Prof. Mahalu (kushoto) akizungumza na Mwanasheria Alex Mgongolwa kwenye viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika siku mojawapo ya kusikilizwa kwa kesi yake. |
Balozi wa zamani wa Tanzania nchini
Italia, Prof.Costa Ricky Mahalu (63), ameachiwa huru mchana huu na
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo baada ya kuonekana kuwa hana hatia
katika kesi iliyokuwa ikimkabili yeye na afisa ubalozi Grace Martin, ya
kuisababishia serikali hasara ya euro 2,065,827.60.
Akitoa hukumu yake, Hakimu Mkazi Mfawidhi Illivin Mgeta amesema kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kutoa ushahidi wa kutosha kiasi cha kuwatia hatiani washtakiwa Mahalu na Grace.
Awali, hukumu ya kesi hiyo iliahirishwa mwezi uliopita na Hakimu Katemana, kwa maelezo kuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Mgeta aliyekuwa akiisikiliza kesi hiyo kukosekana kwavile alikuwa akikabiliwa na majukumu mengine.
Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka uliokuwa ukiongozwa na mawakili waandamizi wa serikali, Ponsiano Lukosi, Vincent Haule na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ben Linkolin, uliita mashahidi saba na vielelezo tisa vikiwemo mikataba miwili ya ununuzi wa jengo la ubalozi jijini Rome, Italia na upande wa utetezi uliita mashahidi watatu, akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa.

Aliyekuwa
Balozi wa Tanzania nchini Italia, Prof. Costa Mahalu akikumbatiana kwa
furaha na mdogo wake Vilasi Rama baada Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
jijini Dar es salaam leo, kumuachia huru katika kesi ya kuhujumu uchumi
iliyokuwa ikimkabili. (Picha na Daniel Mwita).
Prof.Costa
Mahalu katikati akitoka nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini
Dar es salaam huku akiongozana na wakili wake, Mabere Marando (kushoto).
Prof.Costa Mahalu akipeana mkono na ndugu na jamaa waliofika mahakamani hapo wakati wa hukumu.
Aliyekuwa Ofisa utawala katika ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Grace Martin akitoka Mahakamani.
1 comment:
haleluya mkuu jiunga na chadema sasa kwa sababu hawampendi kikwete
Post a Comment