Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais- Asiye na Wizara Maalumu Prof, Mark Mwandosya akitoa shukurani Aug,1,2012 kwa Serikali na Wananchi waliomuombea wakati akiwa mgojwa hadi kupata nafuu na kuweza kuhudhuria tena katika vikao vya Bunge ,mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi wa Rais (Asiye na Wizara Maalum), Profesa Mark Mwandosya, amerejea bungeni baada ya mwaka mmoja tangu alipoanza kuumwa na kusema ameuona mkono wa Mungu katika uponyaji wake.
Profesa Mwandosya ambaye aliingia bungeni jana muda mfupi kabla ya Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kusoma hotuba ya bajeti yake, alionekana kuwa na afya njema ambapo aliweza kutembea mwenyewe bila msaada wa mtu.
Mara tu alipotokeza kwenye lango la kuingilia ndani ya Bunge, akiwa amevaa safari suti yenye rangi bluu iliyoiva, wabunge wote walianza kushangilia kwa makofi na vigelegele, jambo ambalo lilimfanya Mwenyekiti wa Bunge, Jenista Mhagama, kumwambia Dk. Mwakyembe asimame kwa muda ili aeleze vifijo na nderemo hizo zilisababishwa na nini.
Mhagama aliwambia wabunge na Watanzania kuwa Bunge lilizizima kwa sababu ya kurejea kwa Profesa Mwandosya bungeni.
Baada ya ufafanuzi huo, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye alikuwa akikaimu nafasi ya kiongozi wa shughuli za serikali bungeni, Samuel Sitta, alitoa hoja ya kutaka Profesa Mwandosya apewe muda wa kusema kidogo ndani ya Bunge.
“Naomba umruhusu aseme maneno machache kwa sababu siku nyingi hatujamuona, naomba kutoa hoja,” alisema Sitta na kuungwa mkono na wabunge wengi na Mhagama kukubali hoja yake ya kuruhusu mambo ambayo hayajawekewa utaratibu kwa kujibu wa kanuni namba 5 (1).
Profesa Mwandosya alisema: “Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa rehema zake kubwa, sikutegemea, lakini imetokea na naona mkono wake Mungu katika uponyaji wangu,” alisema na kuongeza:
“Ni zaidi ya mwaka tangu nimekwenda kwa ajili ya matibabu na sijazungumza katika Bunge hili tukufu.”
“Na moja ya mambo ambayo nilikuwa ninasema mbona ungenirudishia hata kama kwa dakika tano nije kuongea na wabunge wenzangu na mwenyezi Mungu ameridhia ombi langu naomba nitoe shukurani nyangu sana kutoka moyoni kwa Watanzania wote, kumbe ukiugua hakuna chama hamna CCM wala Chadema wala TLP wala chama chochote unakuwa Mtanzania wa kawaida,” alisema.
Aliwashukuru Watanzania wote na kuongeza kuwa anamshukuru sana Rais Jakaya Kikwete ambaye alisisitiza kuwa afya yake ni jambo muhimu sana na kumtaka kuondoka kwenda kutibiwa.
Aliwashukuru viongozi wa juu wa serikali na vyama akiwemo Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Umoja ya ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
“Mimi miaka 45 sijawahi kuona kitanda hospitali, nimekuja kukikuta huko Hyderabad Apollo ( Moja ya hospitali nchini India), nilidhani ni mtu wa afya sana, mtu wa mazoezi asubuhi na jioni, lakini kumbe mwili wa binadamu Mwenyezi Mungu alivyoumba ni maajabu yake mwenyewe,” alisema.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment