Kushoto ni Katibu wa CCM DMV Jacob Kinyemi akiongea jambo na kumkaribisha mwenyekiti wa CCM DMV Loveness Mamuya ili awasalimie Watanzania waliojumuika pamoja kwenye Futari ya pamoja iliyotayarishwa na CCM DMV siku ya Ijumaa Aug 3, 2012 Hillandale Park iliyopo Silver Spring, Maryland. Futari hiyo ilianza kwa swala ya magharibi.
Watanzania wa DMV na marafiki zao wakijumuika pamoja kwenye futari ya pamoja iliyoandaliwa na CCM DMV Hillandale Park.
Watanzania wakipata picha ya pamoja walipojumuika pamoja katika futari ya pamoja iliyofanyikia Hillandale Park Silver Spring, Maryland.
Watanzania na marafiki zao wakiwa wamechukua chakula huku wakibadilishana mawili matatu katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na CCM DMV.
Nguo za rangi ya kijani na njano ndizo nyingi zilizokua zimetawala ndani ya ukumbi wa Hillandale Park katika futari ya pamoja iliyotayarishwa na CCM DMV.
Watanzania waliojumuika pamoja katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na CCM DMV wakiwa kwenye mstari wa kuchukua chakula.
Watanzania na marafiki zao wakiwa kwenye futari ya pamoja.
Watanzania waliojumuika pamoja katika Futari iliyoandaliwa na CCM DMV wakipakua chakula
Wakina mama na watoto wao wakiwa kwenye mjumuiko huo wa futari ya pamoja.
Sheh Omar akiwa nae kwenye Futari hiyo.
Kwa picha zaidi bofya read more
25 comments:
Naona watu wamekuja kutafuta maslai. Huwezi kumtumia mungu kwa manufaa ya Chama. Unawafutarusha watu huku unataka kueneza itikadi za Chama. Jembe hapo ni Saidi Mwamende naona anakamata futari na alama ya CHADEMA. Big up kamanda said- Lucas ukibana hii comment naupeleka huu Uzi jamiiforums na Facebook
Dj Luka Mbona hatukuoni?
asalaam aleikum... mimi natuma comment hii na kama utaitia au hutii wewe na mungu wako... Huu ni mwezi mtukufu wa ramadhani kwa waislam, quraani ilishushwa mwezi huu na waislamu wanafanya ibada..sio vizuri kuutumia kwa faida binafsi especially siasa...mnamchezea mwenyezi mungu? na asilimia kubwa waliokuwepo hapo ni wakiristo, na haifai kufungua saumu na wasio wasiofunga kwani kufungua malaika huwa wanazunguka kuchukua ibada... sasa nawaombeni tuziheshimu dini za watu...asante
wakristo kuja kufturu si ubaya, ndio kuna onyesha uislam hauna ubaguzi, kumsilimisha mtu ni thawabu kubwa na mtu hawezi kuslimu kama hajajichanganya na waislam akajua uislam unahusu nini.Ramadhan Kareem
Asante sana kwa maelezo yako. Naona kuna card zimeshikwa za CCM hii ilikuwa kufuturisha au campaign ya CCM? Kwakuwa hawapati watu kwenye mikutano Yao wanatumia futari ndo sehemu yake. Kwanini wanatumia dini yetu Kama bait? Si wangefanya party ya kugawa card na chakura . Kwanini wasiige makao makuu ya CCM kwani wao huwa wanachanganya misa za kanisani na kugawa card au kufuturisha na mambo ya Chama????
DJ Luke tafadhari weka comment yangu tunaelimishina hapa hamna cha chuki binafsi. Mimi ni mdau wako wa vijimambo number1 unanitibuwa sometimes unavobania comment za maana. Nashukuru ulivoruhusu hiyo ya juu.
Sisi em kweli mnaajenda kali, mpaka ugaibuni mnanunua watu kwa wali!!!
nakubalika naye sana mdau wa mwisho alicho sema na nakushukuru sana tena sana dj luke kwa kuweka comment yake, nikweli wameshazoea kuchezea dini ya wenzao na kuona kitu simple and they are not seriously halafu tunasema tanzania tuna amani, amani imetoka kwa waislamu wamevumilia sana toka ukoloni mpaka kupata uhuru kwa vile waislamu hawajadai haki zao wameka kimya na kuwa wanyonge na wapole daima ndo maana wenzetu wanatupanda kichwani na kutufanya wapumbavu.
hivi kweli usiyefunga uje ufutari? kwani unaona sisi tumo katika mchezo mchezo katika mwezi huu?
Naomba Luka usiache kueka hii comment.Mimi ni muislam Niupotoshaji sana dini yetu ya kislam ni dini ya upendo mkubwa mwezi huu mtukufu ni baraka kubwa kwa mtu yoyote kujitolea sadaka ,kula pamoja ndiyo maana futari inaliwa njee na hanyimwi mtu kula Futari muhimu kuzingatia kufunika kichwa kwa wanawake Futari inaliwa njee na watu wote Laah umefunga au ujafunga ni wewe na mungu wako lakini tunapaswa kufunga waislam wote na kama haufungi basi unatoa sadaka na kufuturisha kwa wingi na kusaidia yatima ,kwa hili naomba tusipoteze jamii na maadili ya dini asante bwana Luka Ramadhani kareem
FUNGA SI KUJIZUIYA KULA NA KUNYWA TU, KUNA MAMBO MENGI AMBAYO HATUYAZINGATII, WENGI WANAFAHAMU KUFUNGA NI KUJIZUIYA KULA NA KUNYWA, HAPA NATAKA KUONGELEA FUTARI, SI KILA MWENYE KUFUTARISHA IMEKUWA FUTARI ( namaanisha kuwa futari ya halal, vipi ilivyopatikana na uhalali wake)KAMA ULIWEZA KUFUNGA UKAJIZUIA KULA NA KUNYWA NA MAMBOMENGINE YENYE KUBATILISHA SWAUM, PIA IANGALIE SANA FUTARI UNAYOFUNGULIA SWAUM YAKO ILI IWE MAKBUL,WAISLAM HILO NI CHANGA LA MACHO TUWE MAKINI NA MAMBO YA USHABIKI AU KUMRIDHISHA MTU KATIKA DINI HATUNA VITU KAMA HIVYO KAMA JAMBO NI LA KUMUGHASI MWENYEZI MUNGU HATA KAMA BABA YAKO UNAWEZA KUMKATALIA, HAKA KAMA BABA YAKO UNAJUA FUTARI ALIOILETA NYUMBANI SI HALALI UNAWEZA KUIKATAA.
TUJIEPUSHENI JAMANI NA HAYA MAMBO YANAYOJITOKEZA SASA TUTAKUJA KUWA NI WENYE KUJUTA SIKU YA SIKU, TULIKUWA TUNAFUNGA, LAKINI SWAUM ZETU NI BURE TUTOKANA NA MAMBO KAMA HAYA. WAISLAM KUWENI MAKINI.
Mshamba wewe huna lolote
hujaiweka comment yangu na hapa pia sawa mkuu lakini namunga mkono mdau wa mwisho watu hawakufunga wanadijai kuanda futari mnafikir sisi tunacheka katika mwezi huu tunamuambudu mola wetu sio fashion za kufutarisha na kuimarisha chama tumeshaamka bwana
nyie ndio wachochezi wa dini ina maana malaika akipita akakuta wafuturu na wakristo hupati thawabu? nakubaliana na mambo ya siasa lakini hayo mengine achana nayo mwislam mwenzangu ndio nyinyi mnaofanya uislam uonekane mgumu. asalaam aleikum my sis or bro
Sasa jamani hii inakuwaje wewe uliyeandika hapo juu sijui unawaza nini?hivi ukiangalia hapo wakristu ndiyo wengi au tu jaziba zako?swali langu ni moja tu sasa mala nyingi sana hawa ndugu zetu huwa wanatualika kwenda kufuru nao pamoja sasa hiyo karibu ni ya kinafiki?au unataka kuwaambia nini watu wa mathehebu mengine.jamani tupendane mambo ya udini tuyaache tukifuata hivyo hatutafika .Dj Luke isibanie irushe tu
Nakubaliana na mwandishi wa hapo juu!msitumie mwezi huu mtukufu kwa michezo ya siasa! muogopeni mungu jamani dunia ya kupita tu hii.
DMV siasa itatupeleka kubaya miaka yooote tumeshirikiana kama watanzania PLEASE PLEASE PLEASE nyie mnaotafuta public office bongo kupitia watanzania wengi tuliokuja kutafuta maisha msituletee mgawanyiko. Kwanza kura zenyewe hatupigi huku nje kuna faida gani ya kupoteza muda wetu na mambo ya chama????? LETS BUILD A STRONG TANZANIA COMMUNITY ili tuweze kuleta maendeleo nyumbani. Na mdau hapo juu nakubali kabisa sisi waislamu tunayoijua dini yetu hatukusogea kwenye hili genge! Quran is very clear katika mambo ya ibada so please with due respect kabla ya kufanya mambo kama haya muwe munauliza watu wenye dini zao ili wawaelimishe. SIASA ZIKO BONGO HUKU NJE TUACHE MAJUNGU CHUKI NA MGAWANYIKO WA KISIASA MAANA TUNASIKIA JINSI GANI WATU WANATUKANANA NA KUDHALILISHANA NA HII IMEKUWA KAMA KITU CHA KAWAIDA HAPA DMV, ITS A SHAME! SISI NDIYO TUKO HAPA MAKAO MAKUU NA TUNATAKIWA TUWE NA MSHIKAMANO NA UPENDO BUT KUTWA WATU WANACHIMBANA MANENO LEO VYAMA VYA SIASA DMV WAKISIKIA JUMUIYA INAFANYA PARTY NA WAO WANATANGAZA PARTY SAME DAY! USTAARABU UKIONA MWENZAKO KATOA TANGAZO LA MKUTANO 0N AUGUST 25 WHY CANT YOU MOVE YOUR PARTY TO THE OTHER DATE???? KAMA KWELI TUNATAKA KUSHIRIKIANA THAN KUTENGANA??? Watu wa state zingine wanauliza hivi DMV kuna nini??????? I GAT NO DAMN ANSWER. JAMANU TUACHE UTOTO NA UBI-SHOW LETS ALL ACT MATURED (AGE APPROPRIATELY), LUCA USIIBANE WE NEED TO STOP THIS ENOUGH IS ENOUGH TUNATAKA UMOJA NA UPENDO.
AEISEE MDAU HAPO JUU NAKUBALIANA NA WEWE 100%.TUNATAKIWA KUENDELEZA JUMUHIA YA WATANZANIA DMV SIYO MNAANZA KUTULETEA UPUMBAVU WENUWA WA SIASA.TUNATAKA VIONGOZI WANAO NA WATAKAO INDELEZA NCHI SIYO KUIIBIA NCHI.
CCM Mmekosea , Mimi ni mkereketwa wa hapa DMV. Kufuturisha si Vibaya mbona mmefanya kama ushabiki?, Bendera, mavazi ya CCM, na vurugu tu. Mnawakosea waislamu na msitake kuleta ugomvi na chuki. Wewe Kinyemi ni Muislamu Huoni hata aibu. Mungu atakuuliza siku ya kiama unayoyafanya. Unawadhalilisha waislamu, kwa kutowaongoza viongozi wenzako wa CCM kwamba wangetaka kufuturisha wangefuturisha lakini sio kuleta Kebehi na ushabiki.
Kinyemi mungu anakuangalia ndie wewe kwenye uchaguzi wa DMV uliekuwa ukileta fitna za Kumsingizia Kaka wa Watu Iddi Sandaly, kuwa ni mdini maskini. Hivi unaelekea wapi. Kama unataka Madaraka Tanzania kwanini usiende nyumbani kaka?.
Kama Utasoma hii Comment naomba unipe majibu ya maswali haya . 1. Je CCM au CHADEMA itasaidia nini watanzania wanaoishi hapa? 2. Je wewe Kama Mwana CCM utasaidia kipi ambacho unaona Jumuia ya Watanzania DMV hawawezi kukifanya?
Mwisho nawaomba watanzania wenzangu tuwemakini na haya jamani.
Napenda kuchangia katika hili. lazima tuelewa haya mambo yanaonyesha watanzania washio USA wamepoteza muelekeo au wamefia upeo wa kufikiri,wale wanasiasa wa Tanzania wameshindwa kuleta maendeleo nyumbania Tanzania na nyie mlioko huku mnaingia kwenye mzunguko huohuo sasa kuna faida gani kuwepo marekani na mawazo yako na mipango yako inafanana na mtu aliye Bongo ambaye hajui nini maana ya kujikwamua kimaendeleo. Dj Luke lazima turuhusu maojiano haya hili tuweze kutoka hapa tulipo. Ahsante
Swadakta!!!! well said hapo juu. WHAT R WE REALLY GETING OUT OF VYAMA HUKU UGHAIBUNI??? HAWA WANATAKA KUTUTUMIA KUJITANGAZA KWA VIONGOZI WA VYAMA BONGO ILI WAPEWE MADARAKA YALE YA KUTEULIWA FROM NOWHERE U JUST WATCH. PEOPLE WAKE UP..UMOJA WA TANZANIA NDIYO CHOMBO KITAKACHOTUJUMUISHA SOTE BILA DINI WALA ITIKADI.
Kwa kweli wewe luka unapaswa kuwa mkweli hizi comment unaziweka ili watu wachukiane au unafanya hivi kwa sababu wewe ni chadema ?Halafu mkae mkijuwa mnapata dhambi kubwa nendeni mkaaone Artel walikuwa wanafuturisha wateja wao wale walikuwa ni wakristo kwa nini wewe uchukie ccm kufuturisha mavazi ni ushabiki wa mtu pale ilipikwa futari na sio kuuza kadi wale walioshika kadi ni ushabiki wao angalia picha vizuri waislam walikuwa wengi kuliko wakristo shame on you yote haya kisa ccm walikuepo ingekuwa wengine msinge sema kitu acheni unafki nyie watu hampendi siasa kaeni pembeni
Luka kama unajuwa uongozi ulishapita leo hii kwa nini unaruhusu comment ya kumtukana kinyemi na idd wewe hauoni ni uchonganishi?? wewe kama mwenye blog lazima ujuwe nini cha kuweka sio kuchonganisha jamii huu sio muda wa kampeni luka ujafanya vizuri kaka hope umenielewa kwanza kuweka comment za kidini ni uchonganishi mkubwa kwa jamii nadhani ujaweka kwa kujenga bali unabomoa sio vizuri hii uchonganishi mbona zamani ulikuwa hauweki comment??unatakiwa uwe kiongo kwa jamii uweke habari za maana sio kuwachonganisha jamii hii unaimanisha nini ??kwa jamii kumbuka siasa itakuepo utake usitake
namshukuru dj luke kuziruhusu hizi comments zote kwa uhuru na uwazi! maana kunakipindi ulikuwa huruhusu comments za watu wakiwa na idia tofauti au mawazo tofauti mnawaona kama wakorofi.ni uhuru wa habari tu! im just sayying
Mimi namtetea sana kaka luke... Huyu ni mtu mmoja ambaye anakuja kufuturu na anaonyesha heshima katika dini ya kiislamu.. na yeye kuziweka comment hachonganishi ila anaweka hali halisi kwa hiyo muacheni mkaka wa watu... kitu kingine hapo ni sawa na msikitini sisi waislamu tuna masharti mengi ya dini kama huyo mwenyekiti wenu kushika mike ni dharau na utovu wa nidhamu.. Nyinyi kama muliamua kutoa sadaka mungewakabithi wakuu wa tamko sio kuja kucheza ngoma za ccm na malemba yenu... kinachosikitisha ni waislamu wanafiki waliochangia.. Kwenye Quraan imeandikwa msiiuze dini yenu kwa thamani duni kwani ni dhambi kubwa na malipo yake ni moto mkubwa.
hamjakatazwa kuja kuomba ibada lakini muwe mumeamini.. na kuleta chakula pale sio sababu ya nyinyi kuja sisi tunakula halal.. tunawaomba tu muiheshimu dini yetu kama sisi tunavyoheshimu yenu..Na kama ccm mnataka kampeni fanyeni kwengine sio sehemu ya ibada..tuombeni msamaha kwa mola wetu na tuacheni tabia hii chafu na ni ukosefu wa ustaarabu tu..
Na nyinyi waislamu munaoshabikia tabia hii mnaudhalilisha uislamu so Shame on you.. sisi hatuendi kwenye misa jumapili tumevaa kiislamu kwa sababu tunaheshimu dini za wenzetu.
Na nyinyi wanasiasa wa DMV wacheni kuchemsha hivi ni muko that Desperate? Hivi CCM na chama chenu mtanifanyia nini hapa marekani?
Naomba sana Dj Luke asiwekwe kwenye hizi hoja yeye amemaliza majukumu yake wekeni hoja zenu. Kwanza napenda kuwapongeza uongozi wa Kihislam hapa DMV kwa kazi nzuri"mimi ni mkristo" mnayoifanya,lakini inaonyesha kidogo mnaanza kupoteza muelekeo miaka yote mmefanya vitu vizuri kwa pamoja leo mnakuja kuruhusu Kejeli,Dharau,kebehi kwa ajili ya chakula cha siasa hamuini kwamba hii ni aibu si kwenu hata MOLA unamuaibisha,msitafute mchawi nyie ndio wachawi wenyewe. Bongo watu wananunuliwa kwa upande wa khanga na pilau sasa na nyie wa USA ni hivyohivyo sasa kuna tofauti gani ya kukaa hapa kama unatofauti na mtu aliyeupo kule Bagamoyo kijijini? DJ Luke ahsante kwa Bunge lako hulu
Usiulaumu uongozi wa Kiislamu. Hawa hawakushirikiana na TAMCO hata kidogo. Kama wewe unawajuwa TAMCO umemuona kiongozi yeyote wa TAMCO kwenye picha hizo ? AU umewaona Wanatamca halisi hapo kwenye picha ?. TAMCO wako makini sana hawawezi kuingia kwenye mtego huu wa kitoto.
Post a Comment