Mtaalamu
maswala ya umeme Joseph Matwani akiwaelezea baadhi ya wananchi
waliotembele banda hilo jinzi kifaa hicho kinavyofanyakazi
MWANAFUNZI
wa Chuo kikuu cha sayansi na teknolojia Mbeya (MIST) amebuni na
kutengeneza kifaa maalum kinachodaiwa kuweza kudhibiti kupunguza na
ikiwezekana kumaliza kabisa tatizo la ajali za vyombo vya usafiri wa
bahari kama ilivyotokea hivi karibuni kwa Meli ya Mv.Skargit
iliyogharimu maisha ya watanzania wengi.
Akizungumza
na Mbeya yetu Mtaalamu wa masuala ya umeme katika chuo hicho,Joseph
Matwani amemtaja mwanafunzi aliyekitengeneza kifaa hicho ambacho
kinabaini meli ama boti litakalozidisha abiria ama mizigo kuwa ni
Zuberi Rutumbo.
Bw.Matwani
alisema kifaa hicho ambacho bado akijapewa jina kitakuwa na uwezo wa
kutoa taarifa katika mamlaka husika mathalani,Sumatra,Polisi,kwa
mmiliki,nahodha na mamlaka nyinginezo zitakazoingizwa katika programu
maalum kuwa meli Fulani imejaza mzigo kuliko uwezo wake na hivyo
kusaidia kuizuia bandarini kabla haijaondoka.
Mtaalamu
huyo amesema kuwa kifaa hicho kitafungwa katika vyombo mbalimbali vya
usafiri wa baharini ambapo vitawaonesha makapteni kuona kiasi cha mzigo
uliopakiwa na kuwajulisha endapo watazidisha baada ya maji kuvuka
mstari wa chombo husikai kabla ya kuondoka na hivyo kutoa mlio wa
taadhari na baada ya sekunde kumia ujumbe unakwenda katika nambari za
simu zilizokuwa zimefanyiwa programu katika kadi ya simu
.
Amesema
kutokana na taarifa hiyo ya ujmbe mfupi wa maneno katika simu za
wahusika wanatumaini kuwa watachukuwa hatua kukizuia chombo hicho
kisiondoke na hivyo kufanikiwa kunusuru maisha ya abiria na kupunguza
ajali zinazodaiwa zinasababishwa na uzembe wa makapteni kuzidisha mzigo
kwa makusudi.
Mvumbuzi
huyo Rutumbo amesema ameamua kutengeneza kifaa hicho alichoanza
kukifikiria tangu mwaka 2011 baada ya kuibuka kwa ajali mbaya za meli
ya Mv.Bukoba,Mv.Spice na juzi Mv.Skargit na hivyo kuamua kuandika
‘project’ ( mradi) baada ya kushuhudia matukio hayo.
Amesema
ajali nyingi zinaonekana zinasababishwa na uzembe wa watu wachache waio
na huruma na watanzania lakini anaamini kupitia kifaa hicho uwajibikaji
utaongezeka na kila mmoja atawajibika kupitia nafasi yake na kuwabaini
wazembe ambapo pia kifaa hicho kinaweza kufungwa katika mlango ama
dirisha katika nyumba na kuprogramu katika simu na hivyo kukupa taarifa
ya uhalifu endapo unatokea.
|
2 comments:
sasa tusiite kuvumbua kwani wazungu wanavyo siku nyingi sana tu, tuseme kaweza kutengeza kutumia njia ya kuunganisha unganisha isiyo ya kitaalam zaidi.
uvumbuzi ni pale ambapo kitu hicho ni cha kipekee na hakijawahi kutokea.
Hongera na pongezi zimfikie mwanafunzi huyu kwa kuvumbua kifaa kipya tena katika kipindi cha uhitaji mkubwa kutokana na takwimu za ajali za majini kuongezeka.Haya ni maarifa makubwa kwa ngazi yako na kwa taifa pia.Watu kama hawa wanatakiwa kuwa recognized na pia vipaji vyao viendelezwe kwa gharama yoyote.Nchi zilizoendelea walianza hivi na ndio maana hata sasa watu wenye vipaji maalumu wamekuwa wakinunuliwa kwa njia nyingi ili kufanikisha nchi zilizoendelea ni wakati wetu sasa kuthamini vipaji hivi kwa ajili ya manufaa ya nchi yetu.
Post a Comment