ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 1, 2012

EXCLUSIVE: NGASSA AFUNGUKA: SINA TAARIFA RASMI JUU YA KUUZWA SIMBA - AZAM WAFUATE TARATIBU













Muda mchache uliopita tumefanikiwa kufanya mazungumzo na mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Mrisho Ngassa ambaye klabu yake Azam leo imethibitisha kwamba ameuzwa kwenda klabu ya Simba.


Katika mazungumzo hayo Mrisho Ngassa amesema kwamba yeye binafsi hajapata taarifa rasmi kutoka kwa klabu yake ya Azam juu ya kuuzwa kwenda Simba. "Kiukweli hizo taarifa mie nazisikia na kusoma kwenye mitandao tofauti lakini muajiri wangu bado hajanipa taarifa rasmi juu ya hili suala. Pia huu utaratibu sidhani kama ni sahihi, wanawezaje kuniuza timu nyingine bila kunihusisha, vipi kuhusu maslahi yangu katika hiyo timu nyingine nani ameyasimamia? Kwa maana hii bado nashindwa kuamini kama Azam watakuwa wamefanya hivyo. Ilipaswa wanipe taarifa kwamba Ngassa tunakuuza kwenda timu fulani na nina haki ya kuchagua kukubali au kukataa.

Ngassa akaendelea alivyoondoka Yanga, "Mimi sitaki kuondoka Azam huku kukiwa kuna hali ya kutokuelewana kati yangu na wao pamoja na wapenzi na mshabiki wa klabu hiyo ambao wamekuwa wakinisapoti kwenye kipindi chote nilichokaa pale. Unaweza ukajiuliza kwanini mimi mpaka leo kwanini mashabiki wa Yanga wanaonyesha mapenzi kwangu au ninakuwa na ukaribu nao, ni kwa sababu wakati naondoka Yanga nilipewa baraka zote na klabu yangu, yaani niliondoka vizuri. Azam walikuja wakaongea na Yanga wakakubaliana na ada ya uhamisho then na mie nikapewa taarifa nikakaa chini na Azam tukakubalina mahitaji yangu binafsi sasa iweje leo wao wameshindwa kufuata utaratibu ule ule ambao waliufuata wakati wa kuninunua kutoka Yanga. Ilipaswa wao kabla ya kukubaliana na Simba ingebidi na mie nipewe taarifa ili kuweza kukubaliana mahitaji yangu binafsi na Simba then ndio niuzwe. lakini sivyo walivyofanya."

Alipoulizwa kama Simba wakimpa vile anavyovitaka atakuwa tayari kuichezea klabu hiyo, Ngassa alijibu, "Mpira ni kazi yangu, ninafanya hii kazi ili kuweza kujikimu kimaisha maisha. Kama klabu yoyote ikikubali kunipa mahitaji yangu niyatakayo na nikapendezewa nayo nitajiunga nayo. Taratibu lazima zifuatwe na kuniuza kama kiroba cha mchele, kwa hali ilivyo mpaka sasa sitoweza kujiunga na Simba"
Bofya hapo kumsikiliza Mrisho Ngassa


By Aidan Charlie

1 comment:

Anonymous said...

Kwa mtaji huu Simba watabaki kuwa vibonde tu. Sasa Ngassa ana mpira gani mpaka anunuliwe na Simba?