VYAMA YENU YALIKUWA WAPI SIKU ZOTE.

KAMA MWANZO ULIKUWA MBAYA NA WATU WAMEJARIBU KUREKEBISHA , KWANINI MNATAKA KUTUGAWA TENA. JAMANI TUACHIENI UMOJA WETU, WENYE KUTAKA SIASA HUKU UGENINI RUDINI NYUMBANI.KWANZA WENGI WENU UMESHAUKATAA URAIA WA TANZANIA SASA SIASA ZA BONGO ZINAWASAIDIA NINI JAMANI

Anonymous said...

nakujibu vizuri kufunguw matawi sio kosa bali lazima ujuwe kukaa huku ndiyo usahau nyumbani usije ukachanganya jumuiya na vyama chadema imefunguwa na ccm imefunguwa kwanza kabisa usisahau hili. Tunataka sana kuna na vyama hata kafu wakitaka pia wafungue maana tunataka tujuwe je nani ccm nani chadema na michango yetu ifike kwa walengwa ndiyo maana kuna katiba ya ccm inasema kuna matawi ya nje ya nchi sasa basi muelewe hamna alieyevunja katiba ya ccm wewe kwa nini unachukia vyama ? je ukiwa huku utakosowaje yale mabaya ya vyama vyetu mimi naona kabisa ni vizuri tuwe na vyama ni muhimu sana na pia ni vizuri kusaidia vyama vyetu muhimu tusigombane na tuwe tunasaidiana kama watanzania maana lengo la vyama vingi sio kutukanana bali ni kuelimishama na wote ni tunania nzuri kabisa sema tunatofautiana itikadi kwa hiyo ni vizuri kabisa kuwa na vyama nje ya nchi naona ni kitu kikubwa vyama kukubali kuweka matawi na tunataka tena tuweze kupiga kura 1015 kweli kabisa hili ni wazuri sana

Anonymous said...

ndugu yangu haujakatazwa kuwa cuf,ccm,chadema, suala hapa la kujiuliza jee hivi vyama vina umuhimu wa kuwa na haya mashina huku nje ya nchi, jee kwanini imetokea sasa hivi, ni kwa sababu zipi.

tunajifunza nini na haya mashina, nionacho mie ni mwanzo wa kutengana na kuwa na matabaka.wenzetu wote wakiwa nje ya nchi wanakuwa wamoja , hayo mavyama yote yanafanyia siasa nyumbani maana huko ndiko kwenye uwanja wa kufanya hivyo.sasa wewe unasema haikatazwi kuwa na matawi nje ya nchi, kwa faida gani maana wengi wa watu walioko huku USA wengi wao wameshaukataa huo utanzania ni RAIA wa huku.
MIE NAONA NI NJIA YA KUTUGAWA NA KUUVUNJA UMOJA WETU.tulikuwa tumekaa kitambo hapa DC bila ya kuwa na uongozi wa jumuiya , sasa wazo la kufufua jumuiya limekuja na watu wakagombea na baada ya uchaguzi ndio mamboa ya kufungua haya matawi yanaanza.

mfano mdogo wa migongano ni angalia jumuiya inataka tarehe 25 kuwa mkusanyiko wa wana jumuiya na ccm nao wanataka kuwa na mkutano wao wa kufungua shina na kugawa kadi. sasa hapa si unaona ndio mwanzo wa migongano , na huu ndio mwanzo itafika wakati wa msiba na sherehe zingine , watu watasema mie siendi kwenye hu msiba kwa sababu jamaa ni wa chadema au sichangii kitu, hili linakuja na wenye upeo wa mbali tunaliona maana limeshaanza kuonekana.dalili ya watu kugombea uongozi na kushindwa na kisha kuanzisha jumuiya ingine kwa migongo ya vyama ni dalili ya watu kuwa wanapenda kuwa viongozi, na wanatafuta njia ya kupata umaarufu, hakuna mtu anaekatazwa kuwa mwana ccm au chadema lakini huku kuwa na matawi nje ya nchi ni kwa faida gani.

SIJAONA MATAIFA MENGINE AMBAYO YANAFANYA UPUMBAVU KAMA HUU, HUU NI UJINGA WA AKILI MAANA , INASAIDIA KULETA MATABAKA. NYUMBANI IMESHAANZA WALE CUF,WALE CCM.,WALE CHADEMA NA NDIO HATA WATU WANASHIRIKIANA HIVYO, SASA MNATAKA NA HAPA YAANZE, KAMA MNATAKA YAANZE HAYA MSIJE KUJUTA MBELE MAANA INAONYESHA AKILI NI NYWERE KILA MTU ANA ZAKE.

SIKUBALIANI NA HIZI SIASA ZA KIJINGA , UHURU TUMESHAPATA SASAHUKU NJE YA NCHI TUNATAKA HIVI VYAMA VYA NINI, WAZO LANGU NA USHAURI WANGU, MWENYE KUPENDA SIASA KWANINI USIRUDI NYUMBANI KUGOMBEA MAANA KWANZA BONGO KUNA WATU WENGI AMBAO HAWAJASOMA NA WANAHITAJI WALIOSOMA WAWAONGOZE LAKINI HUKU TULIPO SIO MAHALA PA KUFANYA SIASA JAMANI. SIASA ZITATUGAWANYA MUDA SI MREFU.

IDUMU JUMUIYA YA WATANZANIA DMV, TUIPE SAPOTI, TUICHANGIE IWEZE KUFANYA KAZI ZAKE, TUACHANE NA HAYA MAVYAMA MAANA NDIO MWANZO WA MIGONGANO KATI YETU

kazimoto said...

Hawa watu Wa ccm ni wapuuzi Wa kupindukia hawana mwelekeo wala Sera za thati za kupambana na haRi mbaya ya umaskini inayoendelea Tanzania ni majitu yasiyojitambua nini yanatakiwa kufanya. What I can say chadema mwendo mdundo.