Yanga
wakishangilia Kombe lao baada ya kukabidhiwa
Kiiza
akishangilia bao la kwanza alilofunga dakika ya 44
Wachezaji wa Yanga
wakishangilia bao la kuongoza
Said Bahanuz wa Yanga akimtoka
Beki wa Azam,Aggrey Moris.
Mshambuliaji wa Yanga,Hamis
Kiiza akiondoka na mpira huku mlinzi wa Azam,Jabir Aziz akimkimbiza kwa kutaka
kumzuia mshambuliaji huyo.
Mlinzi wa timu ya Azam,Said
Moradi akiwania mpira na Mshambuliaji wa Timu ya Yanga,Said Bahanuz wakati wa
mchezo wa fainali ya Mashindano ya Cecafa Kagame cup.
Mashabiki nao hawakua nyuma
wakati wa ushangiliaji
YANGA ya Dar es Salaam imetwaa
Kombe la Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam, baada ya kuifunga Azam FC mabao
2-0.
Yanga sasa imebakiza mara moja
kufikisha idadi sawa na wapinzani wao wa jadi, Simba kutwaa Kombe hilo, mara
tano kwa sita. Yanga ilibeba taji hilo 1975, 1993, 1999, 2011 na
2012.
Mashujaa wa Yanga leo walikuwa
Hamisi Kiiza aliyefunga bao la kwanza dakika ya 44 na Said Bahanuzi aliyefunga
la pili dakika ya tatu ya muda nyongeza, baada ya kutimu dakika 90 za mechi
hiyo.
Kiiza alifunga bao lake, baada
ya kuuwahi mpira uliookolewa na kipa Deo Munishi ‘Dida’ na kumpiga chenga kipa
huyo kisha kuusukuma mpira nyavuni.
Bahanuzi aliuwahi mpira mrefu
uliopigwa na beki Oscar Joshua na kuwazidi ujanja mabeki wa Azam kabla ya
kumtungua Dida.
Mechi hiyo imechezeshwa vema na
refa Thierry Nkurunzinza kutoka Burundi, akisaidiwa na Simba Honore wa Rwanda na
Peter Sabatia wa Kenya, wakati mezani atakaa Issa Kagabo wa Rwanda, Kamisaa
Hassan Amir wa Somalia na Mtathmini wa marefa ni Anangwe Robert wa
Kenya.
Katika mchezo uliotangulia wa
kusaka mshindi wa tatu, AS ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) iliifunga
APR ya Rwanda mabao 2-1, mabao yake yakifungwa na Magola Mapanda dakika ya 18 na
Mutombo Kazadi dakika ya 67, wakati la kufutia machozi la timu ya jeshi la
Rwanda, lilifungwa na Jean Mugiraneza dakika ya 89.
Magoli mawili
yaliyopachikwa wavuni na washambuliaji wa Yanga Hamisi Kiiza katika dakika ya 44
kipindi cha kwanza na lile la Said Bahanuzi katika dakika ya 90 ya mchezo
yameiwezesha Yanga kuibuka Mabingwa tena wa Kombe la Kagame 2012 baada ya
kuchapa bila huruma mahasimu wao Azam FC kwa goli 2-0, katika mchezo wa fainali
uliochezwa leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Tanzania ijnakila sababu ya
kujivunia ushindi huo wa Yanga na nafasi ya pili ya Azam katika michuano hiyo ya
mwaka huu ambapo Tanzania kama mwenyeji wa michuani huyo iliingiza timu 4
zikiwapo za Simba na Mafunzo zilizotolewa katika hatua ya robo
fainali.
Yanga pia waliutumia mchezo
wa leo kulipiza kisasi cha kufungwa goli 3-1 na Azam katika mchezo wao wa Ligi
Kuu msimu uliopita na kupelekea wachezaji kadhaa wa Yanga kufungiwa baada ya
kushambulia mwamuzi kwa ngumi.
No comments:
Post a Comment